Tunajifunza nini kutokana na kitendo cha Raila Odinga kumpokea Rais Uhuru Kenyatta mjini Kisumu katika ziara ya kiserikali?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tumeshuhudia wale wapinzani wakubwa wa kisiasa wa kisiasa nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odibga, wakiwa kwenye meza moja, mjini Kisumu wakicheka na kutaniana, katika ziara aliyofanya Rais Uhuru Kenyatta mjini huko

Tukumbuke kuwa uhasama uliokuwepo kati ya Uhuru Kenyatta na Raika Odinga ilikuwa mkubwa, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu mwaka Jana ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi katika duru ya pili, baada ya duru ya kwanza kutangazwa na mahakama nchini humo kuwa matokeo yake yalikuwa batili

Tukumbuke pia Raila Odinga aliifikia hatua ya kujiapisha kuwa Rais wa wananchi, lakini kitendo hicho alichofanya Raila, ingawa kilikuwa cha kuvunja Katiba ya nchi, hatukumuona Rais, akiyaagiza majeshi "yake" yamkamate na kumweka ndani Raila Odinga

Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa na mahasimu hao wakubwa wa kisiasa nchini Kenya, ya kuombana msamaha kutokana na yaliyotokea Siku za nyuma na kauli zilizotolewa na viongozi hao wawili kuwa wanasimamia maslahi mapana ya Taifa lao na wanaweka pembeni maslahi yao binafsi

Hali ni tofauti sana nchini kwetu ambapo siasa za chuki ndizo zinazotawala

Tukumbuke kuwa kiongozi Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini,Freeman Mbowe, yupo Segerea hivi sasa kwa karibu mwezi mzima sasa, baada ya kufutiwa dhamana, kwa "maelekezo" ya Mkuu wa nchi, pale Chuo kikuu cha Dar, alipokuwa akifungua maktaba mpya, pale alipotamka hadharani na kumwambia aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuwa awaambie viongozi wenzake wa Chadema, wa-behave, ama sivyo wataishia magerezani!

Ndicho tunachokiona hivi sasa kwa mahakama nchini, kutekeleza "amri" ya Mkuu wa nchi, kuwafanya akina Mbowe waozee gerezani!

Tunajua kuwa Rais wetu hapendi kabisa kukosolewa na huko ku-behave anakoongelea yeye Rais ni kuwataka wapinzani hao wote wajiunge katika timu ya kusifu na kuabudu, juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuwaletea maendeleo watanzania

Lakini Mheshimiwa Rais anasahau kuwa haitatokea hata Siku moja wapinzani wa nchi hii wakaungana na wanaccm na wananchi wengine, katika kutoa sifa pekee kwa Mheshimiwa Rais.

Ajue kuwa wajibu mkubwa wa viongozi wa vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali ili ijirekebishe kwa ajili ya kuwaletea maendeleo chanya kwa wananchi wake

Inabidi Rais Magufuli aige mfano wa mwenzie wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na kuona kuwa mpinzani wako siyo adui na unaweza kukaa naye meza moja na mkabadilishana mawazo kwa lengo la kuipeleka nchi mbele kimaendeleo

Ikiwa Rais Magufuli ana mawazo ya kuifanya nchi hii sote tuwe tunaimba mapambio ya kumsifu yeye tu, basi atasubiri sana na Siku hiyo kamwe haitafika, kwa kuwa ni sawasawa na kusubiri mto Rufiji, ukauke kabisa maji yake yanayotiririka!

Mungu ibariki Tanzania
 
Huyo Rais unayemsemea ( tofauti na Uhuru) kuna kitu hajakifahamu kama anakifahamu basi ni jeuri ya kuzungukwa na walinzi na majeshi.
Kitu hiko kinaitwa peace of mind.. tukiachana na figisu za Uhuru K. Jamaa hata ukimtizama usoni utajua anaandaa mazingira ya kustaafu na hiyo ndiyo "peace of mind" nayozungumzia.
Ukiwa mstaafu huku ukiwa unajua kuna mambo uliyafanya pindi una mamlaka itakutesa na hautakuwa mwenye utulivu wa akili hata kukupelekea kuteseka kisaikolojia.
Sasa huyu mpori pori anahisi akiwa nje ya system hiyo jeuri atakuwa nayo "Hapana"

Kuna mawili tu nimeyasoma kwa bushmeni

1.Uozo mwingi unaendelea hivyo kunyamazisha critics hakukwepeki

2. Roho yake si sampuli ya watanzania hivyo utaifa unanitia mashaka.
 
Huyu ndiye Aliyetabiliwa na marehemu mzee kingunge Kuwa alistahili Kuwa mnyampala wa barabara na si vinginevyo sasa yametimia.
 
binafsi nimependa sana walivyofanya uhuru na odinga, Kuwa upinzani haimaanishi ndio muwe maadui mpaka mfyatuliane risasi. Nchi yetu nasisi tukifikia huko kwenye ukomavu wa Uhuru na Odinga basi hata kufànikisha Tanzania ya viwanda itakuwa kazi rahisi
 
CCM aka gambas hawawezi kufanya hivyo, kama tiss, jwtz, police na NEC wako upande wao, they don't care wananchi au upinzani wakiteseka, wakifa au kuozea jela, cha muhimu kwao ni madaraka na kupiga deal, na ndio maana kila rahisi lazima aje mradi wake ili iwe pension akotoka madarakani.
 
Unataka tujifunze nini?
hapo kenyatta keshamgawia jamaa kipande kikubwa cha keki ya taifa lazma wawe marafiki.tatizo hapa kwetu wanakula peke yao
 
Uhuru atacheka na Odinga sawa ila hata wakifanya uchaguzi leo jioni na Odinga akashinda Uhuru hatokubali na hatoachia kijiti. Nchi nyingi za Afrika vyama tawala ni vyama vilivyomuondoa mkoloni vingine viliendesha mapambano kutokea msituni, vyenyewe huamini waliokuja baada ya wao ni mapandakizi ya wakoloni. Ni nadra kwa chama tawala kuachia madaraka kisa matokeo ya boksi la kura.
Kuombana msamaha haijamsaidia Odinga kumfutia mawazo hayo Uhuru.
 
Idadi kubwa ya wanachuo sasa hawana kazi

Wengi tunaoandika humu asilimia kubwa kwa kukejeli na matusi ni watu ambao at least tuna kipato

Ukivaa viatu vya vijana wetu mtaani akina Dada na Kaka inasikitisha sana

Siasa za kijinga za kutaka kuitwa nabii huku mamilioni ya watu wakiishi Katika umaskini uliotopoea ni kupotezeana muda

Maendeleo kwa kundi hili la vijana tangu mwaka 2015 mpaka Leo ni ndoto,

Siasa za Kenya wanaangalia Give and Take, Nipe na Nikupe, Tanzania siasa wanaangalia Njaa ya tumbo

Njaa ya tumbo Tanzania huanzia kelele mdomoni baadae tumboni na kuelekea kichwani

Njaa ikifika kichwani Tanzania, Hapo watawala hujiita manabii na wafalme wakijifanya kuwatabiria Wengine maendeleo na uzalendo
 
JPM aliyekua mpinzani wake katika uchaguzi ndugu maMvi wanaelewana. JPM hana tatizo na DJ , tatizo lenu mnalazimisha ionekane kuna bifu kati ya JPM na DJ. DJ ameikosea heshma mahakama na mahakama ni mhimili unao jitegemea na Mahakama imeamua kumkumbusha DJ kwamba asiingize siasa uchwara na dharau kwenye kesi inayo endelea.
 
MIMI SINA CHA KUJIFUNZA ILA NINACHOKIONA WOTE HAWA NI UHURU NA ODINGA NI
WALE WALE WATOTO WA BABA WA MMOJA WANAKULA SAHANI MOJA NA WANALALA CHUMBA KIMOJA.

ILA WAKITOKA NJE NYUMBA YAO WANAJIFANYA HAWAELEWANI BASI KWA WALE MAJIRANI WENYE UPEO MDOGO NA TUSIOKUWA SEHEMU YA FAMILIA TUNAJIFANYA TUNAKAA KUSHABIKIA UGOMVI

SIO SIRI ODINGA NA KENYATA WANACHEZA NA AKILI ZA WAKENYA
 
If you can't beat them, join them.

Samahani.

Hiyo ni misemo miwili ya hovyo kabisa.

Tafadhali epuka kuwafunza wanao misemo hiyo.

Kama 'yaliyopita si ndwele', basi ndio tuyasahau kabisa?

Watu walipoteza maisha katika chaguzi hizo zilizoleta matatizo. Hao waliopoteza watoto wao, wapenzi wao, leo unawaambia 'yaliyopita si ndwele', bila hata kuonyesha masikitiko kwa yote yaliyotokea?

Hawa viongozi wanatakiwa katika 'kuganga yajayo' waanze na kuwatambua hao waliopoteza maisha yao juu ya siasa walizokuwa wanazifanya hao viongozi.

Hawawezi tu kusahau na kwenda mbele kana kwamba hakuna lililotokea. Maisha ya wale watu hayakuwa 'toilet paper'.

Msemo wako huo wa pili pia ni wa hovyo kabisa. Tukikubali kila tunaponyanyaswa, eti 'to join them', hakuna siku ambayo manyanyaso yatakwisha Manyanyaso yatakwisha tu wakishaona kuna nguvu inayowapinga ambayo inaweza kuwaangamiza.

Uhuru Kenyatta aliona haitakuwa rahisi kwake kuendesha nchi wakati Raila akipinga. Raila 'haku'join them' out of weakness.
 
Hukuwa na nia ya sisi kujifunza kitu hapa
Lengo ilikuwa kuuelezea udhaifu wa mweshimiwa
.
.
Hata hivyo ngoja wajuvi waje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…