Zanzibar 2020 Tunakubaliana na maridhiano, lakini Maalimu Seif na ACT Wazalendo lazima muwajibu Watanzania haya

Zanzibar 2020 Tunakubaliana na maridhiano, lakini Maalimu Seif na ACT Wazalendo lazima muwajibu Watanzania haya

CHADEMA mnazidi kupotea, mnazidi kupoteza uhalali na kukubalika kisiasa. Watu huwa hawaishi kwa uhasama miaka yote ingawa uhasama wenu ni wa kimaslahi pia.

Wazanzibari wameona hawawezi kuishi kwa kununiana wakati wanaweza kuunganisha nguvu na kujenga nchi yenye kufanya shughuli za kimaendeleo zenye kupiga hatua haraka.

CHADEMA mnayo changamoto ya kupata uongozi mpya wenye maono mapya kabisa, huu wa sasa umeshapoteza muelekeo.
Bwana Mnyika ndio kabisa hakuna kitu pale
 
Naomba nichangie kidogo kwa hatua iliyofikiwa leo kwa Maalim Seif kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwanza niseme mimi ni muumini wa maridhiano na ninaunga mkono "dhana" ya maridhiano iliyofikiwa leo pale Zanzibar.

Lakini ninapinga maridhiano haya yasiyo weka wazi msingi wa Maridhiano. Ninasema haya kwakuwa hadi sasa ACT na CCM hawajatueleza msingi wa maridhiano haya ni nini na hawajatuambia matunda yamaridhiano ya nyuma nini na kitendo cha leo kuweko maridhiano tena ni tafsiri ya kuwa maridhiano ya nyuma hayakuzaa matunda.

Nimesikiliza hotuba ya Maalim Seif leo, ni nzuri lakini haijajibu hoja za msingi za sisi tunaohoji msingi wa maridhiano haya. Imekuwa ni hotuba ya jumla zaidi inayo tulazimisha tufute machozi bila kutueleza kuwa kesho hatutalia kwasababu ya hili na lile.

Moja ya kichaka cha hoja wanachojificha wanaotetea ACT kujiunga na CCM ni hiki kinachoitwa "Siasa za Zanzibar zina namna yake". Hivyo hata tukihoji kwamba sababu zilizofanya 2015 wagomee zimetatuliwa ndipo wameingia tena au laaa? Wao wanatuziba kwa kujificha kwenye kichaka kinachoitwa historia ya siasa za Zanzibar.

Tumehoji hapa kwamba ni makubaliano gani ambayo ACT na CCM wameyaweka mezani hadi kufikiwa maridhiano ya leo ili kesho yasijirudie haya? Bado hatujibiwi tunarudishwa kwenye kichaka kanakwamba sisi hatujui historia ya Zanzibar.

Mfano Chadema imeweka mezani msingi wa maridhiano ya kitaifa kati yake na CCM ambayo ni 1. Kutambua kuwa uchaguzi ulikuwa batili, 2. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, 3. Mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba kuendelea

Pengine kuna wanachoshindwa kusema wazi kuwa maslahi ya Maalim na Wenzake yamezingatiwa kuliko malengo ya Wazanzibar ya kupata nchi yao ambao ndio msingi ulioasisiwa na CUF ya Maalim. Nani leo mtetezi wa Wazanzibar??

Jibu liko Pemba na Unguja!

_______________

Nakukumbusha, ni mwezi wa Sikukuu, Watu watano watapata ZAWADI ya kitabu cha Ujasusi kwa 20,000 tu popote ulipo badala ya 80,000.

Lipia 20,000/= kwa

TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

Instagram Follow @yerickonyerere

View attachment 1644809
Perfect.
Kabla ya jambo lolote lile, ACT walipaswa waseme kwanza wameridhiana na CCM kwa lipi hasa, msingi wa maridhiano yao ni upi, na kipi tukitegemee kitazaliwa na maridhiano yao?

Kuhusu kuwa wanachama wa ACT walipiga kura kuamua kuingia kwenye SUK, hilo nalo siliamini kwa 100% kwa sababu mbili.
(i)Wanachama wa ACT hawakujulishwa mantiki ya kile ambacho chama chao kimepanga kukifanya.
(ii)Hatukuona mchakato wowote wa ndani ya ACT wa kupiga hizo kura.
 
Hahahahahahaha lol! Kwani ulilazimishwa kwenda Zitto?

1607454837452.png
 
Shukrani sana mkuu
 
Kumekuwa na mapenzi makubwa ya Katiba kipindi hiki. Wanaowatetea wabunge wa COVID19 wananukuu katiba, wanaomtetea Maalim Seifu nao wananukuu katiba.

Je mapenzi haya ya Katiba yataendelea kwa vifungu vyote kwa mfano uwepo wa vyama vingi, haki ya kuandamana, haki ya kupewa dhamana kwa mshtakiwa et cetera et cetera!
Katiba huwa mwamvuli kwa yale yanayowafurahisha tu. Wanapoivunja hawaikumbuki kabisa.
 
Perfect.
Kabla ya jambo lolote lile, ACT walipaswa waseme kwanza wameridhiana na CCM kwa lipi hasa, msingi wa maridhiano yao ni upi, na kipi tukitegemee kitazaliwa na maridhiano yao?

Kuhusu kuwa wanachama wa ACT walipiga kura kuamua kuingia kwenye SUK, hilo nalo siliamini kwa 100% kwa sababu mbili.
(i)Wanachama wa ACT hawakujulishwa mantiki ya kile ambacho chama chao kimepanga kukifanya.
(ii)Hatukuona mchakato wowote wa ndani ya ACT wa kupiga hizo kura.
Mngekuwa mnahoji pia kuhusu mishahara ya wafanyakazi wa ACT na pango za majengo zinalipwaje bila nyie kushirikishwa ingekuwa poa sana
 
Kaka,Yerico kabla hatujaisimanga ACT Wazalendo Hata nyie CDM mna maswali ya Kujibu Kwann madiwani wenu wameapa na watakuwa madiwani wakat uchaguz hamuutambui?..

Pili kwann ishu ya maridhiano ya wazanzbar Nyie wabara ndo mmekua mna uchungu nayo?

Tatu Maalim hakuingia serikalin 2015--2020 je Chuki,hasama ziliongezeka au Kupungua?..
Achen unafiki kama mnajiona Mpo sahihi mngemfukuza Aidan wa nkasi ma madiwan wenu woote nchi nzma waloapa
 
Kumekuwa na mapenzi makubwa ya Katiba kipindi hiki. Wanaowatetea wabunge wa COVID19 wananukuu katiba, wanaomtetea Maalim Seifu nao wananukuu katiba.

Je mapenzi haya ya Katiba yataendelea kwa vifungu vyote kwa mfano uwepo wa vyama vingi, haki ya kuandamana, haki ya kupewa dhamana kwa mshtakiwa et cetera et cetera!
Wanachgua vipengele vinavyo wa fauvor wanasiasa na ulaji kuliko vyenye maslahi kwa wananchi

Mfano sisi wananchi tunaumizwa na mfumo wa Kodi

Hakuna mwanasiasa anayelipa Kodi

Nani atusemee

Seif na act wameuuza mechi
 
Msingi wa uanzishwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ilikuwa ni nini?

CCM na ACT-Wazalendo walichofanya ni kutimiza takwa la Katiba ya Zanzibar 1984.

Kama ndani ya katiba kuna maridhiano basi walichofanya ni kutekeleza kilichoko ndani ya katiba.

Inanishangaza ulipoandika ''Mfano Chadema imeweka mezani msingi wa maridhiano ya kitaifa kati yake na CCM ambayo ni 1. Kutambua kuwa uchaguzi ulikuwa batili, 2. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, 3. Mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba kuendelea''

CHADEMA mnataka maridhiano na nani? Kwa lipi? Kwa msingi wa katiba ipi?
Katiba ya Tanzania inasema, the winner takes all. Kwa Tanzania bara uchaguzi umeisha!

CHADEMA wanatakiwa waishi na wakati na sio matamanio hewa!

Ninajua baada ya muda CHADEMA wataanza kupokea ruzuku za serikali lakini pia watapeleka wabunge wa viti maalum bungeni hata kama sio kina Mdee na kundi lake!

KILICHOFANYWA NA ACT NA MAALIM SIO MARIDHIANO
Kumekuwa na maoni mengi hasa baada ya ACT Wazalendo na MAALIM kukubali yaishe kwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, kumekuwa na na majibu hasa kutoka kwa ACT Wazalendo wakitetea walichokifanya kwamba ni kukidhi takwa la katiba ya Zanzibar juu serikali ya umoja wa kitaifa.

Watetezi kutoka ACT Wazalendo wanaita ni maridhiano,kwa mtizamo wangu haya si maridhiano bali ni kukimbilia madaraka kwa masilai ya chama chao zipo sababu nyingi.

1:Maalimu sio mara ya kwanza kufanya maridhiano na CCM zaidi mara nne yote yalizingatia masilai ya umma ndo maana hitimisho ilikuwa 2010 walipofanya mabadiliko ya katiba ili kuwepo serikali ya umoja wa kitaifa,na wakati wote kilichofanywa ni kila upande kuleta mapendekezo yake na mwishowe mnakubaliana ndio maana maalimu hakulaumiwa.

2:Tofauti ya uchaguzi wa 2015 na 2020 hakuna yote ilikuwa uporaji na wengi kuumizwa na wengine kufa kama ACT Wazalendo walipodhibitisha na imewapelekea kufungua case icc japo kwa hatua hii ya sasa watafifisha kwa kitendo cha kujiunga na waliowapora uchaguzi ili wahalalishe uchafuzi waliofanya

3:Maalim 2015 alifanya mazungumzo ya maridhiano na CCM wakashindwa kufikia muafaka sasa leo anakwenda bila maridhiano yaani ukiwauliza wanakuambia tunatimiza takwa la kikatiba ambalo lilikuwepo 2015 alioshindwa kuafikiana

Mwisho tulitaraji kuwe na mazungumzo ya maridhiano ya kuponya majera ya Zanzibar kuliko kumponya maalimu kisiasa watu wamekufa, wameteswa wamefilisiwa ilitakiwa waliokamatwa kwa sababu ya uchaguzi waachiwe waliokufa familia zao ziangaliwe pia kuwepo kwa usawa haki na wajibu wa vyama kufanya kazi za kisiasa ,lakini maalim na ACT Wazalendo wameangalia masilai ya chama chao kuliko umma

Maridhiano huwaweka maasimu wawili kwa pamoja ili kutatua maswaibu yaliyowakuta na Zanzibar ina makovu mengi yanayopaswa kuponywa
 
Tupo wengi sana kwa hili halikubaliki kabisa,lkn siku zote nimekuwa nikisema kuwa upinzani wa Zitto unatia mashaka sana hapa Tanzania.
Mmawia
Ukitaka kujua maana yake nakushauri anzisha chama chako ambacho kitakuwa cha kipinzani kwa upinzani huo unaouona kwako.
 
Mmawia
Ukitaka kujua maana yake nakushauri anzisha chama chako ambacho kitakuwa cha kipinzani kwa upinzani huo unaouona kwako.
Mimi nipo cdm chama ambacho naamini ni cha upinzani wa kweli kabisa ,kwa sasa tunaendelea kuwaondoa makapi, wale wasiyo na moyo wa subira.
 
Back
Top Bottom