Tunajifunza nini kutokana na kitendo cha Raila Odinga kumpokea Rais Uhuru Kenyatta mjini Kisumu katika ziara ya kiserikali?

Tunajifunza nini kutokana na kitendo cha Raila Odinga kumpokea Rais Uhuru Kenyatta mjini Kisumu katika ziara ya kiserikali?

Tusikubali kugombana kwa ajili ya itikadi za kisiasa kwani muda wowote wanasiasa wanaweza kupatana wao huku wakituacha sisi na mgawanyiko na uhasama miongoni mwetu raia wa kawaida.
 
Chama kilicho lrta uhuru kulikuwa siku nyingi Uhuru anawakilisha jubilee, muungano wa vyama
Baada ya hiko chama kufa watu waliobeba ideology ya kutokea hiko chama ndiyo wameunda Jubilee. Old wine in a new bottle.
 
Upinzani si uadui, mnaweza kuwa wapinzani lakini bado mnaweka mbele maslahi ya Nchi, kukaa meza moja, kujadiliana kustaarabu kutojenga chuki na uhasama wa hali ya juu hadi kufikia kutaka kutoana roho.
Ishu hapa kwetu chama tawala ndio kinalazimisha kufanya upinzani uwe uadui
 
Wakenya wanamuita odinga mr hand cheque, yani akili zake hazina tofauti na mwita waitala
 
Upinzani si uadui, mnaweza kuwa wapinzani lakini bado mnaweka mbele maslahi ya Nchi, kukaa meza moja, kujadiliana kustaarabu kutojenga chuki na uhasama wa hali ya juu hadi kufikia kutaka kutoana roho.
Mzee BAK mwanzo nilikuwa nakupinga sana mpaka inafikia tulikuwa tunatoleana mapovu ila kwa sasa nisamehe.Nimegundua nilipotea njia nilimuamini sana nikahisi kaja kuikomboa Tz kumbe kaja kutumaliza.Sorry my fellow jf member.
 
MIMI SINA CHA KUJIFUNZA ILA NINACHOKIONA WOTE HAWA NI UHURU NA ODINGA NI
WALE WALE WATOTO WA BABA WA MMOJA WANAKULA SAHANI MOJA NA WANALALA CHUMBA KIMOJA.

ILA WAKITOKA NJE NYUMBA YAO WANAJIFANYA HAWAELEWANI BASI KWA WALE MAJIRANI WENYE UPEO MDOGO NA TUSIOKUWA SEHEMU YA FAMILIA TUNAJIFANYA TUNAKAA KUSHABIKIA UGOMVI

SIO SIRI ODINGA NA KENYATA WANACHEZA NA AKILI ZA WAKENYA
msela wa manzese bora hao wanajua kucheza na akili za wananchi wao huku mambo yao yanaenda kuliko sisi hawajui kuchezea hizo akili zetu..kama upinzani na wao wakiwekewa mazngira mazuri yasiyokandamizi hata sisi vitu kama hivyo vitakuwa kawaida kuviona huku kwetu
 
Kuna mtu anaijua ikulu na kuna mtu hataki kujifunza namna ya kuishi ikulu ndo mana ushamba unaongoza utendaji kazi wake wa kila cku
 
Tumeshuhudia wale wapinzani wakubwa wa kisiasa wa kisiasa nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odibga, wakiwa kwenye meza moja, mjini Kisumu wakicheka na kutaniana, katika ziara aliyofanya Rais Uhuru Kenyatta mjini huko

Tukumbuke kuwa uhasama uliokuwepo kati ya Uhuru Kenyatta na Raika Odinga ilikuwa mkubwa, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu mwaka Jana ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi katika duru ya pili, baada ya duru ya kwanza kutangazwa na mahakama nchini humo kuwa matokeo yake yalikuwa batili

Tukumbuke pia Raila Odinga akifikia hatua ya kujiapisha kuwa Rais wa wananchi, lakini kitendo hicho alichofanya Raila, ingawa kilikuwa cha kuvunja Katiba ya nchi, hatukumuona Rais, akiyaagiza majeshi "yake" yamkamate na kumweka ndani Raila Odinga

Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa na wahasimu hao wakubwa wa kisiasa nchini Kenya, ya kuombana msamaha kutokana na yaliyotokea Siku za nyuma na kauli zilizotolewa na viongozi hao wawili kuwa wanasimamia maslahi mapana ya Taifa lao na wanaweka pembeni maslahi yao binafsi

Hali ni tofauti sana nchini kwetu ambapo siasa za chuki ndizo zinazotawala

Tukumbuke kuwa kiongozi Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini,Freeman Mbowe, yupo Segerea hivi sasa kwa karibu mwezi mzima sasa, baada ya kufutiwa dhamana, kwa "maelekezo" ya Mkuu wa nchi, pale Chuo kikuu cha Dar, alipokuwa akifungua maktaba mpya, pale alipotamka hadharani na kumwambia aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuwa awaambie viongozi wenzake wa Chadema, wa-behave, ama sivyo wataishia magerezani!

Ndicho tunachokiona hivi sasa kwa mahakama nchini, kutekeleza "amri" ya Mkuu wa nchi, kuwafanya akina Mbowe waozee gerezani!

Tunajua kuwa Rais wetu hapendi kabisa kukosolewa na huko ku-behave anakoongelea yeye Rais ni kuwataka wapinzani hao wote wajiunge katika timu ya kusifu na kuabudu, juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuwaletea maendeleo watanzania

Lakini Mheshimiwa Rais anasahau kuwa haitatokea hata Siku moja wapinzani wa nchi hii wakaungana na wanaccm na wananchi wengine, katika kutoa sifa pekee kwa Mheshimiwa Rais.

Ajue kuwa wajibu mkubwa wa viongozi wa vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali ili ijirekebishe kwa ajili ya kuwaletea maendeleo chanya kwa wananchi wake

Inabidi Rais Magufuli aige mfano wa mwenzie wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na kuona kuwa mpinzani wako siyo adui na unaweza kukaa naye meza moja na mkabadilishana mawazo kwa lengo la kuipeleka nchi mbele kimaendeleo

Ikiwa Rais Magufuli ana mawazo ya kuifanya nchi hii sote tuwe tunaimba mapambio ya kumsifu yeye tu, basi atasubiri sana na Siku hiyo kamwe haitafika, kwa kuwa ni sawasawa na kusubiri mto Rufiji, ukauke kabisa maji yake yanayotiririka!

Mungu ibariki Tanzania
Enzi hizo nasoma nilikuwa naomba tupate rais ambaye atakuwa na misimamo mikali atoke chama tawala ama upinzani ili nchi iendelee! maana ilifikia pahala rais anatekenywa na watu anacheka cheka tu!

Japo mi mwenyewe naumia lkn nimefurahi kwa kumpata jiwe hataki upuuzi upuzi ivi najua mazuri yanakuja Mungu kajibu maombi yangu. Bila kuwa na mtu kamajiwe nchi huwa haiendi badala yake kuna watu wanakuwa na nguvu kuliko mwenye nchi hii ni aibu kabisa yaani baba mwenye nyumba unatishwa na mpangaji? how comes?

Jiwe piga kazi mpka watakapo nyooka na kujua nchi inaendaje!
 
Muafaka wa kisiasa, Uhuru na Raila sawa na Karume na Maalim. Viongozi waliokulia ikulu accommodating.
 
Kwanini usimshauri Mbowe awache kuwa kichwa maji uchaguzi ulishakwisha aondoe tofauti!
Na wewe Mkuu Kipara kipya, hebu jaribu kumshauri Mwenyekiti wako, why kila tunapojaribu kumvisha nguo yeye anazichojoa??
 
Tusikubali kugombana kwa ajili ya itikadi za kisiasa kwani muda wowote wanasiasa wanaweza kupatana wao huku wakituacha sisi na mgawanyiko na uhasama miongoni mwetu raia wa kawaida.
That's very correct by 100 percent

Lakini usitegemee hilo.litokee kwa Jiwe!
 
JPM aliyekua mpinzani wake katika uchaguzi ndugu maMvi wanaelewana. JPM hana tatizo na DJ , tatizo lenu mnalazimisha ionekane kuna bifu kati ya JPM na DJ. DJ ameikosea heshma mahakama na mahakama ni mhimili unao jitegemea na Mahakama imeamua kumkumbusha DJ kwamba asiingize siasa uchwara na dharau kwenye kesi inayo endelea.
Hebu tuanze na hapo, hivi Mbowe ana kesi ya jinai au ya kisiasa??

Hebu niulize swali la pili, hivi yule askari aliyefyatua "kizembe," zile risasi zilizomwua yule msichana aliyekuwa kwenye daladala, Akwilina Akwiline, ni kwanini hajapanfoshwa kizimbani kujibu mashitaka yake??

Swali la tatu, hivi yule Mkurugenzi wa Kinondoni aliyesababisha yote haya, kwa kuamua tu kwa makusudi "kuvikalia" viapo vya mawakala wa Chadema, wakati tayari alishawapa wenzao wa CCM, ni kwanini hapandishwi kizimbani kujibu mashitaka ya kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline??
 
Simpendi kabisa Magufuli. Na kila siku namuombea mabaya. Kwani bomoaboa za nyumba nami imenigusa

Unamuombea kwa Shetani ama? Maana mabaya yote hutoka kwa Mwovu ibilisi, na kama ulijenga nyumba kwenye Hifadhi ya barabara ulitaka afanyaje?
Mwisho wa siku ni Dua la kuku halimpati mwewe,
 
Kuna siku moja Simba na Yanga wataungana na kuwa timu moja japokuwa sio maadui . Just thinking tu.
ALAFU LIGI IFE, yani sizonje sijui huwa anwaza nini, au labda kwakuwa analala na mafaili kitandani, tumuombee kwa Yesu
 
1544781267454.png

1544781295306.png

1544781323690.png
 
Hakuna neno Mkuu nilikuwa nakusoma na nikawa nashangaa kidogo na kudhani wamekuibia password yako. Karibu kwenye upande wa kutetea maslahi ya Watanzania, haki na uhuru wa kujiamulia kile tukitakacho kwa faida ya Nchi yetu na vizazi vijavyo bila woga wala vitisho.

Mzee BAK mwanzo nilikuwa nakupinga sana mpaka inafikia tulikuwa tunatoleana mapovu ila kwa sasa nisamehe.Nimegundua nilipotea njia nilimuamini sana nikahisi kaja kuikomboa Tz kumbe kaja kutumaliza.Sorry my fellow jf member.
 
Hakuna neno Mkuu nilikuwa nakusoma na nikawa nashangaa kidogo na kudhani wamekuibia password yako. Karibu kwenye upande wa kutetea maslahi ya Watanzania, haki na uhuru wa kujiamulia kile tukitakacho kwa faida ya Nchi yetu na vizazi vijavyo bila woga wala vitisho.
Asante sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom