Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...


Haitasaidia. Ukweli wa mambo is behind close doors.

Leo tunaongelea Udini, ukabila, ukanda CDM, kesho kesho kutwa tutaongelea mengine. Wewe subiri hujionee viroja juu ya viroja. Hili sijasema mimi wala sijalitaka mimi, ila ni sera na uongozi mmbovu wa ccm na serikali yake.


Harakati na hata hoja za siasa ndani ya Tanzania na CCM zitabadilika sana. Tegemea mabadiliko makubwa. Unajua kuwasha moto msitu ni rahisi sana ila kasheshe ipo kwenye kuuzima.

Subiri after 2015.
 
Hao wanaotaka kupitisha mambo ya chama chao kwa kisingizio cha maslahi ya taifa hawana chao. Kama kiongozi mkubwa kama Kificho anaitaka zanzibar yake tuyegemee nini? Tsnganyika inakuja
 

Wewe ni mtanganyika unaejielewa.
 
Eee Mola wangu, nisaidie na nijaalie nchi ya Tanganyika inikute nikiwa hai...aamin!
 
Mimi hawa wapemba na ardhi yetu huku boko bunju siwataki kabisa warudi kwao zenj haraka Tanganyika irudi bana.

Chuki zako ni kwa wapemba tu ila kwa wachina na makaburu wanao keketa tembo wenu poa tu.
 
Tunataka Tanganyika na Zanzibar huru.....unafiki wa viongozi wetu ndo umetufikisha hapa. Wametuongoza miaka 50 bila Tanganyika wamefeli nasi tunataka miaka 50 hii ya kizazi chetu tukiwa na Tanganyika.
 

Sio kweli kwamba Tanganyika ni jina lililotungwa na mkoloni; wajerumani walipoingia kama wakoloni waliita ardhi yetu pamoja na maeneo mengine ya karibu waliyo hodhi "german east africa; baada ya vita vya pili vya dunia kuisha na mjerumani kunyang'anywa makoloni yake, mwaka 1920 Mwingereza akachukua eneo husika; administrators wa kikoloni wakataka kulipa eneo husika majina yenye asili ya uingereza yanayofanania na Victoria na kaa hayo; utawala wa uingereza ukakataa na kuhimiza kwamba litafutwe jina ambalo asili yake ni ya eneo hilo hilo (indigenous name); yakafikiriwa mengine kama vile Tabora n.k, na hatimaye jina la Tanganyika likachaguliwa; jina hili lilikuwa linatumiwa na wenyeji wa maeneo ya Kigoma kabla hata ya ujio wa wakoloni;



Tanzania Kwanza,
Tanganyika Kabla

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

swala ni kuwa na usawa katika nchi tunayoishi. na sasa hivi Mzanzibari anahaki na kufaidika zaidi ya Mtanganyika. Nakama una akili kidogo utajua watu wanacho ongelea sio jina la nchi bali haki na uswa kwa kila mwananchi. Hata jina la Tanzania lilitungwa na muhindi na ndie unae muita baba yako. Nchi itajengwa baada ya kuifukuza miCCM na hatuitaji maombi wala kufunga mpendwa
 
Hakuna maneno yanayonitia kinyaa km "uhuru wa Tanzania bara"...najiuliza hii ndo nchi gani?na ilipata huo uhuru toka kwa nani?...ya kwangu mm ni TANGANYIKA tu full stop!...
...ooh Tanganyika,Tanganyika nakupenda kwa moyo wote
Tanganyika,Tanganyika jina lako ni tamu sana!
 

Sijakuelewa Hebu dadafua
 

Muungano upo ICU umebakia kofia tu ,Maana Zanzibar ana Katiba yake,wimbo,bendera zake sasa wanaandaa Sarafu zao ,Ardhi ni Mali yoa peke yao si ya Muungano ,Hawalipii Gharama za kuhudumia muungano,anayeng'ang'ania muungano kwa njia ya Kujipendekeza ni Tanganyika tu ! Kwani Zanzibar wamefanya Visa vingi wazi wazi ili Ndoa ivunjike lakini Tanganyika wameziba masikio na kufumba macho wanaubembeleza Muungano kwa Mamilioni ya fedha huku Huduma za jamii zakidumaa.. Tambua huu muungano kwa sasa hauna Faida kwa Tanganyika anayefaidika na matunda ya muungano ni Zanzibar .
 
Baada ya miaka 50 je unaweza kufukua kaburi na kutoa kitu kilicho hai? Je kurudi kwa Tanganyika kutasaidia kupunguza ukali wa maisha yetu ya kila siku ? Je ufisadi utapungua na raslimali zigawanyewe sawa kwa wote? Je Afya, Elimu, Makazi zitaboreswa?

Kama haya yatatekelezwa na nikihakikishiwa basi na mimi nitachukua jembe kwenda kusaidia kulifukua kaburi ili Tanganyika atoke akiwa hai
 
Jamani Tanganyika irudi isiwe kama ndege ya Malaysia iliyopotea! Come back Tanganyika, Come back again!
 
ili kubalance Haki kwa wale wanachunwa sasa yaani Tanganyika lazima Muungano utizamwe kwa Undani zaidi ili sasa uwe Muungano Digtal Kama wa kule Marekani ambapo kuna muungano wa Nchi 52 hawana kero za muungano wala wizara ya muungano , hata zile Nchi ndogo si tegemezi kwa Muungano wala hazina Utitiri wa Wabunge na viongozi wengi Kama Zanzibar. Zinachangia gharama za muungano bila tatizo , Hakuna ubaguzi wa Udini wala Uchoyo wa Ardhi ,tuige Mfano huu ili tuachane na Muungano wetu Analogia ambao Zanzibar analundika Viongozi kwa Kutegemea Mshahara ulipwe na Tanganyika mda wa kujipendekeza umetosha sasa tunaitaka Tanganyika huru.
 
Wanabodi!!!

  1. Unawachukua wabunge 80 toka Visiwani (kwa miaka50!) wanakaa Dodoma wanajadili Barabara za Geita na Katavi. Unawalipa msharahakila mwezi na posho kwa kodi toka Tanganyika!
  2. Unammchukua Makamu wa Raisi, Mawaziri, Mabalozi na 20% ya wafanyakzi wa Wizara za Muungano toka visiwani.. kisha unawalipa mishahara na posho (kwa miaka 50!) kwa kodi za Watanganyika!
  3. Tunajuinga na Afrika Mashariki. Bara wanalipia pesa ya kodi gharama za Afrika Mashariki.. Wabunge ni 9 kama walivyo wabunge toka Rwanda (9), Kenya (9). Then!!!!! Tanyanyika inatoa Wabunge (6) Na Visiwan iwabunge (3). Then Bara kwa kodi zao unawalipia wabunge wa Visiwani katika Bungela Afrika Mashariki!!!
  4. Unawateua wabunge toka Visiwani kamati za Bunge Muungano kukagua barabara kule Ngara na Tandahimba unawalipa pesa ya kodi ya Tanganyika kwa miaka 50!
  5. Halafu unakaa unajivuna Muungano huu ni waKuigwa Bara la Afrika na Dunia yote na unajipiga2 kifua kuwa na fikra sahii za waasisi wa Taifa hili!
  6. Miaka 50! Wewe unakuwa rafiki au mshirika wangu!Siku zote tukionana mimi nakununulia tu soda au bia wewe.. wewe hata siku mojahaununui… na unaona ni poa tu! Kwa mika 50!
  7. Halafu watoto wetu wa shule kule Handeni naKondoa wanakaa Chini hawana madawati na tunalalamika na kuona ni sawa!
SAA INGINE NAONA KAMA TANGANYIKA AU TANZANIA BARA TUMEROGWA AND WE ACTUALLY DO NOT KNOW OUR PRIORITIES!
WATOTO NA WAJUKUU ZETU WATAULIZA SIKU MOJA NA HATUTAKUWA NAMAJIBU!

WATANGAYIKA TUAMKE TUACHE UNAFIKI HUU!
 
Adui no moja wa muungano bila kumungunya maneno ni ccm kama hutaki angalia wakati uliopita, uliopo na ujao utapata jawabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…