Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baada ya hiko chama kufa watu waliobeba ideology ya kutokea hiko chama ndiyo wameunda Jubilee. Old wine in a new bottle.Chama kilicho lrta uhuru kulikuwa siku nyingi Uhuru anawakilisha jubilee, muungano wa vyama
Ishu hapa kwetu chama tawala ndio kinalazimisha kufanya upinzani uwe uaduiUpinzani si uadui, mnaweza kuwa wapinzani lakini bado mnaweka mbele maslahi ya Nchi, kukaa meza moja, kujadiliana kustaarabu kutojenga chuki na uhasama wa hali ya juu hadi kufikia kutaka kutoana roho.
Pole sana mkuu kumbe na nyie mmebomolewa!!Simpendi kabisa Magufuli. Na kila siku namuombea mabaya. Kwani bomoaboa za nyumba nami imenigusa
Mzee BAK mwanzo nilikuwa nakupinga sana mpaka inafikia tulikuwa tunatoleana mapovu ila kwa sasa nisamehe.Nimegundua nilipotea njia nilimuamini sana nikahisi kaja kuikomboa Tz kumbe kaja kutumaliza.Sorry my fellow jf member.Upinzani si uadui, mnaweza kuwa wapinzani lakini bado mnaweka mbele maslahi ya Nchi, kukaa meza moja, kujadiliana kustaarabu kutojenga chuki na uhasama wa hali ya juu hadi kufikia kutaka kutoana roho.
msela wa manzese bora hao wanajua kucheza na akili za wananchi wao huku mambo yao yanaenda kuliko sisi hawajui kuchezea hizo akili zetu..kama upinzani na wao wakiwekewa mazngira mazuri yasiyokandamizi hata sisi vitu kama hivyo vitakuwa kawaida kuviona huku kwetuMIMI SINA CHA KUJIFUNZA ILA NINACHOKIONA WOTE HAWA NI UHURU NA ODINGA NI
WALE WALE WATOTO WA BABA WA MMOJA WANAKULA SAHANI MOJA NA WANALALA CHUMBA KIMOJA.
ILA WAKITOKA NJE NYUMBA YAO WANAJIFANYA HAWAELEWANI BASI KWA WALE MAJIRANI WENYE UPEO MDOGO NA TUSIOKUWA SEHEMU YA FAMILIA TUNAJIFANYA TUNAKAA KUSHABIKIA UGOMVI
SIO SIRI ODINGA NA KENYATA WANACHEZA NA AKILI ZA WAKENYA
Enzi hizo nasoma nilikuwa naomba tupate rais ambaye atakuwa na misimamo mikali atoke chama tawala ama upinzani ili nchi iendelee! maana ilifikia pahala rais anatekenywa na watu anacheka cheka tu!Tumeshuhudia wale wapinzani wakubwa wa kisiasa wa kisiasa nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odibga, wakiwa kwenye meza moja, mjini Kisumu wakicheka na kutaniana, katika ziara aliyofanya Rais Uhuru Kenyatta mjini huko
Tukumbuke kuwa uhasama uliokuwepo kati ya Uhuru Kenyatta na Raika Odinga ilikuwa mkubwa, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu mwaka Jana ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi katika duru ya pili, baada ya duru ya kwanza kutangazwa na mahakama nchini humo kuwa matokeo yake yalikuwa batili
Tukumbuke pia Raila Odinga akifikia hatua ya kujiapisha kuwa Rais wa wananchi, lakini kitendo hicho alichofanya Raila, ingawa kilikuwa cha kuvunja Katiba ya nchi, hatukumuona Rais, akiyaagiza majeshi "yake" yamkamate na kumweka ndani Raila Odinga
Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa na wahasimu hao wakubwa wa kisiasa nchini Kenya, ya kuombana msamaha kutokana na yaliyotokea Siku za nyuma na kauli zilizotolewa na viongozi hao wawili kuwa wanasimamia maslahi mapana ya Taifa lao na wanaweka pembeni maslahi yao binafsi
Hali ni tofauti sana nchini kwetu ambapo siasa za chuki ndizo zinazotawala
Tukumbuke kuwa kiongozi Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini,Freeman Mbowe, yupo Segerea hivi sasa kwa karibu mwezi mzima sasa, baada ya kufutiwa dhamana, kwa "maelekezo" ya Mkuu wa nchi, pale Chuo kikuu cha Dar, alipokuwa akifungua maktaba mpya, pale alipotamka hadharani na kumwambia aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuwa awaambie viongozi wenzake wa Chadema, wa-behave, ama sivyo wataishia magerezani!
Ndicho tunachokiona hivi sasa kwa mahakama nchini, kutekeleza "amri" ya Mkuu wa nchi, kuwafanya akina Mbowe waozee gerezani!
Tunajua kuwa Rais wetu hapendi kabisa kukosolewa na huko ku-behave anakoongelea yeye Rais ni kuwataka wapinzani hao wote wajiunge katika timu ya kusifu na kuabudu, juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuwaletea maendeleo watanzania
Lakini Mheshimiwa Rais anasahau kuwa haitatokea hata Siku moja wapinzani wa nchi hii wakaungana na wanaccm na wananchi wengine, katika kutoa sifa pekee kwa Mheshimiwa Rais.
Ajue kuwa wajibu mkubwa wa viongozi wa vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali ili ijirekebishe kwa ajili ya kuwaletea maendeleo chanya kwa wananchi wake
Inabidi Rais Magufuli aige mfano wa mwenzie wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na kuona kuwa mpinzani wako siyo adui na unaweza kukaa naye meza moja na mkabadilishana mawazo kwa lengo la kuipeleka nchi mbele kimaendeleo
Ikiwa Rais Magufuli ana mawazo ya kuifanya nchi hii sote tuwe tunaimba mapambio ya kumsifu yeye tu, basi atasubiri sana na Siku hiyo kamwe haitafika, kwa kuwa ni sawasawa na kusubiri mto Rufiji, ukauke kabisa maji yake yanayotiririka!
Mungu ibariki Tanzania
That's very correct by 100 percentTusikubali kugombana kwa ajili ya itikadi za kisiasa kwani muda wowote wanasiasa wanaweza kupatana wao huku wakituacha sisi na mgawanyiko na uhasama miongoni mwetu raia wa kawaida.
Hebu tuanze na hapo, hivi Mbowe ana kesi ya jinai au ya kisiasa??JPM aliyekua mpinzani wake katika uchaguzi ndugu maMvi wanaelewana. JPM hana tatizo na DJ , tatizo lenu mnalazimisha ionekane kuna bifu kati ya JPM na DJ. DJ ameikosea heshma mahakama na mahakama ni mhimili unao jitegemea na Mahakama imeamua kumkumbusha DJ kwamba asiingize siasa uchwara na dharau kwenye kesi inayo endelea.
Simpendi kabisa Magufuli. Na kila siku namuombea mabaya. Kwani bomoaboa za nyumba nami imenigusa
ALAFU LIGI IFE, yani sizonje sijui huwa anwaza nini, au labda kwakuwa analala na mafaili kitandani, tumuombee kwa YesuKuna siku moja Simba na Yanga wataungana na kuwa timu moja japokuwa sio maadui . Just thinking tu.
Mzee BAK mwanzo nilikuwa nakupinga sana mpaka inafikia tulikuwa tunatoleana mapovu ila kwa sasa nisamehe.Nimegundua nilipotea njia nilimuamini sana nikahisi kaja kuikomboa Tz kumbe kaja kutumaliza.Sorry my fellow jf member.
Asante sana.Hakuna neno Mkuu nilikuwa nakusoma na nikawa nashangaa kidogo na kudhani wamekuibia password yako. Karibu kwenye upande wa kutetea maslahi ya Watanzania, haki na uhuru wa kujiamulia kile tukitakacho kwa faida ya Nchi yetu na vizazi vijavyo bila woga wala vitisho.