Tunamchukulia poa lakini ukweli ametushika pabaya, tena pabaya sana

Tunamchukulia poa lakini ukweli ametushika pabaya, tena pabaya sana

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,472
Reaction score
9,542
“A cornered animal is the most dangerous.”

Tangu Oktoba 29, 2025, Bi Kobe amekuwa akiishi katika hali ya mashaka na hofu kubwa. Chuki inayoongezeka miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yake, uwezekano wa mashitaka ya kimataifa, vikwazo na mashinikizo kutoka kila kona ya dunia—vyote vinaonekana kutomlegeza, bali kumfanya awe sugu na hatari zaidi.

Kwa sasa, Bi Kobe anaonekana kufika point of no return. Ameingia katika hali ya kuona kwamba ni ama maslahi yake yalindwe kwa gharama yoyote, au Watanganyika ndio walipe gharama. Kwa mwenendo wa mambo, ni vigumu kukataa kwamba ametushika pabaya.

Kuanzia vigogo na wapambe wa CCM hadi sisi makonki wapenda haki, sote tunajikuta tukicheza mdundo wake. Hakuna anayeonekana kuwa tayari au mwenye uwezo wa kumgusa. Amegeuka oil chafu: ukimgusa, unachafuka; ukimwacha, anaendelea kusambaa.

Kikosi chake maalumu cha makachinja “wasio na visogo”—(Dula Army) kinaonekana kuvishikilia mateka vyombo vyote vya dola. Hawacheki na kima wala kunguni; hawaogopi mkubwa wala mdogo. Kwa sasa, tunachoonekana kubaki nacho ni maneno, matumaini na ramli chonganishi.

Tunaweza kuongea, kujipa moyo na kutengeneza matumaini tunayoyataka, lakini ukweli mchungu unabaki pale pale: Bi Kobe ametushika pabaya.

Hata yule mstaafu wa Msoga, ambaye baadhi ya watu bado wanaamini ana ushawishi mkubwa juu yake, kwa sasa haonekani kuwa lolote wala chochote mbele ya Bi Kobe. Akijaribu kuleta ujuaji, hawa “wasio na visogo” wanaweza kuruka nae wakati wowote.

Historia inaonyesha kwamba hakuna utawala wa hofu unaodumu milele. Lakini katika kipindi hiki, huenda ikahitajika zaidi ya maneno kutuokoa kutoka katika mkono wa chuma wa jamii ya wasio na visogo.
 
Sahihi kabisa, ametushika masabauri na hakuna tunachoweza kumfanya, huenda kwa hali hii hata watanganyika hawapo kwenye ile meza ya kuamua nini kifanywe nini kiachwe, we are doomed!

Ikitokea wote tukafika 2030, ahakikishe anayeingia baada yake anamlimda na kulinda legacy(we all know her legacy) yake. Otherwise utakuwa wakati wa kulipiza visasi.
 
Sahihi kabisa, ametushika masabauri na hakuna tunachoweza kumfanya, huenda kwa hali hii hata watanganyika hawapo kwenye ile meza ya kuamua nini kifanywe nini kiachwe, we are doomed!

Ikitokea wote tukafika 2030, ahakikishe anayeingia baada yake anamlimda na kulinda legacy(we all know her legacy) yake. Otherwise utakuwa wakati wa kulipiza visasi.
Safari za Uganda za mwanamfale nikwasababu yakwenda kuchukua madesa..Huyu sasahivi kajipanga vyema , sio rahisi kudeal nae kama watu wanavyofikiri
 
Mika 7:3-4

[3]Mikono yao inayashika mabaya wayatende kwa bidii; mtu mkuu aomba rushwa, kadhi yu tayari kuipokea; mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.

[4]Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya walinzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao.
 
mstaafu wa Msoga, ambaye baadhi ya watu bado wanaamini ana ushawishi mkubwa juu yake, kwa sasa haonekani kuwa lolote wala chochote mbele ya Bi Kobe. Akijaribu kuleta ujuaji, hawa “wasio na visogo” wanaweza kuruka nae wakati wowote.
Huyu Kinara wa Wanamtandao yupo bega kwa bega na Bi mkubwa, lao moja. Sasa hivi Tanganyika ni shamba lao, wanavuna kwa bidii bila kusaza
 
Back
Top Bottom