tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Ati Mkoa wa Mbeya umetumia Trilioni 13 kutekeleza miradi mbali ya maji, elimu na afya kwa mwaka 2021/2022. Hii ikiwa ni zaidi ya robo ya bajeti Taifa iliyotengwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambayo ilikuwa ni kiasi cha trilioni 41. Ikiwa kila mkoa umetumia trilioni kiasi kama hicho basi Taifa zima litakuwa limetumia zaidi ya trilioni 400 kwa mwaka huo huku makusanyo yetu kila mwezi yakivunja record ni kama trilioni 2.
Wanasiasa huu uwongo mnaotengeneza utaligharimu taifa.
Trilioni 13 zatekeleza miradi ya afya, elimu Mbeya
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge Viti Maalum mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake ( UWT) kutoka Wilaya sana za Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias.
By Hawa Mathias
Mkoa wa Mbeya umetumia zaidi ya Sh13 trilioni katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwepo elimu na afya ambapo kati ya hizo Sh12 trilioni zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kipindi cha mwaka 2021/22.
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema hayo leo Jumatatu Desemba 26, 2022 wakati akizungumza na wajumbe wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Wilaya saba za Mkoa wa Mbeya.
Mhandisi Mahundi amesema kati ya fedha hizo Sh1 trilioni zimetumika katika ujenzi ya miundombinu ya vituo vya afya katika Wilaya za Chunya, Kyela, Rungwe, Mbeya Jiji na Mbeya vijijini huku trilion 12 zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 464 na Shule 172 kupitia Uviko-19.
Amesema “Tunaona vivyo hivyo katika Sekta ya Maji Mkoa (Mbeya) umepokea zaidi ya Sh250 bilioni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji kutoka mto Kiwira Wilaya ya Rungwe ambao utakuwa mwarobaini wa tatizo la maji”amesema.
Akifungua Mkutano huo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema licha ya uwekezaji mkubwa wa Serikali katika Mkoa wa Mbeya bado kuna changamoto ya suala la usafi katika maeneo mengi ya Jiji la Mbeya kutokuwa salama.
“Niwaombe madiwani wakati Serikali inaendelea kufanya mambo makubwa tuangalie namna ya kusimamia suala la usafi ikiwepo pembezoni mwa miundombinu ya barabara ambazo zinaendelea kujengwa kwani uchafu wa mazingira imekuwa tishio''amesema.
Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mbarali, Mary Mbilo amesema kuwa kazi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita ikiwepo kwenye Sekta ya afya, elimu, maji na barabara vinawafanya kutembea kifua mbele.
Mwananchi

Muktasari:
- Mkoa wa Mbeya umetumia zaidi ya Sh13 trilioni katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwepo elimu na afya ambapo kati ya hizo Sh12 trilioni zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kipindi cha mwaka 2021/22.