Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sokoine, atakumbukwa Jumanne hii kwa ibada maalumu ya kumwombea kuadhimisha miaka 27 tangu kufariki kwake, Aprili 12, 1984.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, katika siku hii, kumeandaliwa ibada maalumu ya kumwombea Hayati Sokoine katika kanisa alilosali mara ya mwisho kabla ya kifo chake mjini Dodoma.
Lowassa ambaye ni Kiongozi Mkuu wa jamii ya kabila la Kimasai ‘Olaigwanani' wa Tanzania na Kenya, alibainisha hilo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa kimila na viongozi wa jamii ya Kimasai wa Kanda ya Mashariki yenye mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro uliofanyika Kijiji cha Wami Sokoine wilayani Mvomero.
"Aprili 12, siku ya kifo chake kilichotokea kwa ajali ya gari eneo la Wami Ruhindo, Barabara Kuu ya Dodoma – Morogoro…sisi wana Jimbo la Monduli pamoja na Watanzania wenzetu, tumeandaa ibada maalumu mkoani Dodoma itakayofanyika kwenye kanisa alilosali siku ya mwisho kabla ya kupatwa na mauti yake," alisema.
Alisema kwa vile siku hiyo vikao vya Bunge, vitakuwa vikiendelea, wamepanga ibada maalumu kwa ajili ya Watanzania kumwombea ifanyike katika kanisa ambalo alisali mara ya mwisho mkoani Dodoma.
Aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero kwa kuandaa mipango mizuri ya kupaendeleza mahali alipofia Sokoine kwa ajali ya gari, Kijiji cha Wami Ruhindo, wakati akitokea bungeni Dodoma kwenda Dar es Salaam.
Pamoja na kuusifu uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Mvomero, Lowassa amewataka wafugaji wa jamii ya Kimasai wanaoishi katika vijiji vya Wami Sokoine, Wami Dakawa na Wami Ruhindo kuanzisha vivutio kwa kujenga mgahawa wa kisasa eneo hilo.
Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, alifariki dunia jioni ya Aprili 12, 1984 baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa Afrika Kusini katika eneo hilo la Wami Ruhindo na kupoteza maisha papo hapo.
Ndugu Edward Moringe Sokoine (01/08/1938-12/04/1984) alikuwa Waziri Mkuu wa aina yake nchini Tanzania. Aliongoza katika kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu sana ya kiuchumi. Ni miaka 27 toka Taifa limpoteze shujaa huyu. Katika kuenzi fikra zake ambazo bado zinahitajika sana leo, Ninaomba niwaletee ndugu wana jf baadhi ya nukuu nilivyowahi kuzipata kutoka kwenye Kitabu cha Edward Moringe Sokoine: Kiongozi wa Watu Aliyejitolea kilichoandikwa na Luteni Kanali Albert N. Kigadye mnamo mwaka 1984:
"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asumuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977Nionavyo mie ni kwamba tuna mengi zaidi tunahitaji kujifunza kutoka kwa viongozi wetu waliotutangulia mbele za haki ama kwa kupitia kwenye hotuba zao au kwa kupitia kwenye maandiko mbalimbali.Na kwa kuwa jamii forum ni mojawapo ya maktaba muhimu kwenye uhifadhi wa habari muhimu za ujenzi wa Taifa letu la TANGANYIKA basi ninaona ni heri wote tuisome na kuitafakari kwa pamoja.
![]()
Leo ni miaka 23 tangu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine atutoke ghafla na kuacha simanzi na wingu la huzuni. Siku ile ya machozi na majonzi imebakia katika kumbukumbu za Watanzania wengi kama vile jana. Mfano wake ni kumbukumbu ya Wamarekani waliposikia habari za kuuawa kwa Rais John F. Kennedy. Kila mtu aliyekuwa mtu mzima wakati ule anakumbuka vizuri siku hiyo alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini. Je pengo aliloliacha marehemu limeanza kuzibwa?
Je kuna kiongozi yoyote ambaye anakaribia sifa na utendaji kazi wa Marehemu Sokoine? Leo tunamkumbuka Edward Sokoine.
Pata kidogo chini hapa toka kwa mkuu Kyoma: