Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

Malawi Ni nchi Maskini kuzidi Tanzania Kwa kila kitu. Nilitua pale Blantyre (Chileka) Airport kama airport ya Kijiji vile!
 
Tanzania ipo eneo strategic Kwa safari za Southern (SA-Joburg, Cape town), Eastern (Kenya-Nairobi, Mombasa) na Central (Burundi, Rwanda, Congo, Zambia). ATC wajipange mapema tu
Sio kila kituo ATCL aende hasa kwa kuangalia connection walizo nazo. Jiulize mtu atoke Mombasa au Kigali kuja kufanya nini Tanzania? Sidhani kama ATCL atakuwa hata na assurance ya 40% ya ujazo wa ndeg kama hana ndege za kuunganisha na ambazo hazipatikani huko Rwanda na Kenya. Hivi wewe unaweza kwenda Kenya bila sababu eti iko strategic position? ATCL atengeneze connection kutoka Dar kwenda nje ya nchi kama anavyofanya Guangzhou na Mumbai. London inaweza kuleta abiria wachache wa nje ila wengi watakuwa wa ndani. Kurudi Joburg na kuongeza Cape town kama ndege haitashikwa kutampa abiria wa India wengi kupitia Dar na pia wanigeria wengi kutoka South Africa kwenda Lagos na kurudi akianzisha hizo safari. DRC aongeze Kinshasa na Goma pia Malawi kwa safari za kuunganisha kwenda India na China. Aongeze huduma kwenye njia alizonazo yaani Lusaka, Ndola, Lubumbashi, Harare, Nairobi, Bujumbura, Entebbe, Comoro ili zilishe China na India na pia London na Lagos zikianza. Kigali sioni sababu ya kwenda huko, kwa soko lipi?
 
ATC chukueni ushauri huu WEST AFRICA (Lagos & Accra), SOUTHERN (Johannesburg)
 
Ndege zetu local tu kila siku zinachelewa, hakuna ratiba kutwa kubadili mda
Siku tumetua kisa wanajaza mafuta sasa kuna tofauti gani na daladala
Yaani pilot anaona mshale hautufikishi Dar

Kweli tunaweza kwenda nchi zingine kwa wakati au ni aibu tupu
Tujipige makofi na kusema hatuwezi kitu
 
Zanzibar tupewe mgao wetu kwenye hizo ndege. Kila mtu akapambane kivyake. Mambo ya kuja kulaumiana baadae hatutaki kwenye hizo ndege 11 sisi tupeni zetu 5 tutapambania Watalii waje Unguja
Mlichangia ngapi kwenye kuzinunua kama tu umeme mnatumia bure?
 
Wanyasa kwa ufadhili wa Ethiopian airlines Wana ndege 2 wanafanya maajabu international destinations (DAR, NBO, LSK, JNB & HRE) . Sisi ndege 11 international destinations za kuhesabu kwann bado hatukamati destinations za maana? Tumirogwa?
Hii COVID ilipaswa kukamata alipofeli South Africa Airways ( DAR-JNB-CPT-DUR)

View attachment 2019984

Tatizo ni madeni ya nchi kwa sababu ya viongozi wetu wasiopenda kwenda na utawala wa kisheria. Madeni hayo yanafanya wadeni watishie kukamata ndege zetu.

Kama soko la abiria wa TZ to SA, ni kubwa na tumeliacha kwa ndege za Kenya na Rwanda, huku Watanzania wakilazimika kufanya safari za kuzunguka mno.

Lakini, hatuwezi kuhudumia soko hilo, kwani ndege zetu zikitia pua tu SA, yule mkulima anaidaka papo hapo. So tulipe madeni na viongozi wetu wafuate utawala wa sheria.

Ova
 
Ndege zetu local tu kila siku zinachelewa, hakuna ratiba kutwa kubadili mda
Siku tumetua kisa wanajaza mafuta sasa kuna tofauti gani na daladala
Yaani pilot anaona mshale hautufikishi Dar

Kweli tunaweza kwenda nchi zingine kwa wakati au ni aibu tupu
Tujipige makofi na kusema hatuwezi kitu
Nimecheka kufa. Wewe hujui ndege inaendeshwa vipi. Ndege haindoki kama haina mafuta ya kutosha kufika aendako na akiba ya dharura kwenda uwanja wa dharura. Hakuna rubani mjinga hivyo maana ndege haina break huko angani
 
Nimecheka kufa. Wewe hujui ndege inaendeshwa vipi. Ndege haindoki kama haina mafuta ya kutosha kufika aendako na akiba ya dharura kwenda uwanja wa dharura. Hakuna rubani mjinga hivyo maana ndege haina break huko angani
Mkuu ni majanga mnaweza kubadilishiwa route ukasikia ndege inaenda Kigoma kwanza ndio Dar 😄
Kuna siku nimekaa na mzungu jirani ndege iko angani kapita rubani anaanguka anguka (anapepesuka)
Jamaa akaniuliza rubani kalewa? Nikamwambia welcome to Africa
Sasa unacheka ya mafuta, cheka na hii
Nb: hivi ndege inajua inaenda wapi? Mpaka igome kwenda kisa mafuta au tunaongelea mwewe hapa 😄
Basi tuliingizwa mujini
 
Back
Top Bottom