Jokakuu,
Usiandike kama vile unashindana. Mie wachangiaji wa hivyo huwa siwapendi. Kama upo kushindana basi umeshinda na nirudie maneno yako "Miafrika ndivyo tulivyo". Ila kama ni kuelewashana, basi soma ujumbe wangu nilioweka hadi video ya Yeltsin. Kama ujumbe wangu unaona nafagilia ULEVI, basi NUNUA MIWANI.
Nimeandika hadi mfano wa Mwalimu wangu ambaye alikuwa katoa jukumu la mtoto wake wa miaka 10 ndiyo awe mtunza nyumba na kusema ILIPENDEZA KUWAONA BABA NA WANAE WAKIWA CLOSE mara baada ya baba kuacha pombe. Sasa kufagilia ulevi hapa nani kasema? Yaani ukimwangalia Yeltsin alivyolewa hadi anatia huzuni, unataka kusema Warusi walikuwa PROUD na Rais wao?
Sipo hapa kusifia ULEVI wa SHABA. Ulevu ni kitu hatari sana na kweli Shaba alewe na asilewe, huwa anakaukorofi fulani. Pana wakati nasikia alianzisha varangati uchagani alipokwenda kwenye mazishi kwa kumwita jamaa mmoja kama Mbwa.
Lazima ujuwe kuwa kesi ya Shaba haijaanza leo. Shaba alikuwa mtu wa mkoa wa Mara kama Nyerere na wakati Katibu mkuu wa Rais ni Mzee Timothy Apiyo na yeye akiwa mtu wa hukohuko. Wawili hawa wasingeliruhusu ndugu yao aadhirike namna hiyo. Hata Prof. Sarungi alivyonyanyaswa pale Muhimbili, kisa tu kasoma Hungury wakati wenzie wamesoma West, alitaka kufunga manati na kurudi Hungury, Wazee wa Musoma wakamwambia abaki na akabaki. Shaba, nina uhakika walifanya njia nzote wakakwama na kilimsaidia kuwa bila kujali kalewa au laa, alikuwa anachapa mzigo wake barabara. Vinginevyo sidhani hata wazee wa kwao wangelimsaidia katika ulevi wake.
Wengi walikuwa wanaichukulia hali ya kazi anayoifanya na kujumlisha mengine ambayo nina uhahika Nyerere aliyafahamu na wakaamuwa kumuacha. Miaka nenda miaka rudi alifanya hizo kazi na hata kudeal na mwili wa Sokoine.
Hapa lazima nisema kuwa viongozi wa wakati ule walikuwa hawaoni vitu kama Black and white only kama wee unavyoona. Kiongozi Mzuri ni yule anayesema "Huruhusiwi kulewa kazini..... labda kama kuna special cases......" Prof. Shaba alikuwa kama toto tundu ambalo lazima ulivumilie kama wewe ni baba.
Kuna kisa nasikia kwamba Shaba alikuwa akiomba wamuwekee Viyoyozi kwenye ofisi zake na uongozi wa Muhimbili wakawa wanakataa. Siku moja akaitisha mkutano na uongozi ukaja na walipokuja, akatoka na kuwafungia ndani kama nusu saa. Aliporudi wakamwambia, Mkutano umeisha na ujumbe umefika, WAKAFUNGA VIYOYOZI maana hilo joto na hiyo harufu, wenyewe waliipata habari yao.
Nirudie tena, ulevi wa Shaba si kitu cha kujivunia, wala cha kuiga. Ila mawili, kama alishindikana, wangelimfukuza kazi au wamuache na ulevi wake hasa ukichukulia anaifanya kazi yake vizuri bila kujali kuna asilimia ngapi kichwani?
Yaani Drs wote wa Muhimbili hawakuliona hilo, hadi wee Jokakuu ndiyo umeliona? Wakamuachaniza mwenzao hadi anaenda kwa nguvu ya Ze Bia? Anyway, inawezekana ukawa sahihi yaani tuseme kuanzia Nyerere, Apiyo ...... familia ya Kisanga alikoolea, Drs wote wa Tanzania, Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ndani na nje ya Tanzania, walifurahia kumuona Shaba Mlevi maana ni KITENDO CHA KUIGWA, hadi akaja JOKAKUU ndiyo akaliona hilo. HONGERA SANA JOKA KUU, kweli wee una akili sana zaidi ya hao MAJUHA WOTE.