Tunajenga Taifa la Wajinga Kujinufaisha Kisiasa - Ati Trilioni 13 zatekeleza miradi ya afya, elimu Mbeya

Ata hiyo sidhani kama imefika...mi nadhan Serikali itakua imetumia 13T kwa miradi tajwa kwa nchi nzima.
Hata wewe nadhani huna tofauti na huyo NW kiakili na kiufahamu juu ya takwimu na mambo ya fedha..

Ukitaka kujua kuwa sikuonei kukuambia hivyo, hebu jaribu kufikiri haya;

1. Makusanyo ya kodi ya nchi kwa mwaka 2021/2022 yalikuwa shilingi ngapi?

2. Bajeti yote ya nchi kwa mwaka 2021/2022 ilikuwa shilingi ngapi?

3. Ni kiasi gani kilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo, na kulipia deni la taifa?

✓ Ukijibu vyama maswali haya utagundua kuwa fedha ya maendeleo kwa ujumla wake kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 ktk sekta zote i.e afya, elimu, miundo mbinu ya barabara, reli nk nk ilikuwa haizidi trilioni 10...!!

✓ Sasa cha ajabu NW anasema uongo kuwa kwa mwaka mmoja tu na Mbeya tu tena kwenye sekta ya afya pekee eti trilioni 13 zimetekeleza miradi ya afya...!!

Ingekuwa kweli, nakuambia hivi Mbeya ingekuwa ni PARADISO YA TANZANIA. Lakini ukweli ni kuwa Mbeya ilivyokuwa miaka ile ndivyo ilivyo leo pamoja na hizo trilioni 13 za uongo...!!!!

Labda ndugu yangu huijui trilioni ni nini achilia mbali hizo 13...
 
Makosa ya kiuandishi,sahihi Ni 1.3Trilioni
Hata 1.3 trilioni ni kubwa sana kwa mkoa mmoja tu tena ktk:sekta ya afya tu na tena ktk mwaka mmoja pekee 2021/202 wa kifedha...

Hizo ni takwimu za wanasiasa tu kudanganyia watu. Hakuna uhalisia kwenye hilo...

Trilioni 1.3 ndani ya mkoa mmoja ktk sekta ya afya pekee ingekuwa na impact kubwa balaa. Lakini iko wapi hiyo...?
 
MAMBUZI BANA ...

Yani kama vile yanavyolia Bandani Meee! lingine kule Meee! Makelele yasiyo na maana mwisho wa siku yanaishia kuchinjwa kuliwa Nyama

Ndio hivyo hivyo utasikia Trilioni 13, lingine kule tunamshukuru Mama kutoa fedha za maendeleo lingine huko sijui miradi imetekelezwa ....

Yaani makelele ya kudanganyana mwisho wa siku yanaishia kuiba na kunufaisha Mambuzi makubwa kwa makelele ya uongo
 
Sio sekta ya Afya tuu Bali sekta zote za Uchumi kuanzia Afya Hadi barabara
 
Sio sekta ya Afya tuu Bali sekta zote za Uchumi kuanzia Afya Hadi barabara
Kama ina - cover project zote katika sekta zote za kijamii yaani elimu, afya, miundombinu ya barabara, nk , then it makes some senses..

Lakini ingekuwa sekta moja tu kama ilivyoripotiwa na mwandishi wa Mwananchi, isingeingia akilini kwa sababu ktk financial year moja, hakuna mkoa unaopata fedha za maendeleo trilioni kadhaa labda kipekee ukiutoa mkoa wa DSM....
 
Huyu Naibu Waziri wa Maji ni kiazi mbatata, nashangaa mnamuita Mhandisi. Yeye ameamua kuwa Chawa wa Tulia Ackson kwa vile ndiye aliyempihania kumpa ubunge wa viti maalum.
Mhandisi hawezi kuwa kiazi mbatata.
 
Hv inakuwaje Naibu Waziri anashindwa kutofautisha B na T ?? ccm kwa uongo tu , nadhani huwa wanasomea kwanza uongo ndo uteuzi unafuata ..
 
Magazeti haya haya.
Jana wamesema Kuna upungufu wa madaraka 4000 (elfu nne) !
Yaani kuwafanya waTanzania mambuluma au?!
Kulikuwa na ujenzi wankutumia pesa ya COVID 19. Badala ya kuelekea pesa Kwa afya kuhusiana na tatizo lenyewe wao wamepeleka kujengwa madarasa ambayo Sasa mengine ni hewa!!
Hii ni aibu Kwa Taifa linalojinasibu kukua!! Sifa hizi zinazoendelea walah ni balaah Kwa kizazi kijacho!

Simamieni haki na utawala Bora..
 
"Mbeya vijijini huku trilion 12 zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 464 na Shule 172 kupitia Uviko-19."

Hii haipo sawa..
 
Duh...jifunze kusoma mabandiko/maoni ya wenzako vizuri kàbla hujatoa maoni yako...Kujua kusoma na kuandika nadhani ndio basic qualifications kujiunga jukwaa hili.
 
Ni pale mtumwa anapopanda farasi wakati tajiri akienda Kwa mguu,

Ni pale WASOMI wanapozurura mitaani bila ajira wakati ajira wakigawiwa UVCCM wasio na vyeti.

Imekwisha. Amen
 
Tuwekee clip ya video tumsikilize wenyewe! Haiwezekani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…