Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

Malawi Ni nchi Maskini kuzidi Tanzania Kwa kila kitu. Nilitua pale Blantyre (Chileka) Airport kama airport ya Kijiji vile!
 
Tanzania ipo eneo strategic Kwa safari za Southern (SA-Joburg, Cape town), Eastern (Kenya-Nairobi, Mombasa) na Central (Burundi, Rwanda, Congo, Zambia). ATC wajipange mapema tu
 
ATC chukueni ushauri huu WEST AFRICA (Lagos & Accra), SOUTHERN (Johannesburg)
 
Ndege zetu local tu kila siku zinachelewa, hakuna ratiba kutwa kubadili mda
Siku tumetua kisa wanajaza mafuta sasa kuna tofauti gani na daladala
Yaani pilot anaona mshale hautufikishi Dar

Kweli tunaweza kwenda nchi zingine kwa wakati au ni aibu tupu
Tujipige makofi na kusema hatuwezi kitu
 
Zanzibar tupewe mgao wetu kwenye hizo ndege. Kila mtu akapambane kivyake. Mambo ya kuja kulaumiana baadae hatutaki kwenye hizo ndege 11 sisi tupeni zetu 5 tutapambania Watalii waje Unguja
Mlichangia ngapi kwenye kuzinunua kama tu umeme mnatumia bure?
 
Tatizo ni madeni ya nchi kwa sababu ya viongozi wetu wasiopenda kwenda na utawala wa kisheria. Madeni hayo yanafanya wadeni watishie kukamata ndege zetu.

Kama soko la abiria wa TZ to SA, ni kubwa na tumeliacha kwa ndege za Kenya na Rwanda, huku Watanzania wakilazimika kufanya safari za kuzunguka mno.

Lakini, hatuwezi kuhudumia soko hilo, kwani ndege zetu zikitia pua tu SA, yule mkulima anaidaka papo hapo. So tulipe madeni na viongozi wetu wafuate utawala wa sheria.

Ova
 
Nimecheka kufa. Wewe hujui ndege inaendeshwa vipi. Ndege haindoki kama haina mafuta ya kutosha kufika aendako na akiba ya dharura kwenda uwanja wa dharura. Hakuna rubani mjinga hivyo maana ndege haina break huko angani
 
Nimecheka kufa. Wewe hujui ndege inaendeshwa vipi. Ndege haindoki kama haina mafuta ya kutosha kufika aendako na akiba ya dharura kwenda uwanja wa dharura. Hakuna rubani mjinga hivyo maana ndege haina break huko angani
Mkuu ni majanga mnaweza kubadilishiwa route ukasikia ndege inaenda Kigoma kwanza ndio Dar 😄
Kuna siku nimekaa na mzungu jirani ndege iko angani kapita rubani anaanguka anguka (anapepesuka)
Jamaa akaniuliza rubani kalewa? Nikamwambia welcome to Africa
Sasa unacheka ya mafuta, cheka na hii
Nb: hivi ndege inajua inaenda wapi? Mpaka igome kwenda kisa mafuta au tunaongelea mwewe hapa 😄
Basi tuliingizwa mujini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…