Katika safari ndefu, kiongozi anakuwa peke yake , mlinzi na dereva. Nyuma ya gari yake kuna escort na baada ya escort huwa kuna gari la kubebea wasiadizi wake km private secretary, press secretary.
Sokoine alifariki kwa sababu hakuwa amevaa mkanda (safety belt). Dreva na milinzi wake walipona kwa sababu walikuwa wamevaa mikanda.
Tukirudi kwenye hizi conspiracy theories, kama kuna mtu/watu walifanya hila na kumua Sokoine, ni kitu gani kinacho washinda ku msilence Shaba?
Wale wote waliyokuwa kwenye msafara je nao ni part and parcel ya huo mpango?
Hakuna siri zaidi ya mtu mmoja!
Heri asante kwa hii.
Nyie wote wenye conspiracy theory behind kifo cha EMS, endelezeni conspiracy theories zenu, lakini hili la kumuhusisha Mwalimu JKN, ni kutenda dhambi na mtahukumiwa kwa hilo kupitia mahakama ya 'karma'.
Kwa wanaomjua Julius, mimi nilisoma primary enzi zake, kama hakuhitaji, hakopeshi, hutangazwa kwenye habari za saa 2:00 RTD. Alikuwa habembelezi wala hajikombimbi kombi kwa wenye nazo kama wafanyavyo waliopo. Hakuwa na sababu yoyote ya kutumia njio hiyo kumueliminate mtu wakati tunajua there were 1001 ways clean, sefer na more silent ways za kutumika.
Kitu ambacho nakubaliana na baadhi ya wachangiaji, ni kweli ajali na kifo vimetokea kwenye mazingira ya kutatanisha, lakini ukweli unabaki kuwa ni ajali ya kawaida, kama ajali ya Wangwe pia ni ajali ya kawaida lakini watu walisema sana na wanaendelea kusema. Ajali ya Mama Mbatia pia ni ajali ya kawaida, lakini watu weanasema sema. Ajali ya Akukweti ni ajali ya kawaida, lakini watu wamesema, na aliyemrithi amefarikika kwa kifo cha kutatanisha na wameendelea kusema.
Kifo cha Kolimba ni natural death, wakusema wamesema, kofo cha Malima ni natural death, wakusema wamesema. Yaani mkubwa au mtu maarufu akifa kwenye ajali, kuna kitu, tangu anzi za Salum Abdala, alikuwa kwenye siti ya abiria teksi ikagonga mlingoti wa daraja pale moro, mlango ukafunguka, jamaa kachomoka na kuporomea darajani, wakusema wakasema, vivyo hivyo Mbaraka Muhishee nae kafa kwa ajali, wakusema, wamesema, hata mtoto wa Dandu wakusema wamesema, hata hii ya juzi ya Abou Semhondo wakusema wamesema.
Kwa wale tuliopitia kusoma imani za East, tunaelewa, there is nothing new under the sun, whataver happens, hata kiwe ni cha miaka mingapi mbele, it is a pre meditated move, na kitatokea tuu kile ambacho kilikuwa kitokee, hivyo chochote ambacho kinatokea na kusababisha kifo, ndivyo kilivyokuwa kimepangwa na kitokee, na kama kilikuwa hakikupangwa, kifo hakitokei hata ajali iwe mbaya kiasi gani, ndio maana kuna watu wana survive ajali za kutisha huku wengine wakijifia isingizini.
Kifo cha Sokoine ndio siku yake ilifika, na kilikuwa kitokee kwa ajali ya kawaida nothing more nothing less.
RIP Edward Moringe Sokoine.
Pasco.