BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ishu hapa kwetu chama tawala ndio kinalazimisha kufanya upinzani uwe uadui
Karibu tena mkuu Mimi sijakuona kitambo sasa.
Haya yote wanayowafanyia upinzani m wisho wa siku ni yale yale yanayowatesa nchi jirani kama drc congo rwanda burundi na uganda kwa vikundi vya waasiKabisa Mkuu angalia walivyotaka kuchukua uhai wa Lissu, Ben Saanane mwaka wa tatu huu. Upinzani na hasa Chadema kila leo wanabambikiwa kesi zisizo na kichwa wala miguu. Mbowe na Matiko si ajabu Christmas na Mwaka mpya wakazilia lupango kutokana na chuki dhidi yao pamoja na kuwa hawana hatia yeyote huku aliyemuua Akwilina akiendelea kupeta uraiani.
Hii ndio taabu ya wanasiasa wanakufa maelfu halafu wakijinufaisha kisiasa wanawaacha solemba.Tumeshuhudia wale wapinzani wakubwa wa kisiasa wa kisiasa nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odibga, wakiwa kwenye meza moja, mjini Kisumu wakicheka na kutaniana, katika ziara aliyofanya Rais Uhuru Kenyatta mjini huko
Tukumbuke kuwa uhasama uliokuwepo kati ya Uhuru Kenyatta na Raika Odinga ilikuwa mkubwa, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu mwaka Jana ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi katika duru ya pili, baada ya duru ya kwanza kutangazwa na mahakama nchini humo kuwa matokeo yake yalikuwa batili
Tukumbuke pia Raila Odinga aliifikia hatua ya kujiapisha kuwa Rais wa wananchi, lakini kitendo hicho alichofanya Raila, ingawa kilikuwa cha kuvunja Katiba ya nchi, hatukumuona Rais, akiyaagiza majeshi "yake" yamkamate na kumweka ndani Raila Odinga
Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa na mahasimu hao wakubwa wa kisiasa nchini Kenya, ya kuombana msamaha kutokana na yaliyotokea Siku za nyuma na kauli zilizotolewa na viongozi hao wawili kuwa wanasimamia maslahi mapana ya Taifa lao na wanaweka pembeni maslahi yao binafsi
Hali ni tofauti sana nchini kwetu ambapo siasa za chuki ndizo zinazotawala
Tukumbuke kuwa kiongozi Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini,Freeman Mbowe, yupo Segerea hivi sasa kwa karibu mwezi mzima sasa, baada ya kufutiwa dhamana, kwa "maelekezo" ya Mkuu wa nchi, pale Chuo kikuu cha Dar, alipokuwa akifungua maktaba mpya, pale alipotamka hadharani na kumwambia aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuwa awaambie viongozi wenzake wa Chadema, wa-behave, ama sivyo wataishia magerezani!
Ndicho tunachokiona hivi sasa kwa mahakama nchini, kutekeleza "amri" ya Mkuu wa nchi, kuwafanya akina Mbowe waozee gerezani!
Tunajua kuwa Rais wetu hapendi kabisa kukosolewa na huko ku-behave anakoongelea yeye Rais ni kuwataka wapinzani hao wote wajiunge katika timu ya kusifu na kuabudu, juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuwaletea maendeleo watanzania
Lakini Mheshimiwa Rais anasahau kuwa haitatokea hata Siku moja wapinzani wa nchi hii wakaungana na wanaccm na wananchi wengine, katika kutoa sifa pekee kwa Mheshimiwa Rais.
Ajue kuwa wajibu mkubwa wa viongozi wa vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali ili ijirekebishe kwa ajili ya kuwaletea maendeleo chanya kwa wananchi wake
Inabidi Rais Magufuli aige mfano wa mwenzie wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na kuona kuwa mpinzani wako siyo adui na unaweza kukaa naye meza moja na mkabadilishana mawazo kwa lengo la kuipeleka nchi mbele kimaendeleo
Ikiwa Rais Magufuli ana mawazo ya kuifanya nchi hii sote tuwe tunaimba mapambio ya kumsifu yeye tu, basi atasubiri sana na Siku hiyo kamwe haitafika, kwa kuwa ni sawasawa na kusubiri mto Rufiji, ukauke kabisa maji yake yanayotiririka!
Mungu ibariki Tanzania
Kwa Jiwe sidhani.....Hii ndio taabu ya wanasiasa wanakufa maelfu halafu wakijinufaisha kisiasa wanawaacha solemba.
Very soon Jiwe atakaa na akina Mbowe just a matter of time.
Mkuu tumeku-miss sana kwenye jukwaa la siasa za Home.......Upinzani si uadui, mnaweza kuwa wapinzani lakini bado mnaweka mbele maslahi ya Nchi, kukaa meza moja, kujadiliana kistaarabu kutojenga chuki na uhasama wa hali ya juu hadi kufikia kutaka kutoana roho.
Mkuu tumeku-miss sana kwenye jukwaa la siasa za Home.......
Hata hivyo ninakukaribisha katika kumkosoa huyu Jiwe ambaye yeye anaamini, kwa kuzungukwa na vifaru vya kijeshi na magari ya washawasha, ndiyo AMEKUWA HAWEZEKANIKI!
Anasahau kuwa walikuwepo madikteta, akina Iddi Amin, Bokassa, just to mention a few......
Ajiulize wako wapi madikteta hao??
Wote wameenda kuudongo, ambako ndiyo mwisho wetu sote......
Whether wewe unalindwa na vifaru vya kijeshi, lakini mwisho wako ni huo wa kuchimbiwa chini ya ardhi, katika shimo lisilozidi futi 6x6!
Huwa naangalia likes ulizopata, ndio nacomment.Sisi tunaweka ndani kiongozi mkuu wa upinzani.