kajirita
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,575
- 637
TANGANYIKA ililetwa na Wajerumani na
kuendelezwa na Waingereza. Tanganyika ilizaliwa
pasipo Mtanganyika yoyote kuwepo, kuamua
nani awatawale, mfumo upi uwatawale, na
mipaka ya nchi hiyo iitwayo Tanganyika bali
mchakato ulitawaliwa na ulafi wa rasilimali na
ubepari pamoja European Nationalism. Na tangu
kuzaliwa kwake mwaka 1885 imekuwa ndani ya
ukoloni, unyonyaji, ubaguzi, matabaka na
utumwa mpaka mwaka 1918 ilipochukuliwa na
Waingereza na Waingereza hao kurithi mfumo
wenye tabia hiyo hiyo mpaka 1961. Kwa mantiki
ya kihisabati kuanzia mwaka 1885 mpaka 1961
ni miaka 76 na Mtanganyika aliyezaliwa ndani ya
Tanganyika amezeeka ndani ya maisha hayo na
hata wengine wamefariki wakiwa na tumaini
jipya la kuona utu na Uafrika wao uliochukuliwa
tangu miaka ya 1885 unarudi. Tumaini jipya la
kuona utu na Uafrika wao lilipatikana baada ya
kupata uhuru mwaka 1961 na kukamilika baada
ya Muungano na ndugu zao wa Zanzibar 1964.
Kihistoria na asili ya kuzaliwa kwa Tanganyika na
Zanzibar kama nilivyoeleza hapo nyuma
kulitenganisha ndugu, koo, jamii na jamaa
ambao kabla ya Mkutano wa Berlin walikuwa
wamoja, mfano huu unaweza kuonekana wazi
kupitia mipakani ambapo tunaweza kuona
Wamasai walio Kenya na Tanzania, Watu wa
Pwani walio Tanga na Pemba, Wahaya na
Waganda n.k na ukiangalia hata lugha
wanazozungumza zinaingiliana, zinafanana na
zaidi ni watu wenye asili inayofanana. Kama
ambavyo Mtanganyika na Mzanzibar aliyeishi
miaka 76 au zaidi ndani ya Ukoloni angesema,
kuidai, kuishadadia, kuishabikia, kujivunia au
kuitukuza Tanganyika au Zanzibar na kuibeza,
kuipuuza, kuiua, au kufanya vitu kuiua au
kuivuruga ni kurudisha ukoloni, ni mawazo ya
wakoloni au kupandikizwa na wakoloni kwa watu
wanaojivika ama uzawa ama uzalendo, ni
kuutukuza
ukoloni au kuwatukuza walioleta ukoloni zaidi ya
hapo ni kudai utumwa mana kwa Muafrika na
Mtanzania wa leo anayejitambua vizuri asingedai
tuu muungano wa Tanganyika na Zanzibar bali
Muungano wa Afrika nzima.
Mkuu,
Lengo la muungano huu ilikuwa si kuipata Tanzania tu Bali ilikuwa njia ya kuipata USA(United States of Africa).Lakini kwa kuwa wanasiasa wameshindwa kuja na mfumo wa kisiasa unaoleta usawa Kati ya Tanganyika na Zanzibar basi ni bora tu Tanganyika irudi tu labda tukikutana kwenye shirikisho malengo ya Afrika moja yatarudi tena.
Mwisho,tungekuwa na nia ya dhati na muungano tungeweka muungano wa serikali moja lakini mbili au tatu ni kudanganyana!
Asante!