Tunajenga Taifa la Wajinga Kujinufaisha Kisiasa - Ati Trilioni 13 zatekeleza miradi ya afya, elimu Mbeya

Tunajenga Taifa la Wajinga Kujinufaisha Kisiasa - Ati Trilioni 13 zatekeleza miradi ya afya, elimu Mbeya

Trilioni 12 kwa madarasa 464 ina maana kila darasa liligharimu bilioni 25. Duh! Hawa viongozi baadhi wanafanya CCM ikejeliwe
 
Hata wewe nadhani huna tofauti na huyo NW kiakili na kiufahamu juu ya takwimu na mambo ya fedha..

Ukitaka kujua kuwa sikuonei kukuambia hivyo, hebu jaribu kufikiri haya;

1. Makusanyo ya kodi ya nchi kwa mwaka 2021/2022 yalikuwa shilingi ngapi?

2. Bajeti yote ya nchi kwa mwaka 2021/2022 ilikuwa shilingi ngapi?

3. Ni kiasi gani kilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo, na kulipia deni la taifa?

✓ Ukijibu vyama maswali haya utagundua kuwa fedha ya maendeleo kwa ujumla wake kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 ktk sekta zote i.e afya, elimu, miundo mbinu ya barabara, reli nk nk ilikuwa haizidi trilioni 10...!!

✓ Sasa cha ajabu NW anasema uongo kuwa kwa mwaka mmoja tu na Mbeya tu tena kwenye sekta ya afya pekee eti trilioni 13 zimetekeleza miradi ya afya...!!

Ingekuwa kweli, nakuambia hivi Mbeya ingekuwa ni PARADISO YA TANZANIA. Lakini ukweli ni kuwa Mbeya ilivyokuwa miaka ile ndivyo ilivyo leo pamoja na hizo trilioni 13 za uongo...!!!!

Labda ndugu yangu huijui trilioni ni nini achilia mbali hizo 13...
Ccm wanatabia mbaya Sana ,wamealibu asilimia kubwa ya fikra KWa vijana
 
Hakuna mjanja wa hii Dunia bali ni Mwenye Enzi Mungu tu!
Kwani tumewaona wangapi?
Hata waliko peperushwa na Mungu hapa eleweki walahi!
Atatenda tu! Walahi[emoji24]
Vilio vyetu haviendi bure!
 
Zigo la lawama ktk tarakimu zisizo sawa watasukumiwa waandishi wa habari wa kiTanzania wasio makini.
 
Back
Top Bottom