Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
Nilifikiri Profesa shaba ameshafariki? naomba mnisahihishe.. Maana kama yupo hai basi naona tunaandikia mate!
Nilifikiri Profesa shaba ameshafariki? naomba mnisahihishe.. Maana kama yupo hai basi naona tunaandikia mate!
Sikonge,
..siku moja majira ya saa 10 jioni nilimshuhudia PROFakiwa amelewa chakari kiasi kwamba alishindwa hata kuruka kadimbwi kadogo ka maji. Prof alikavaa kadimbi kale chapwa-chapwa akatokea upande wa pili na kuendelea na safari yake. ilinisikitisha sana kumuona MSOMI WETU ktk hali ile.
..kuna utamaduni wa kuona ulevi ni kitu cha kawaida.
..wengine inaelekea tunautukuza ulevi na tunaona ni kitu poa tu cha kupigiwa mfano.
..kazi ya Prof.Shaba haikuwa kupasua na kuchunguza maiti peke yake. kuna wakati mwingine alikuwa akipelekewa tissues and other samples kuchunguza magonjwa yanayowakabili wagonjwa mbalimbali.
..lakini hata kama kazi yake ingekuwa ni kupasua maiti tu kama unavyoamini, sidhani kama jukumu hilo lilipaswa kubebwa na mlevi aliyekubuhu.
..umedai kwamba kuna matukio ambapo Prof.Shaba aliotokea kilabuni akiwa amelewa chakari na moja kwa moja kwenda "mo-chwari" kuchunguza maiti. nadhani huko ilikuwa ni kukiuka maadili ya kiapo cha kazi yake.
..ripoti za wataalamu wa Phathology zinatumika na madaktari wenzao ili kuweza kutoa huduma sahihi na bora zaidi kwa wagonjwa, na zaidi zinatumika hata ktk mamlaka za sheria kama ushahidi wa matukio mbalimbali ya vifo.
..binafsi naamini kwamba Shaba alikuwa na matatizo ya ulevi na alipaswa kusaidiwa. lakini wengine pale mjini wamekuwa wakiamini kwamba kumpa pombe zaidi mzee wa watu ndiyo kumsaidia.
..inawezekana pia kuna kitu kilichokuwa kikimchanganya zaidi ya kazi zake. kwasababu wako wengine wanaofanya kazi kama yake lakini siyo walevi waliokubuhu.
..sijui kama unafahamu kwamba Prof.Shaba alipigwa risasi mguuni na walinzi wa maeneo ya karibu na nyumbani kwake wakati akitokea kwenye ulevi? wakati mwingine Prof akishalewa anakuwa na lugha ya matusi na mgomvi, na hilo nimewahi kulishuhudia.
NB:
..sina uhakika kama Prof alifanya kazi nje ya nchi baada ya kurudi toka masomoni. ninachojua ni kwamba alisomea Scotland na alikuwa registered Pathologists huko, na kama angekosa uzalendo angeweza kulowea huko.
..kuna daktari mwingine bingwa wa upasuaji pale Muhimbili, he was considered one of the best, akiitwa Dr.Omari aliharibu kazi yake kutokana na ulevi.
..
kama anaweza kupasua maiti akiwa mtungi na watu wanamuamini kupasua vizuri, itakuwaje usimuamini akisema hayo maneno....
na hajasema mara moja karudia hayo maneno zaidi ya mara moja kwa siku tofauti bar moja pale karibu na muhimbili inaitwa centre...
mtu akifanya kitu akakuambia jana alikuwa amelewa ndio maana akafanya hivyo ujue huyo alidhamiria....
- Saafi sana na hii ndio ninaiita kumkoma nyani mpaka giladi!Jokakuu,
Usiandike kama vile unashindana. Mie wachangiaji wa hivyo huwa siwapendi. Kama upo kushindana basi umeshinda na nirudie maneno yako "Miafrika ndivyo tulivyo". Ila kama ni kuelewashana, basi soma ujumbe wangu nilioweka hadi video ya Yeltsin. Kama ujumbe wangu unaona nafagilia ULEVI, basi NUNUA MIWANI.
Nimeandika hadi mfano wa Mwalimu wangu ambaye alikuwa katoa jukumu la mtoto wake wa miaka 10 ndiyo awe mtunza nyumba na kusema ILIPENDEZA KUWAONA BABA NA WANAE WAKIWA CLOSE mara baada ya baba kuacha pombe. Sasa kufagilia ulevi hapa nani kasema? Yaani ukimwangalia Yeltsin alivyolewa hadi anatia huzuni, unataka kusema Warusi walikuwa PROUD na Rais wao?
Sipo hapa kusifia ULEVI wa SHABA. Ulevu ni kitu hatari sana na kweli Shaba alewe na asilewe, huwa anakaukorofi fulani. Pana wakati nasikia alianzisha varangati uchagani alipokwenda kwenye mazishi kwa kumwita jamaa mmoja kama Mbwa.
Lazima ujuwe kuwa kesi ya Shaba haijaanza leo. Shaba alikuwa mtu wa mkoa wa Mara kama Nyerere na wakati Katibu mkuu wa Rais ni Mzee Timothy Apiyo na yeye akiwa mtu wa hukohuko. Wawili hawa wasingeliruhusu ndugu yao aadhirike namna hiyo. Hata Prof. Sarungi alivyonyanyaswa pale Muhimbili, kisa tu kasoma Hungury wakati wenzie wamesoma West, alitaka kufunga manati na kurudi Hungury, Wazee wa Musoma wakamwambia abaki na akabaki. Shaba, nina uhakika walifanya njia nzote wakakwama na kilimsaidia kuwa bila kujali kalewa au laa, alikuwa anachapa mzigo wake barabara. Vinginevyo sidhani hata wazee wa kwao wangelimsaidia katika ulevi wake.
Wengi walikuwa wanaichukulia hali ya kazi anayoifanya na kujumlisha mengine ambayo nina uhahika Nyerere aliyafahamu na wakaamuwa kumuacha. Miaka nenda miaka rudi alifanya hizo kazi na hata kudeal na mwili wa Sokoine.
Hapa lazima nisema kuwa viongozi wa wakati ule walikuwa hawaoni vitu kama Black and white only kama wee unavyoona. Kiongozi Mzuri ni yule anayesema "Huruhusiwi kulewa kazini..... labda kama kuna special cases......" Prof. Shaba alikuwa kama toto tundu ambalo lazima ulivumilie kama wewe ni baba.
Kuna kisa nasikia kwamba Shaba alikuwa akiomba wamuwekee Viyoyozi kwenye ofisi zake na uongozi wa Muhimbili wakawa wanakataa. Siku moja akaitisha mkutano na uongozi ukaja na walipokuja, akatoka na kuwafungia ndani kama nusu saa. Aliporudi wakamwambia, Mkutano umeisha na ujumbe umefika, WAKAFUNGA VIYOYOZI maana hilo joto na hiyo harufu, wenyewe waliipata habari yao.
Nirudie tena, ulevi wa Shaba si kitu cha kujivunia, wala cha kuiga. Ila mawili, kama alishindikana, wangelimfukuza kazi au wamuache na ulevi wake hasa ukichukulia anaifanya kazi yake vizuri bila kujali kuna asilimia ngapi kichwani?
Yaani Drs wote wa Muhimbili hawakuliona hilo, hadi wee Jokakuu ndiyo umeliona? Wakamuachaniza mwenzao hadi anaenda kwa nguvu ya Ze Bia? Anyway, inawezekana ukawa sahihi yaani tuseme kuanzia Nyerere, Apiyo ...... familia ya Kisanga alikoolea, Drs wote wa Tanzania, Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ndani na nje ya Tanzania, walifurahia kumuona Shaba Mlevi maana ni KITENDO CHA KUIGWA, hadi akaja JOKAKUU ndiyo akaliona hilo. HONGERA SANA JOKA KUU, kweli wee una akili sana zaidi ya hao MAJUHA WOTE.
Worst conspiracy theory I've ever heard.Hivi huyo saint hakuwa na njia nyingine bora zaidi ya "kumpoteza" Sokoine zaidi ya kumuua?Pamoja na kutumia lugha ya mafumbo,what you're trying to suggest kuwa Nyerere,au watu wake wa karibu, alimuua Sokoine.Au,Nyerere alifahamu fika kuhusu mpango huo....Hakuna chakujadili. The autopsy was conducted by Prof Shaba and after many years kuna siku alilewa chakari akaanza kuropoka akasema jamaa alikuwa na bullet holes. Sokoine was killed by the Stalin/Mao/Lennin side of our soon to be saint... U know WHO.. Simple as.. The Saint has ultimate power within the country at the time and no one could have acted without his knowledge or approaval. Thats what it is.
He was a Prime Minister of the United Republic of Tanzania, URT. He was knocked by a car (involved in a car accident): Yes: Who where there?
1. Mr. Mustafa Nyang'anyi - Leader wa msfara
2. Mr. Chuma - The driver who had a passenger in his passenger sit; Mr. Edward Sokoine. Had suffered a broken leg, where he is? He never testified!!! (Huyu ndiye alikuwa mlinzi wake wala hakuwa Dereva wake)
3. Acadogo Chiledi - was sitting beside Mr. Sokoine during the accident!
4. The circumstance that Mr. Dube crashed the PM car, was not valid, another car was crashed; and even pictures are showing that the car which Mr. Sokoine was in was knocked from the back. His own Usalama wa Taifa knocked him from behind. But Mr. Dube was coming in an opposite direction, and then this car didn't show that it was knocked on the side (ubavuni).
5. A Prime Minister with such a popurality dies; at least there should be an investigation carried. A Task Force, Tume, or anything to investigate on the cirumstances of the death.
Let us be serious!!
Maybe that can be ok for a pathologist! Lakini mie kweli kama naumwa nikijua huyu daktari ni mlevi sitakuwa na imani ya kupona. Nitashangaa kama utamwona daktari kalewa ati aruhusiwe kumpasua mwanao.
Hata hivyo sio Dr. Shaba tu hulewa wakati wa kazi yake, pale muhimbili ni kawaida kabisa kuona daktari kanywa bia tatu (kwenye ki-store chao pale juu) nA kwenda kufanya upasuaji.
Ulevi ni tabia mbaya, hasa kama unakwenda kufanya kazi.
Ndio hapo, wanasema alifanya kazi kwa ufanisi kabisa na aliaminiwa akiwa amelewa,na pia wengine hufundisha vyema na kueleweka wakiwa wamelewa,lakini kusema jambo(Kama alivyosema Shaba Kuhusu risasi) akiwa amelewa haaminiki,inategemea na priorities...I am confused.
Jmushi1:
Tanzania bado ina syndrome ya First Generation of University Graduates ni wa kweli wa kila kitu. Mmojawapo ni professor Shaba. Katika field yake alikuwa ni wa kwanza. Hivyo procedures, rules, expertise, ethics na mambo mengine ya utaalamu ni yeye pekee alikuwa anajua na wengine tulitakiwa kukubali kile anachofanya kama ni kweli.
Sikonge said:Jokakuu,