SoC04 Tunaitaka Tanzania ya watanzania shupavu, hodari na imara wenye kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka

SoC04 Tunaitaka Tanzania ya watanzania shupavu, hodari na imara wenye kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ototo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2016
Posts
1,237
Reaction score
1,140
UTANGULIZI
Dunia iliumbwa kwa misingi ambayo ni sawia kabisa. Nikiwa na maana ya kwamba kila pande ya dunia kuna namna ilipewa rasimali ambazo zitawasaidia wakazi wa eneo hilo, kuweza kuendesha maisha na kuyafanya yawe rahisi.

Wenzetu wa bara la ulaya wana ufinyu wa rasilimali na hali ya hewa isiyo rafiki sana. Lakini walijaaliwa uwezo na akili ya kuyatafuta maarifa, yaliyowasaidia kuyashinda magumu yao na kujiletea maendeleo mpaka leo hii wamekua na kupigiwa mfano.

Waarabu walipewa mafuta, na wameyatumia vyema sana katika kujiletea maendeleo pamoja na hali ya ujangwa waliyonayo. Hasa umoja falme za kiarabu(Dubai)

Tanzania tuna karibia kila rasilimali inayohitaji duniani kote, tukianzia kwenye madini, bahati iliyoje tuna madini adhimu ya tanzanite yapatikayo nchini kwetu pekee. Mbuga za wanyama,mlima kilimanjaro, bahari, maziwa, mito na ardhi kubwa yenye rutuba karibu eneo lote la nchi.

Pamoja na upendeleo wote huo wa rasilimali tuliopendelewa na Mungu, Tanzania bado ni miongoni mwa nchi maskini, Tunao tapatapa katika kila sekta kuanzia miundombinu, umeme, Afya na teknolojia

KWANINI TANZANIA NI MASKINI?
Hili ni swali ambalo kila mwenye akili lazima limuumize kichwa, ikiwa nchi ina kila kitu cha kuifanya iwe na maendeleo makubwa katika sekta zote. "Umaskini wa Tanzania na watanzania ni kwa sababu ya watanzania wenyewe"

Ndio..! hilo ndilo linaweza kuwa jawabu la moja kwa moja. Maana "maendeleo siku zote huletwa na watu kwa ajili ya watu husika." Hakuna mtu anayeweza kuja kukujengea nyumba kwako ili ukae na mkeo na watoto wako

Sifa kubwa tuliyonayo watanzania ni kutokuwa na haraka, uvivu,uoga na ugoi goi. Ukitaka kugundua hilo tazama watu wakiwa wanatembea barabarani, wengi wanatembea kama kuku wenye mdondo! Watu hawana ule ukakamavu, Hawana haraka yaani. Mwendo pekee unaweza kumtambulisha mtu ni wa aina gani, kupitia mwendo unaweza kujua huyu mtu kiwango chake cha kujiamini ni kiasi gani!

Ukienda popote kupata huduma hasa kwenye ofisi za uma, watumishi wanahudumia taaratibu mwendo wa Kobe. Unakuta ni asubuhi ila mtu anakuhudumia kama amekesha masaa 24 bila kufumba macho.

Kwenye migahawa ndo usiseme unaweza agiza chakula ukaletewa baada ya masaa mawili, huyo anayekuletea sasa anavyotembea unaweza jikuta njaa yenyewe tu imeyeyuka..!

NINI KIFANYIKE?
Wanasema kugundua tatizo ni mwanzo wa utatuzi.

Serikali iwekeze kuwajenga raia katika misingi ya uchapakazi, kujiamini, kwenda na muda na uharaka katika kutekeleza majukumu kwa ufanisi. Dunia inaenda kwa kasi sana hatuweza kuenenda na Dunia kwa mwendo ambao kwa sasa watanzania tunaenda nao. (we need to be very fast and sharp) kwa kufanya yafuatayo:-

1)kuwekeza na kuhamasisha watu wawe na utamaduni wa kufanya mazoezi na kujihusisha na michezo mbali mbali.

Hii miili yetu haikuumbwa kukaa tu bila kuishughulisha angalau itoe Jasho, tunahitaji kufanya kila liwezekakalo angalau kila siku jasho litoke.

Dunia ya kileo shughuli zake nyingi hasa mjini hazihitaji matumizi ya nguvu, hali inayopelekea miili kulundika sumu na kuleta matatizo mbali mbali ya kiafya.

Watanzania wengi wanakumbwa na matatizo ya uzito uliopitiliza, mtu mwenye uzito uliopitliza" kibonge nyanya" hawezi kuwa na ufanisi katika shughuli zake, hawezi kuwa chapuchapu kwa mambo atendayo, lazima atakua wa pole pole kuanzia maamuzi mpaka vitendo vyake

A) Faida za kufanya mazoezi mara kwa mara.

Ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara una faida nyingi kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa kwa ujumla kama ifuatavyo:-

i) Kuwa na afya njema. Afya njema ndio utajiri wa kwanza ambayo mwanadamu anahitaji kuupata kabla ya vyote, Taifa likiwa na watu wenye afya njema, uzalishaji utaongezeka zaidi na kupunguza utegemezi, hivyo pato la taifa na la mtu mmoja mmoja kukua kwa kasi.

ii) Akili yenye utulivu. Mtu mwenye utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara akili yake inakua yenye utulivu zaidi kulinganisha na kipindi ambacho hakua na utaratibu wa kufanya mazoezi. Hii itaongeza ufanisi kwenye shughuli zake za kila siku, na katika ufanyaji wa maamuzi yenye tija.

iii) Kupunguza gharama katika katika sekta ya afya. Tukiwa na utaratibu kama taifa wa kufanya mazoezi mara kwa mara, safari za hospitalini zitapungua sana hivyo kupelekea serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zinaelekezwa kwenye kununua madawa na ujenzi wa vituo vya afya. Badala yeke zitaenda kufanya shughuli nyingine za maendeleo. Kwenye hili "case study" ni mimi mwenyewe, toka nianze kufanya mazoezi huu ni mwaka wa saba sasa sijameza kidonge wala kuchoma sindano.

iv) Kuitangaza nchi kimataifa na kuvutia watalii, tukiwa na utaratibu wa kufanya mazoezi na michezo mbali mbali mara kwa mara tutazalisha wanamichezo, watakaoitangaza nchi kimataifa. Kuna nchi nyingi zimepiga hatua kutokana na uhodari wa michezo, hivyo Tanzania tunaweza kuiga mfano huo na kuona inawezekana.

v) Kupunguza vifo vitokanavyo na msongo wa mawazo. Ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara huleta furaha na matumaini kwa muhusika, maana mazoezi huwa ni tiba nzuri kwa wenye misongo ya mawazo.

vi) Ufanyaji wa mazoezi huongeza na kujenga uvumilivu na nidhamu(discipline). Ukimuona mtu ana mwili uliojengeka kimazoezi hiyo ni ishara kuwa mtu huo ana uvumilivu na nidhamu ya hali ya juu, maana safari hiyo haikua rahisi. kumbuka pia Uvumilivu na nidhamu ndio misingi mikuu ya maendeleo ya aina yeyote yale, imekua ni kawaida kwa nchi yetu kusikia kashfa zikinazowahusu viongozi wetu, wakituhumiwa kuchota pesa za uma kwa manufaa yao. Yote hiyo ni sababu ya kukosa nidhamu na uvumilivu, watakuaje na nidhamu na uvumilivu ilihali hawana kabisa utaratibu wa kufanya mazoezi?

Hizo ni faida chache kati ya nyingi zitokanazo na ufanyaji wa mazoezi.

B) Namna serikali inavyoweza kuwekeza na kuhamasisha ufanyaji mazoezi. Kiuhalisia ni kwamba idadi kubwa ya watanzania hawana kabisa utaratibu wa kufanya mazoezi, hizi ni hatua serikali ikizichukua itapelekea idadi kubwa kama sio yote ya watanzania wapende kufanya mazoezi

i) Kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wanaowekeza kwenye sekta ya michezo na mazoezi. Serikali iangalie namna inavyoweza kuwaunga mkono wawekezaji katika sekta hii kwa kuwapunguzia au kuwaondolea kodi katika uagizaji au utengenezaji wa vifaa vya mazoezi, wamiliki wa gyms,vilabu vya mipira n.k..! Hii itepelekea wawekezaji kuvutiwa kuwekeza katika sekta hii kwa wingi zaidi.

ii) Sekali itenge maeneo ya wazi kila kitongoji kwa ajili ya watu wa kitongoji husika waweze kufanyia mazoezi hapo. Maana si kila mtu anaweza gharama za gym, na mazoezi yanahitaji hamasa tukisema kila mtu afanyie nyumbani inakua ngumu. Na vitawekwa vifaa vichache vitakavyowezesha ufanyaji wa mazoezi kuwa rahisi
images.jpeg

Source:www.damienboschi.com

Vifaa kama vinavyoonekana kwenye picha hapo vinafaa kuwepo kwenye viwanja vya wazi na maeneo ya beach katika nchi yetu, hiyo itahamasisha watu wengi zaidi kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi.

iii) Yaandaliwe mashindano ya kufanya mazoezi mbali mbali kitaifa na washindi wapewe zawadi nono. Na mashindano haya angalau yawe yanafanyika mara 2 kwa mwaka, na yawe yanapewa uzito na viongozi kwa kutangazwa na vyombo vya habari na kupewa promo ya kutosha.

Hilo likifanikiwa tutakuwa na watanzania wakakamavu na wanaojiamini katika utekelezaji wa majukumu ya kuijenga nchi.

2) Kuwekeza katika elimu ya vitendo zaidi kuliko ya kukariri.

Elimu yetu imekua ikiwandaa wasomi wetu kuwa watu wa kukariri zaidi kuliko vitendo, tuna elimu ya kwenye makaratasi isiyoleta matokeo yanayoonekana.

Si ajabu kumkuta kijana wa kitanzania ana bachela ya "IT" ila hana uwezo wa kutengeza website au app ya kawaida kabisa. Hii inaonyesha ni jinsi gani serikali inahitaji kutia nguvu zaidi kwenye suala la elimu kiujumla

A) Namna serikali invyoweza kuwekeza na kuhamasisha elimu ya vitendo.
i) serikali inatakiwa ibadili mtaala wa elimu, hasa ya ngazi ya msingi maana ina mkanganyiko sana. Haiwezekani mtoto asome masomo kwa lugha ya kiswahili akienda sekondari aanze tena upya kusoma kwa lugha ya kiingereza, wakati huo kuna wale wa "English medium" wao wanasoma kwa kiingereza toka msingi. Hili linekaa kibaguzi zaidi kwa watoto wanaotoka familia za hali ya chini, maana wakikutana huko juu wote wanawekwa kapu moja.

Mtaala ubadilishwe uwe kwa lugha ya kiingereza toka msingi mpaka chuo, hii itawapa wigo mpana watoto wa kitanzania kupata maarifa zaidi, tofauti na yale wanayojifunza shule.
Maana maarifa mengi yapo kwa lugha kwa kiingereza

ii) Serikali igawanye miaka ya masomo chuoni. Badala kutumia miaka yote ya masomo kuwa vyuoni wakirudia kusoma maandishi waliyokwisha soma toka sekondari.

Unaweza kutumika utaratibu ufatao, Kwa wale wanaotumia miaka 3, mwaka 1 watasoma "theories" miaka 2 iliyobaki inakua miaka ya vitendo tu, kuwa site, wafanye vitu vionekane

iii) Kuwepo na utaratibu wa kuita wataalamu mbali mbali, katika nyanja tofauti hasa teknolojia wawe wanaenda kutoa maarifa vyuoni kwa vijana wa fani husika.! Niliwahi angalia interview moja kwa millard ayo, kuna kijana wa kitanzania alikua anahojiwa anaitwa Benjamin Fernandes, yupo kwenye sekta ya "fintech"na kulingana na maelezo yake chuo cha Avard cha marekani huwa kinamuita akatoe elimu kwa vijana wa "IT" chuoni hapo na chuo kinamlipa. Cha ajabu alishajaribu kujitolea huku kwetu ili awape elimu vijana wetu, ila akakataliwa sababu tu sio profesa. Kumbe hata nchini tu hapa kuna watu wana maarifa ila wanakosa fursa ya kuwagawia wengine.

iv) Serikali iandae mkakati kila mwaka angalau iwe inachukua cream ya vijana 10 smart, wawe wanapelekwa nchi zenye teknolojia ya juu kwa ajili ya kwenda kuchota maarifa na kuja kufanya mapinduzi ya teknolojia hapa nchini. Maana katika sekta ya teknolojia kama nchi tuko nyuma sana. China walitumia mbinu hii miaka ya 70 kupeleka vijana ulaya leo hii, Taifa la China ni miongoni mwa nchi vinara wa teknolojia duniani

v) Kuwe na utaratibu wa kufanya maonyesho ya vipaji katika sekta ya teknolojia kwa vijana, kama yalivyo maonyesho ya saba Saba na nanenane..! Hii nchi kuna vijana wengi tu wana vitu vingi vya kuonyesha ila wamekosa majukwaa ya kuonyesha uwezo walionao, utaratibu huu utahamasisha vijana kujituma zaidi katika sekta ya teknolojia maana wanajua sapoti itakuwepo kama wakionyesha vitu vinavyoshawishi. Na wale watakaoibuka kidedea wawezeshwe katika kufanikisha miradi yao hiyo kwa ukubwa zaidi.

vi) Serikali ijikite zaidi katika kutoa elimu ya haki za raia..! Kila raia ajue haki zake za msingi na mipaka yake kama raia, hii itapelekea taifa kuwa na amani halisi isio na shaka wala hila. Maana kila mtu atakua anapata haki zake bila kudhulumika

HITIMISHO
ili tuweze kupiga hatua kubwa kimaendeleo kama taifa lazima tukubali na tuwe tayari kuwekeza katika watu. (Self improvement) watu ndio msingi na chanzo cha maendeleo katika taifa.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    38.3 KB · Views: 2
  • images.jpeg
    images.jpeg
    38.3 KB · Views: 2
Upvote 1
"Umaskini wa Tanzania na watanzania ni kwa sababu ya watanzania wenyewe"

Ndio..! hilo ndilo linaweza kuwa jawabu la moja kwa moja. Maana "maendeleo siku zote huletwa na watu kwa ajili ya watu husika." Hakuna mtu anayeweza kuja kukujengea nyumba kwako ili ukae na mkeo na watoto wako
Tunakubaliana kubeba wajibu na jukumu kwa maendeleo yetu, binafsi na taifa.

Watanzania wengi wanakumbwa na matatizo ya uzito uliopitiliza, mtu mwenye uzito uliopitliza" kibonge nyanya" hawezi kuwa na ufanisi katika shughuli zake, hawezi kuwa chapuchapu kwa mambo atendayo, lazima atakua wa pole pole kuanzia maamuzi mpaka vitendo vyake
Hahahaaah! so unakubaliana na wanaosema mwili huakisi utendaji wa akili, tabia tunazoziishi mwisho wa siku tunafanana nazo tunajiumba mdogo mdoogo??

Ufanyaji wa mazoezi huongeza na kujenga uvumilivu na nidhamu(discipline). Ukimuona mtu ana mwili uliojengeka kimazoezi hiyo ni ishara kuwa mtu huo ana uvumilivu na nidhamu ya hali ya juu, maana safari hiyo haikua rahisi. kumbuka pia Uvumilivu na nidhamu ndio misingi mikuu ya maendeleo ya aina yeyote yale, imekua ni kawaida kwa nchi yetu kusikia kashfa zikinazowahusu viongozi wetu, wakituhumiwa kuchota pesa za uma kwa manufaa yao. Yote hiyo ni sababu ya kukosa nidhamu na uvumilivu, watakuaje na nidhamu na uvumilivu ilihali hawana kabisa utaratibu wa kufanya mazoezi?
Nimelipata jibu langu, na tunakubaliana. Hata wajerumani walisema, how you do one thing is how you do everything. Yaani vile mtu anatenda kitu kimoja ndivyohivyohivyo anafanya mambo mengine yote.

Sekali itenge maeneo ya wazi kila kitongoji kwa ajili ya watu wa kitongoji husika waweze kufanyia mazoezi hapo. Maana si kila mtu anaweza gharama za gym, na mazoezi yanahitaji hamasa tukisema kila mtu afanyie nyumbani inakua ngumu. Na vitawekwa vifaa vichache vitakavyowezesha ufanyaji wa mazo
Nzuri, calisthenics za kitaa saafi.

Serikali igawanye miaka ya masomo chuoni. Badala kutumia miaka yote ya masomo kuwa vyuoni wakirudia kusoma maandishi waliyokwisha soma toka sekondari.
Elimu isirudiwerudiwe ndiyo kukaririshana. Na hata elimu ya msingi. Kama nilishasoma shule ya msingi rangi za msingi na rangi za upili wasirudie tena kunifundisha primary and secondary color..... twende kwenye undani zaidi kama rangi nyeupe inatengenezwaje basi...... vyuo ndio kabisaa visirudierudie viendeleze.

Kuwe na utaratibu wa kufanya maonyesho ya vipaji katika sekta ya teknolojia kwa vijana, kama yalivyo maonyesho ya saba Saba na nanenane..! Hii nchi kuna vijana wengi tu wana vitu vingi vya kuonyesha ila wamekosa majukwaa ya kuonyesha uwezo walionao
Nanenane effect, watu wajitangaze na wajibu maswali kwa watu wanaovutiwa na ubunifu wao. Kama maonesho tu. Na hili linaweza kufanywa kidijitali mfano:

Mifumo ipo, labda tu tabia zetu zisipofanyiwa kazi itabakia kuwa kikwazo, mfano uzalendo na uaminifu
 
Back
Top Bottom