Ramsy Dalai Lama
JF-Expert Member
- Apr 5, 2021
- 215
- 913
Kwa heshima na taadhima, habari zenu wanajukwaa. Please, ukipata muda tembelea hayo maeneo matatu nitakayo orodhesha hapa au pia naweza kukukumbusha humu humu kama utakua huna muda ili kujikumbusha yalio muhimu sana katika maisha yako.
1. Hospitali.
Hapa utaona jinsi mwanadamu alivyo dhaifu sana na afya zetu zilivyo katika mazingira ambayo muda wowote tunaweza kuathirika na kudhoofika. Huko utamuona Tajiri na Maskini wote wakipambania vitu viwili kwa pamoja ambavyo ni afya zao na uhai wao, na wote wakiomba Mungu wapone ili kuongezewa muda wa kuendelea kuishi. Hapo ndo utaelewa kuwa afya ndio utajiri wako wa kwanza, na vitu vingine vyote ndo vinafuata.
2. Gerezani.
Hapa utashuhudia jinsi kosa moja tu, au hasira ya sekunde chache tu, au maamuzi yasio sahihi, au kutokua katika sehemu/wakati usio sahihi inavyoweza kuharibu safari yako na mustakabali mzima wa maisha yako. Utaelewa gharama halisi ya Uhuru wako, na jinsi huo uhuru uliokua nao sasa ulivyo ni anasa kubwa zaidi unayoweza kuwa nayo maishani mwako kuliko unavyofikiria.
3. Makaburini.
Hapa ndo mwisho wa yote, hapa ndo utaona majina ya watu yaliyochongwa/andikwa kwenye mawe/vigae, bila kutajwa utajiri, urembo, kipaji, umaarufu, wala cheo cha mtu au vile vyote alivyowahi kua navyo akiwa hai. utakacho ona ni majina yake na tarehe ya kuzaliwa na tarehe ya kufariki tu — na kila kitu kilichotokea katika maisha ya huyo mtu kimesalia kwenye ukimya na giza zito sana. Utaelewa kuwa maisha ni mafupi mno. Lakini upendo, wema (sio Sepetu 😉), pamoja na alama/mema unayo ya acha (legacy) ndivyo vitu pekee vitakavyosalia katika vichwa vya watu basi.
okay nawatakia siku njema na tuwe wanyenyekevu (be humble).