Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Mwanakijiji,
Kama alivyoandika PM, aliyefariki ni mwanaye Dr. Harmesh Shaba. Tofauti na baba, yeye alikuwa hanywi pombe wala havuti sigara, ila ..........................

PM, sikujua jamaa alikuwa kafuata nyayo za baba mtu. Ila wakati anasoma Muhimbili, na jamaa yangu alikuwepo hapo miaka hiyo na ndiye aliniambia jinsi ya Dr. Shaba alivyobebwa na kuwekwa kwenye meza ya Maiti na maiti huyo alikuwa Rafiki yake wa Karibu ambaye saa kadhaa nyuma, walikuwa wanakunywa wote bia. Na pombe zake aliifanya kazi vizuri tu na alipotoa jibu, kila mtu akakubali.

Wakati nasoma Arusha (TCA), alikuwepo Mwalimu mmoja jina nimemsahau akifundisha somo liitwalo Mechanical Precision (kama sikosei). Alikuwa mlevi wa kutupwa. Mkewe akamkimbia na akabaki na watoto. Mtoto wake mkubwa wa kike, kipindi mimi nipo ndiyo kwanza kilikuwa shule ya msingi (nafikiri kwenye miaka 8-10), ndiyo kilikuwa kinatunza nyumba. Baba akipata mshahara anakipa hela na chenyewe kinaanza kugawanya hela ya shule, nguo zake na wadogo zake, chakula na mahitaji mengine. Nikiwa mwaka wa mwisho, yule mzee AKAACHA ULEVI/Pombe.

Akawa very close na watoto wake hadi ilikuwa inaleta raha. Ila hamuwezi amini wanafunzi wengi wakaanza kulalamika kuwa TANGU AACHE POMBE, UFUNDISHAJI WAKE UMEPUNGUA HADHI.
 
Sikonge,

..siku moja majira ya saa 10 jioni nilimshuhudia PROFakiwa amelewa chakari kiasi kwamba alishindwa hata kuruka kadimbwi kadogo ka maji. Prof alikavaa kadimbi kale chapwa-chapwa akatokea upande wa pili na kuendelea na safari yake. ilinisikitisha sana kumuona MSOMI WETU ktk hali ile.

..kuna utamaduni wa kuona ulevi ni kitu cha kawaida.

..wengine inaelekea tunautukuza ulevi na tunaona ni kitu poa tu cha kupigiwa mfano.

..kazi ya Prof.Shaba haikuwa kupasua na kuchunguza maiti peke yake. kuna wakati mwingine alikuwa akipelekewa tissues and other samples kuchunguza magonjwa yanayowakabili wagonjwa mbalimbali.

..lakini hata kama kazi yake ingekuwa ni kupasua maiti tu kama unavyoamini, sidhani kama jukumu hilo lilipaswa kubebwa na mlevi aliyekubuhu.

..umedai kwamba kuna matukio ambapo Prof.Shaba aliotokea kilabuni akiwa amelewa chakari na moja kwa moja kwenda "mo-chwari" kuchunguza maiti. nadhani huko ilikuwa ni kukiuka maadili ya kiapo cha kazi yake.

..ripoti za wataalamu wa Phathology zinatumika na madaktari wenzao ili kuweza kutoa huduma sahihi na bora zaidi kwa wagonjwa, na zaidi zinatumika hata ktk mamlaka za sheria kama ushahidi wa matukio mbalimbali ya vifo.

..binafsi naamini kwamba Shaba alikuwa na matatizo ya ulevi na alipaswa kusaidiwa. lakini wengine pale mjini wamekuwa wakiamini kwamba kumpa pombe zaidi mzee wa watu ndiyo kumsaidia.

..inawezekana pia kuna kitu kilichokuwa kikimchanganya zaidi ya kazi zake. kwasababu wako wengine wanaofanya kazi kama yake lakini siyo walevi waliokubuhu.

..sijui kama unafahamu kwamba Prof.Shaba alipigwa risasi mguuni na walinzi wa maeneo ya karibu na nyumbani kwake wakati akitokea kwenye ulevi? wakati mwingine Prof akishalewa anakuwa na lugha ya matusi na mgomvi, na hilo nimewahi kulishuhudia.

NB:

..sina uhakika kama Prof alifanya kazi nje ya nchi baada ya kurudi toka masomoni. ninachojua ni kwamba alisomea Scotland na alikuwa registered Pathologists huko, na kama angekosa uzalendo angeweza kulowea huko.

..kuna daktari mwingine bingwa wa upasuaji pale Muhimbili, he was considered one of the best, akiitwa Dr.Omari aliharibu kazi yake kutokana na ulevi.

..
 
Jokakuu:

Nashukuru kwa mchango wako mzuri. Kwenye posti yangu moja hapa nimezungumzia huyu mwandishi wa habari ambaye ameshutumiwa kwenye utangulizi wa thread.

Inaonekana kwetu, stress ambazo mtu anazipata baada kuwa-traumatized hazichukuliwi kama kuwa ni chanzo cha mtu kuwa na tabia zisizo za kawaida au kuwa mlevi. Siku zote mtu anatakiwa kuwa mgumu.

Kazi anayofanya Doctor Shaba ina-stress zake (period). Pamoja na stress zake, kwa tanzania anatakiwa aishi kwenye mazingira duni na alime mchicha kujiongezea kipato chake.

Ninavyosoma posti hapa, inaonyesha kabisa ulevi wa professor Shaba unachukuliwa kama resilient yake. Hivyo chochote atakachosema hata akiwa chakari ni sahihi. Na kuna wengine wanaoamini kuwa akiwa amelewa ndio anakuwa sahihi zaidi. Kama ni hivyo mbona watu hawakubali kupanda magari yanayoendeshwa na mlevi.

Vilevile tukirudi kwenye mada, kwanini watu wanamshuku acagoda chiledi kwa tabia zake za ajabu ajabu baada ya ajari kutokea? Jiweke mwenyewe kwenye nafasi ya huyu jamaa. Kuna watu wame-run mental kwa ku-fail mitihani ya vyuoni. Je haiwezekani mtu kuwa na matatizo ya kisaikolojia baada ya kuwepo kwenye ajari
 
Zakumi,

..hii thread na masuala ya ulevi yamenikumbusha ujana wangu nikiwa sekondari.

..nakumbuka mwalimu wetu mmoja. alikuwa akisifiwa kwamba ni mwalimu mzuri sana. sasa wiki moja alikuwa ndiyo mwalimu wa zamu. kitu cha ajabu kabisa akatokea straight frm kilabuni na kuja kwenye school assembly.

..asubuhi hiyo alikuwa mchafu, ananuka, hana viatu, na amelewa chakari, halafu anajaribu kutoa mwongozo na ku-discipline wanafunzi.

..sasa kuna wenzetu wengine watasema:" aah mwanawane/kudadekii ..mwalimu fulani hata alewe usiku mzima lakini kama yuko zamu baba ake hakosi kwenye school assembly!!"

..wakati mwingine tujaribu kuzifikiria familia zao-mke na watoto. wanaishi ktk stress ya namna gani kwamba BABA yuko kwenye POMBE mpaka usiku wa manane.

NB:

..kuna kipindi Prof alipelekwa nje ama kwa ajili ya rehab, au kutibiwa majeraha yake ya risasi. aliporudi nyumbani karibu kila mtu aliona kwamba Prof's healthy had really improved.
 
kama anaweza kupasua maiti akiwa mtungi na watu wanamuamini kupasua vizuri, itakuwaje usimuamini akisema hayo maneno....
na hajasema mara moja karudia hayo maneno zaidi ya mara moja kwa siku tofauti bar moja pale karibu na muhimbili inaitwa centre...

mtu akifanya kitu akakuambia jana alikuwa amelewa ndio maana akafanya hivyo ujue huyo alidhamiria....

Ndio hapo, wanasema alifanya kazi kwa ufanisi kabisa na aliaminiwa akiwa amelewa,na pia wengine hufundisha vyema na kueleweka wakiwa wamelewa,lakini kusema jambo(Kama alivyosema Shaba Kuhusu risasi) akiwa amelewa haaminiki,inategemea na priorities...I am confused.
 
Jokakuu,

Usiandike kama vile unashindana. Mie wachangiaji wa hivyo huwa siwapendi. Kama upo kushindana basi umeshinda na nirudie maneno yako "Miafrika ndivyo tulivyo". Ila kama ni kuelewashana, basi soma ujumbe wangu nilioweka hadi video ya Yeltsin. Kama ujumbe wangu unaona nafagilia ULEVI, basi NUNUA MIWANI.
Nimeandika hadi mfano wa Mwalimu wangu ambaye alikuwa katoa jukumu la mtoto wake wa miaka 10 ndiyo awe mtunza nyumba na kusema ILIPENDEZA KUWAONA BABA NA WANAE WAKIWA CLOSE mara baada ya baba kuacha pombe. Sasa kufagilia ulevi hapa nani kasema? Yaani ukimwangalia Yeltsin alivyolewa hadi anatia huzuni, unataka kusema Warusi walikuwa PROUD na Rais wao?
Sipo hapa kusifia ULEVI wa SHABA. Ulevu ni kitu hatari sana na kweli Shaba alewe na asilewe, huwa anakaukorofi fulani. Pana wakati nasikia alianzisha varangati uchagani alipokwenda kwenye mazishi kwa kumwita jamaa mmoja kama Mbwa.

Lazima ujuwe kuwa kesi ya Shaba haijaanza leo. Shaba alikuwa mtu wa mkoa wa Mara kama Nyerere na wakati Katibu mkuu wa Rais ni Mzee Timothy Apiyo na yeye akiwa mtu wa hukohuko. Wawili hawa wasingeliruhusu ndugu yao aadhirike namna hiyo. Hata Prof. Sarungi alivyonyanyaswa pale Muhimbili, kisa tu kasoma Hungury wakati wenzie wamesoma West, alitaka kufunga manati na kurudi Hungury, Wazee wa Musoma wakamwambia abaki na akabaki. Shaba, nina uhakika walifanya njia nzote wakakwama na kilimsaidia kuwa bila kujali kalewa au laa, alikuwa anachapa mzigo wake barabara. Vinginevyo sidhani hata wazee wa kwao wangelimsaidia katika ulevi wake.

Wengi walikuwa wanaichukulia hali ya kazi anayoifanya na kujumlisha mengine ambayo nina uhahika Nyerere aliyafahamu na wakaamuwa kumuacha. Miaka nenda miaka rudi alifanya hizo kazi na hata kudeal na mwili wa Sokoine.
Hapa lazima nisema kuwa viongozi wa wakati ule walikuwa hawaoni vitu kama Black and white only kama wee unavyoona. Kiongozi Mzuri ni yule anayesema "Huruhusiwi kulewa kazini..... labda kama kuna special cases......" Prof. Shaba alikuwa kama toto tundu ambalo lazima ulivumilie kama wewe ni baba.
Kuna kisa nasikia kwamba Shaba alikuwa akiomba wamuwekee Viyoyozi kwenye ofisi zake na uongozi wa Muhimbili wakawa wanakataa. Siku moja akaitisha mkutano na uongozi ukaja na walipokuja, akatoka na kuwafungia ndani kama nusu saa. Aliporudi wakamwambia, Mkutano umeisha na ujumbe umefika, WAKAFUNGA VIYOYOZI maana hilo joto na hiyo harufu, wenyewe waliipata habari yao.

Nirudie tena, ulevi wa Shaba si kitu cha kujivunia, wala cha kuiga. Ila mawili, kama alishindikana, wangelimfukuza kazi au wamuache na ulevi wake hasa ukichukulia anaifanya kazi yake vizuri bila kujali kuna asilimia ngapi kichwani?

Yaani Drs wote wa Muhimbili hawakuliona hilo, hadi wee Jokakuu ndiyo umeliona? Wakamuachaniza mwenzao hadi anaenda kwa nguvu ya Ze Bia? Anyway, inawezekana ukawa sahihi yaani tuseme kuanzia Nyerere, Apiyo ...... familia ya Kisanga alikoolea, Drs wote wa Tanzania, Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ndani na nje ya Tanzania, walifurahia kumuona Shaba Mlevi maana ni KITENDO CHA KUIGWA, hadi akaja JOKAKUU ndiyo akaliona hilo. HONGERA SANA JOKA KUU, kweli wee una akili sana zaidi ya hao MAJUHA WOTE.
 
- Saafi sana na hii ndio ninaiita kumkoma nyani mpaka giladi!

FMES!
 
Hakuna chakujadili. The autopsy was conducted by Prof Shaba and after many years kuna siku alilewa chakari akaanza kuropoka akasema jamaa alikuwa na bullet holes. Sokoine was killed by the Stalin/Mao/Lennin side of our soon to be saint... U know WHO.. Simple as.. The Saint has ultimate power within the country at the time and no one could have acted without his knowledge or approaval. Thats what it is.
Worst conspiracy theory I've ever heard.Hivi huyo saint hakuwa na njia nyingine bora zaidi ya "kumpoteza" Sokoine zaidi ya kumuua?Pamoja na kutumia lugha ya mafumbo,what you're trying to suggest kuwa Nyerere,au watu wake wa karibu, alimuua Sokoine.Au,Nyerere alifahamu fika kuhusu mpango huo....

Kwani Nyerere si ndio aliyemteua Sokoine kuwa PM?If so,si angeweza kumpiga chini kisha akatumia detention act or whatsoever power he had kumdhibiti?

Kwamba hakuna lolote kubwa lingeweza kufanyika pasipo Nyerere kujua ni suala la kufikirika zaidi kuliko practical.Jeshi lilipofanya maasi mara ya kwanza,Nyerere alikuwa ameshakufa?Kesi ya uhaini nayo?Kama si "uzembe flani" watu akian Uncle Tom wangebadili ramani ya nchi.Nobody should fool you kwamba Nyerere alikuwa anajua ABSOLUTELY kila kinachoendelea....He knew most but not all....na mfano mwepesi ni huu:alimjua Kingunge Ngombale Mwiru vizuri kuwa ni mjamaa mwenzake,lakini hakumjua 100% kwamba ana chembechembe za ufisadi,ambao tunaushuhudia hivi sasa.Nyerere alimjua Mkapa kama kijana msafi na mwaminifu.Lakini leo Mkapa ni political bandit.

Well,hiyo yako remains a conspiracy theory kama yangu kuwa wahusika ni Kawawa et al.
 
Maybe that can be ok for a pathologist! Lakini mie kweli kama naumwa nikijua huyu daktari ni mlevi sitakuwa na imani ya kupona. Nitashangaa kama utamwona daktari kalewa ati aruhusiwe kumpasua mwanao.

Hata hivyo sio Dr. Shaba tu hulewa wakati wa kazi yake, pale muhimbili ni kawaida kabisa kuona daktari kanywa bia tatu (kwenye ki-store chao pale juu) nA kwenda kufanya upasuaji.

Ulevi ni tabia mbaya, hasa kama unakwenda kufanya kazi.
 
Ukweli ni kuwa Ufisadi na Umafia wa mauaji Nchi hii ulianza siku nyingi only kwamba hawakuwa na nguvu kama ilivyo sasa hivi simply because this has become "No Mans Land"
 
He was a Prime Minister of the United Republic of Tanzania, URT. He was knocked by a car (involved in a car accident): Yes: Who where there?
1. Mr. Mustafa Nyang'anyi - Leader wa msfara
2. Mr. Chuma - The driver who had a passenger in his passenger sit; Mr. Edward Sokoine. Had suffered a broken leg, where he is? He never testified!!! (Huyu ndiye alikuwa mlinzi wake wala hakuwa Dereva wake)
3. Acadogo Chiledi - was sitting beside Mr. Sokoine during the accident!
4. The circumstance that Mr. Dube crashed the PM car, was not valid, another car was crashed; and even pictures are showing that the car which Mr. Sokoine was in was knocked from the back. His own Usalama wa Taifa knocked him from behind. But Mr. Dube was coming in an opposite direction, and then this car didn't show that it was knocked on the side (ubavuni).
5. A Prime Minister with such a popurality dies; at least there should be an investigation carried. A Task Force, Tume, or anything to investigate on the cirumstances of the death.

Let us be serious!!

Mkuu IO,

Just a small correction, Chuma alikuwa ni mlinzi wa Sokoine hakuwa Dereva. Huyu Chuma bado yuko UWT mpaka leo na nafikiri tayari ana cheo kikubwa kidogo. Dereva wake sikumbuki jina lake vizuri lakini alikuwa ni Mzee mmoja hivi (alikuwa jirani yetu) alikuwa na kajumba kabovu bovu pale Manzese uzuri lakini baada ya ile ajali alijengewa nyumba nzuri na kustaafishwa.

Huyu Mzee ungetaka mkosane, basi umwuulize ile ajali ilitokea vipi!!!! Sijui kama bado yuko hai kwa kuwa baadae nilihama mitaa ile.

Tiba
 
Kuna mtu anajua Professor Shaba anapatikana wapi kwa sasa? physical address au namba ya simu? Kuna mambo ya zamani ningependa kuzungumza naye, sio kuhusu Sokoine. Nitashukuru mkinisaidia
 
Maybe that can be ok for a pathologist! Lakini mie kweli kama naumwa nikijua huyu daktari ni mlevi sitakuwa na imani ya kupona. Nitashangaa kama utamwona daktari kalewa ati aruhusiwe kumpasua mwanao.

Hata hivyo sio Dr. Shaba tu hulewa wakati wa kazi yake, pale muhimbili ni kawaida kabisa kuona daktari kanywa bia tatu (kwenye ki-store chao pale juu) nA kwenda kufanya upasuaji.

Ulevi ni tabia mbaya, hasa kama unakwenda kufanya kazi.

...uhuru wa maoni, Binafsi i dont mind pathologists, Mortuary attendants, Caretakers na Grave diggers kuwa walevi, 'kibarua' cha siku nzima na maiti wa namna kwa namna si mchezo!
 
Ndio hapo, wanasema alifanya kazi kwa ufanisi kabisa na aliaminiwa akiwa amelewa,na pia wengine hufundisha vyema na kueleweka wakiwa wamelewa,lakini kusema jambo(Kama alivyosema Shaba Kuhusu risasi) akiwa amelewa haaminiki,inategemea na priorities...I am confused.

Jmushi1:

Tanzania bado ina syndrome ya First Generation of University Graduates ni wa kweli wa kila kitu. Mmojawapo ni professor Shaba. Katika field yake alikuwa ni wa kwanza. Hivyo procedures, rules, expertise, ethics na mambo mengine ya utaalamu ni yeye pekee alikuwa anajua na wengine tulitakiwa kukubali kile anachofanya kama ni kweli.

Na zaidi ya hapo, uamuzi wake ulikuwa ni final na hakuna second opinion. Hivyo kwa miaka mingi nchi had to live with what we had. Tulikuwa na choice mbili tu. Kutumia ujuzi wake na kukubali matokeo ya uchunguzi wake, au kutofanya uchunguzi kabisa.

Hapa inatolewa mifano mingi ya umahiri wa professor akiwa chakari. Na wanaotoa mifano yake hata glimpse ya pathology hawana.

Maprofessor wa Muhimbili wa fani mbalimbali wakikutana kupata vinywaji, wataongea mambo ya fani zako kwa sababu wataelewana japokuwa wapo chakari. Lakini mazungumzo yao yasichukuliwe kama sehemu ya academic enlightment kama mifano inavyotolewa hapa. Mazungumzo yao ni sehemu ya networking.

Anyway, sehemu kubwa ya mila na desturi zetu ni kujali aliye hai. Aliyekufa ni kazi ya Mungu au kwa maneno mengine Bwana alitoa, Bwana alitwaa case closed.
 
Kwani Prof Shaba bado anaishi pale Garden Avenue?...........ile sehemu/area si alishauziwa Rostam Aziz au?
 
Jmushi1:

Tanzania bado ina syndrome ya First Generation of University Graduates ni wa kweli wa kila kitu. Mmojawapo ni professor Shaba. Katika field yake alikuwa ni wa kwanza. Hivyo procedures, rules, expertise, ethics na mambo mengine ya utaalamu ni yeye pekee alikuwa anajua na wengine tulitakiwa kukubali kile anachofanya kama ni kweli.

Zakumi,

Nafikiri hapa kidogo umeandika kama vile tuko miaka ya 70. Miaka hiyo hadi hiyo miaka ya 80 kulikuwa kweli kuna tatizo hilo. Ila kwa Muhimbili, mambo yalikuja kubadilika sana.

Kumbuka kuwa Prof. Sarungi alisoma Hungury na kuja Tanzania kama Dr. Alipofika pale, alikutana na hiyo syndrom na si kuwa walikuwa wanaangalia una degree, ila walikuwa wanachunguza umesoma wapi (matatizo ya cold war). Waliosoma nchi za Kikomunisti walidharaulika sana na kuonekana hawajui kitu.

Hii ilikuja kuisha baada ya Sarungi kuanza kupanda na baadaye kuja ku-prove uwezo wake katika mifupa kuzidi hata hao waliosoma West. Sarungu alipanda/alipandishwa hadi akawa boss wa Muhimbili na baadaye Waziri wa Afya.

Tangu kipindi hicho, hakuna tena kupeana heshima kwa sababu tu wewe ni fulani au umesoma sehemu fulani au miaka fulani.

Mwisho, ninavyofahamu mie ni kwamba, Prof. Shaba si amejiajiri mwenyewe kwa sasa? Nakumbuka kulikuwa na ugomvi mkubwa sana alipoleta mafrigi ya kutunzia maiti na serikali ikadai kodi.

Mwisho, nafikiri kuna tofauti kidogo kwa kuangalia elimu za zamani na sasa. Zamani ilikuwa wanaukatakata mwili ili kujua nini kimesababisha kifo na siku hizi wanafanya Scanning na wakipata picha, kuna vijana wanakaa na kuzisoma na kutoa jibu.

Sasa kulinganisha hawa vijana na Prof. Shaba, mhhh. Ila heshima mbele kwa sana kwa wazee wetu maana walifanya madude mengi na ya ajabu bila ya kutumia computer. Miaka ya 90 nilikuwa na jamaa yangu mmoja akisema "kama uko Ulaya/West, ukitumia nguvu kufanya kitu chochote basi ujuwe unakosea..." Yes, unakosea ila miaka ya nyuma, ilikuwa lazima utumie NGUVU na hii kwangi ndiyo inafanya TUWAHESHIMU HAWA WAZEE.
 
bullet holles and our soon to be saint how comes ?shabba discovered only bullet hole how comes our soon saint been concerned?
 
Sikonge said:
Jokakuu,

Usiandike kama vile unashindana. Mie wachangiaji wa hivyo huwa siwapendi. Kama upo kushindana basi umeshinda na nirudie maneno yako "Miafrika ndivyo tulivyo". Ila kama ni kuelewashana, basi soma ujumbe wangu nilioweka hadi video ya Yeltsin. Kama ujumbe wangu unaona nafagilia ULEVI, basi NUNUA MIWANI.
Nimeandika hadi mfano wa Mwalimu wangu ambaye alikuwa katoa jukumu la mtoto wake wa miaka 10 ndiyo awe mtunza nyumba na kusema ILIPENDEZA KUWAONA BABA NA WANAE WAKIWA CLOSE mara baada ya baba kuacha pombe. Sasa kufagilia ulevi hapa nani kasema? Yaani ukimwangalia Yeltsin alivyolewa hadi anatia huzuni, unataka kusema Warusi walikuwa PROUD na Rais wao?
Sipo hapa kusifia ULEVI wa SHABA. Ulevu ni kitu hatari sana na kweli Shaba alewe na asilewe, huwa anakaukorofi fulani. Pana wakati nasikia alianzisha varangati uchagani alipokwenda kwenye mazishi kwa kumwita jamaa mmoja kama Mbwa.

Lazima ujuwe kuwa kesi ya Shaba haijaanza leo. Shaba alikuwa mtu wa mkoa wa Mara kama Nyerere na wakati Katibu mkuu wa Rais ni Mzee Timothy Apiyo na yeye akiwa mtu wa hukohuko. Wawili hawa wasingeliruhusu ndugu yao aadhirike namna hiyo. Hata Prof. Sarungi alivyonyanyaswa pale Muhimbili, kisa tu kasoma Hungury wakati wenzie wamesoma West, alitaka kufunga manati na kurudi Hungury, Wazee wa Musoma wakamwambia abaki na akabaki. Shaba, nina uhakika walifanya njia nzote wakakwama na kilimsaidia kuwa bila kujali kalewa au laa, alikuwa anachapa mzigo wake barabara. Vinginevyo sidhani hata wazee wa kwao wangelimsaidia katika ulevi wake.

Wengi walikuwa wanaichukulia hali ya kazi anayoifanya na kujumlisha mengine ambayo nina uhahika Nyerere aliyafahamu na wakaamuwa kumuacha. Miaka nenda miaka rudi alifanya hizo kazi na hata kudeal na mwili wa Sokoine.
Hapa lazima nisema kuwa viongozi wa wakati ule walikuwa hawaoni vitu kama Black and white only kama wee unavyoona. Kiongozi Mzuri ni yule anayesema "Huruhusiwi kulewa kazini..... labda kama kuna special cases......" Prof. Shaba alikuwa kama toto tundu ambalo lazima ulivumilie kama wewe ni baba.
Kuna kisa nasikia kwamba Shaba alikuwa akiomba wamuwekee Viyoyozi kwenye ofisi zake na uongozi wa Muhimbili wakawa wanakataa. Siku moja akaitisha mkutano na uongozi ukaja na walipokuja, akatoka na kuwafungia ndani kama nusu saa. Aliporudi wakamwambia, Mkutano umeisha na ujumbe umefika, WAKAFUNGA VIYOYOZI maana hilo joto na hiyo harufu, wenyewe waliipata habari yao.

Nirudie tena, ulevi wa Shaba si kitu cha kujivunia, wala cha kuiga. Ila mawili, kama alishindikana, wangelimfukuza kazi au wamuache na ulevi wake hasa ukichukulia anaifanya kazi yake vizuri bila kujali kuna asilimia ngapi kichwani?

Yaani Drs wote wa Muhimbili hawakuliona hilo, hadi wee Jokakuu ndiyo umeliona? Wakamuachaniza mwenzao hadi anaenda kwa nguvu ya Ze Bia? Anyway, inawezekana ukawa sahihi yaani tuseme kuanzia Nyerere, Apiyo ...... familia ya Kisanga alikoolea, Drs wote wa Tanzania, Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ndani na nje ya Tanzania, walifurahia kumuona Shaba Mlevi maana ni KITENDO CHA KUIGWA, hadi akaja JOKAKUU ndiyo akaliona hilo. HONGERA SANA JOKA KUU, kweli wee una akili sana zaidi ya hao MAJUHA WOTE.

Sikonge,

..hii posting yako imenishtua kiasi cha kunilazimisha kupitia posting zangu kujua ni kwanini tumefika hapa.

..nadhani nilikosea kutumia ule msemo maarufu wa "Miafrika..." kwa msingi huo basi naomba radhi kwa hilo.

..lets agree to disagree kwenye suala la Prof.Shaba, badala yake turudi kwenye mada kuu inayohusu kifo cha Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine.
 
Back
Top Bottom