Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hakika hotuba aliyotoa jana Rais wetu Magufuli imeniacha na huzuni kubwa, kwa kuwa nilichobaini kutokana na hotuba hiyo ni kama maisha yetu watanzania wote, tumeyaweka rehani na kiyakabidhi mikononi mwa mtu mmoja, ambaye ndiye Rais wa nchi.
Katika hotuba hiyo tulimsikia Rais akikanusha vikali kuwa nchi yetu haina mgonjwa yeyote wa covid 19.
Wakati akikanusha hivyo, mtu huyo huyo mmoja, alisikika akisema kuwa walioleta ugonjwa huo wa covid 19 nchini ni watanzania waliokwenda nje na kuchanjwa chanjo hiyo ya covid 19 na wakauleta ugonjwa huo nchini!
Lakini hakuweza kuwataja ni watanzania wepi hao ambao Rais wetu amedai kuwa walienda nchi za nje na kupata chanjo hiyo ya covid 19 na baadaye kuuleya ugonjwa huo hapa nchini.
Hivi inawezekanaje kwa mtu huyo huyo mmoja, katika hotuba yake akatae kuwa hatuna wagonjwa wa covid 19 na katika hotuba yake hiyo hiyo akiri kuwa tunao wagonjwa wa covid 19, lakini ugonjwa huo akidai kuwa umeletwa na mawakala wa mabeberu, ambao walikuwa wamechanjwa chanjo ya ugonjwa huo?
Hapo hapo Rais amahitimisha hotuba yake hiyo kwa kusema kuwa hataruhusu chanjo hiyo iingizwe nchini, kwa madai yake kuwa mabeberu hawana nia nzuri na chanjo hiyo, kwa vile wanatuonea wivu kwa kiwa Taifa letu ni tajiri sana!
Hivi wajibu wa kulinda uhai wetu watanzania wote, tumemwachia Rais wetu au ni jukumu letu watanzania wote kupaza sauti kuwa hiyo "mentality" anayoijenga Rais siyo sahihi na watanzania tulio wengi tunaihitaji chanjo hiyo ije haraka nchini ili ituokoe maisha yetu mamilioni ya wananchi.
Kwanza ni vyema ikafahamika kuwa WHO inasisitiza Mara kwa Mara kuwa kusiwepo upendeleo wa kugawa chanjo hiyo na inatolewa bure, ikionyesha wazi kuwa shirika hilo la Afya ulimwenguni linajali sana maisha ya sisi raia wanyonge.