Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Kanda2,

Sijasema kwamba Mkapa anahusika wala meya Sykes!.. ila nachosema deal lilianza toka utawala wa Mkapa na nakumbuka deal hilo lilipigwa wakati Sykes akiwa bado meya wa jiji. Wakati huo JK alikuwa bado ni waziri ama niseme rais mtarajiwa. Hii ni pamoja na madeal yote yanayoendelea leo hii nchini ndio maana JK haishi kukimbia nje na kujifanya kipofu...He knows that, he wanted changes but maji mazito bob!
Bongo choo, watammaliza kabla ya wakati wake!
Kulinda gate mwenzangu utaishia kukusanya viti baada ya party na watu kusambaa! yaliyoendelea ndani ni hadithi uliyosimuliwa au sio?.. U got the point!
 
Mkandara,

Unayakana maandishi yako mwenyewe! Now i know wat kind of person ur! Hivi haya huku yaandika wewe?

"Hata hivyo haimfanyi yeye kuwa mjinga, kiongozi mbaya ama mpumbavu. Mwaka 2000 pia nilikuwepo na kama wewe upo ktk vijiwe vyetu utakumbuka kuwa niliwahi kuandika mengi ya wakati ule kule bcstimes. Kwa hiyo haya nayoyaona leo ni mageni kabisa. Mkapa alikuwa na nguvu kubwa sana kama rais na hakuna maamuzi yasiyokuwa na mkono wake ikiwa ni pamoja na mikataba yote."

Ukaendelea kusema yafuatayo;

"Leo hii migawanyo ya mali zote imeisha kamilika, kila kiongozi ana nafasi yake ktk miundombinu, vitega uchumi na kadhalika. Vodafone kashika Rostam na Lowassa, mpumbavu kama mimi huwezi tena kuleta shirika la kupinga unyonywaji wa wananchi ktk muundombinu huo, haikuwa hivyo miaka mitano iliyopita. Umeyasikia ya Citywater, Richmond, n.k ni mambo ambayo yametengenezwa miaka mitano tu ya utawala wa Mkapa na leo hii ndio matunda tunayaona na lawama zetu zinaanzia kwa JK".

Halafu unakana kuwa "hukusema" kuwa Mkapa anahusika na richmond! hata kama kauli hii Umeyasikia ya Citywater, Richmond, n.k ni mambo ambayo yametengenezwa miaka mitano tu ya utawala wa Mkapa na leo hii ndio matunda tunayaona na lawama zetu zinaanzia kwa JK" unayolazimisha tukubali kuwa deal "ilianza" wakati wa Mkapa, je hiyo kauli kuwa mikataba yote ya wakati wa Mkapa ilikuwa na mkono wake nayo haitoshi kumuingiza Mkapa ktk Richmond "iliyoanza" wakati wa Mkapa?

Haya ndio matatizo ya kukurupuka bila kufikiri unajikukuta unachekesha watu.

Kuhusu Sykes ulidai hivi;

"Ndugu Kanda 2, deal la Richmond limjeanza wakati Kreist akiwa Mayor wa jiji. Huyo mhindi aliyewafunga goli amekulia mtaa wa Kipata ambao leo unaitwa Kreist, namjua vizuri - sasa wewe nambie huo ulikuwa wakati gani?.."

Haya! wapi na wapi!

Mie kama mlinda geti wala sina haja ya kujua yaliyojiri ndani, muhimu kwangu ni kuhakikisha hakuna ma- gate-crashers na mwisho wa mwezi navuta!
 
Kanda2,
Yote uliyoyaorodhesha yanadhihirisha wazi kuwa kiswahili ni lugha ngumu kwako.
1. Mkapa alikuwa na nguvu kubwa sana kama rais na hakuna maamuzi yasiyokuwa na mkono wake ikiwa ni pamoja na mikataba yote."

Ndugu yangu mkono ni moja ya kiungo cha binadamu nikiwa na maana kuwa ilikuwa serikali ya Mkapa iliyotuingiza ktk mikataba yote. Hakuna kilichofanyika bila baraka zake na kama kweli wewe unafahamu vizuri lugha hata hiyo Citywater, Mkapa hakuifanya yeye.

2. "Ndugu Kanda 2, deal la Richmond limjeanza wakati Kreist akiwa Mayor wa jiji!

Hii ilikuwa ktk kukukumbusha wewe wakati gani deal hili lilijengewa hoja ya mkataba. Hii nikiwa na maana kwamba wakati Kreist akiwa meya wa jiji JK hakuwa rais bado na ndio Richmond wakati ilipoingia kudai contract. Sasa sielewi reference gani ulipenda niitumie kurudisha kumbukumbu zako.
Nitarudia maelezo ya signature ya ndugu yangu Invisible - Ficha upumbavu usifiche busara zako! hatupo hapa kushindana ila najaribu kukupa facts ambazo wewe huzikubali kwa sababu tu jina nalotumia hapa - Mkapa.
Kumbuka kuna mengi ambayo yamefanyika wakati wa tawala tofauti na kila tunapoyazungumzia haina maana Nyerere, Mwinyi ama JK wamehusika moja kwa moja ila naweza kusema kwamba kutendeka kwake kumetokana na baraka zao kwani hao viongozi wengine wateule ni mikono ya kiongozi mhusika.
 
Mkandara,
hivi siyo kweli kwamba serikali ya Mkapa ilisaini Memorandum of Understang[MOU] na Richmond kujenga bomba la mafuta, na serikali ya Kikwete wao wanahusika na huu mkataba wa majenereta?

Nasema hivyo kwasababu tayari iko "barua" ya Lowassa kwenda kwa Msabaha akimuonya kuhusu malalamiko yaliyoibuka kuhusu Richmond. Vilevile Kikwete alitoa maelezo, naamini in one of his press conferences, kwamba alimuonya Msabaha asijekujitia kitanzi na Richmond.

Zaidi ya hii Richmond, je iko kampuni nyingine ya majenereta ambayo serikali ya Mkapa wanahusika?

NB:
actually habari "nyepesi-nyepesi" ni kwamba Richmond walitaka serikali ya Mkapa waji-commit kwamba hakuna kampuni nyingine itakayopewa mradi wa bomba la mafuta lakini serikali ikasisitiza kusaini Memorandum of Understanding[MOU].
 
Its nice to see the way u advertise ur ignorance! Its simple fact kama mtu akiweka mkono wake mahala then na yeye anahusika. Au wataka kutuambia kuwa uliohusika ni mkono wa Mkapa na sio Mkapa mwenyewe!. Unajikanyaga huku unakubali huku unakataa! wat a game!

Fine, Kleist alikuwa meya wakati wa Mkapa, swali ni anahusika vp na Richmond? Je akija mwingine akisema Athumani Mdoe alikuwa DC Ilala wakati wa Mkapa nae si atakuwa right?

Inavyoelekea hata mgawanyo wa madaraka huujui ukoje kwa kumhusisha meya na Richmond.

Labda tu kukusaidia iko hivi Tanesco-Wizara ya nishati-Rais na upande huu ni Jiji-wizara-Tamisemi-Rais

Nitafutie Kleist hapo na Richmond!
 
Jakakuu,
Huo ndio mwanzo wa hawa jamaa Richmond kujihusisha na maswala ya uwekeshaji nchini. My point ni kwamba yule mhindi ni mtu ambaye ametumiwa kama wanavyotumiwa wahindi wengine kuficha makucha ya baadhi viongozi. Deal la Richmond liliundwa toka Mkapa akiwa madarakani na imekuja kupita wakati wa JK lakini wahusika wakubwa hawakubadilika. Mkapa kama rais alielewa kinachofanyika nchini na hata huyu JK.
Sote leo hii tumekuja gundua kuhusu Richmond kuwa ni kampuni feki imekuwaje walikuwepo ktk orodha za wawekeshaji wakati wote. Hii ndio lugha anayoshindwa kuielewa mzee wangu Kanda2 kwa sababu kati ya Mkapa na JK anafikiri kuna tofauti za kiutawala ndani ya CCM..

Kanda2,
Hilo swala la kreist naona bado walishikia bango. Lakini hata hivyo nitakujibu ya kwamba kama akija mtu na kudai kuwa Athumani Mdoe alikuwa DC Ilala wakati wa Mkapa basi nitapiga hesabu kujua lini swala hilo limetokea na sio kwamba Mdoe ni mhusika, Lugha nyepesi kabisa. Nikirudi ktk swala la mkono ni kwamba kila lililotendeka wakati wa Mkapa, yeye ni mhusika kwani kiongozi aliyetenda ni mkono wa Mkapa. Tunaposema serikali ina mkono mrefu sijui wewe mwenzangu unaelewa vipi?
 
Mkandara,
nimekupata!!....yaani ungekuwa mwalimu basi mitihani yako ingekuwa MIGUMU na lecture notes zako NDEEFU. Nadhani unachojaribu kusema ni kwamba madalali wa hili dili ni walewale, waliobadilika labda ni waidhinishaji tu.

unajua mabadiliko hayawezi kutokea Tanzania bila Watanzania kuunganisha utendaji/uozo/maovu ya serikali zetu na VYAMA.

Unajua nchi kama USA Chama kilichoko madarakani kikishindwa Uchaguzi kila Mteule wa Raisi aliyepita hupoteza kazi yake. Wananchi wakichagua Chama kingine ni kwamba wamechagua MABADILIKO.

Watanzania walipochagua Kikwete/CCM wajue kwamba wamekubali kuendelea na MEMA, MAOVU, UOZA, UBADHIRIFU, na UZANDIKI, wa Mkapa.
 
Jokakuu,

Hili dili la bomba la Mafuta Richmond walipigwa chini! kwa kufuata mantiki ya Mh Mkandara kuwa kila Mkataba Mkapa alikuwa na mkono then tukubali kuwa Richmond Mkapa aliipiga chini lakini Kikwete ndio kaja kuivaa! Thanx kwa ufafanuzi.


Mkandara,

That was exactly my point! kwamba kuwa kiongozi wakati wa Mkapa haina maana kuwa fulani ahahusika na deal fulani. Ndio maana nikakuuliza Meya Kleist anahusika vp na deal la Richmond, unanipiga chenga tu jibu hunipi.
 
Kanda 2,

Nimesema kuwa nimetumia jina la Kreist kukuonyesha ni wakati gani deal hilo linapangwa, sina mfano mzuri labda ningesema Lowassa alikuwa sijui waziri wa....lakini hata hivyo naye hakuwa waziri mkuu na bado yupo serikalini kwa hiyo picha nzima huwezi kuipata vizuri.

Kupigwa chini kwa Richmond ktk mafuta ni mpango uliokuwa umepangwa toka zamani na umekuwa ukigombewa na viongozi wengi kwa maslahi yao toka enzi ya Mkapa. Richmond alikuwa akitumiwa na kundi fulani tofauti na kundi jingine, leo hii unajua ni nani kachukua deal la mafuta?... Je nikisema hilo deal lilikuwepo toka wakati wa Mkapa utasema pia haiwezekani?

Tunachobishana hapa ni wakati sio nani! wahusika ni walewale isipokuwa kila mmoja wao ana speed zake na nyavu zao zimaisha tupwa baharini. Labda nikukumbushe tu kuwa viongozi wetu wote wameisha weka mitego yao na mengi hutayaona leo ama kesho lakini usukuji upo na unaendelea kila kukicha.

Hapa Canada kuna deal moja limekiangusha chama kizima ktk utawala na kumwondoa waziri mkuu ambaye deal deal lilisukwa akiwa bado waziri wa fedha hakuhusika moja kwa moja. Wenzetu wameweza kukihukumu chama kizima pamoja na kwamba waziri mkuu aliyekuwa madarakani kisha staafu na kesi ilirushwa ubaoni - bungeni.

Sisi wadanganyika tunatazama nani rais ili kutafuta mchanga wa macho kumrushia hali sii rais tunayetakiwa kumtazama ila chama kizima.
 
Mkandara,

Kwa hili nakubaliana na wewe.. Bado kidogo tutaanza kuona dili zilizosukwa na JK na timu yake. Hivi sasa nyingi kati ya hizo ni dili zilizoanza kutengenezwa toka nyuma. Ununuzi wa rada ingawa ulihitimishwa wakati wa Mkapa, dili ilianza kuchongwa enzi za Mwinyi.

Suala la kutafuta majenereta ya kuzalisha umeme hayakuja baada ya matatizo ya mwaka jana bali dili ilianza kusukwa miaka michache iliyopita ambapo mtoto (inadaiwa ni mtoto) wa kiongozi mmoja wa Ngazi za juu (hizi za chini huwa hazizungumzwi) alihusika kutafuta fedha za kampeni na katika kubadilishana dili akachonga hiyo ya Richmond!
 
Hi Bob Mkandara

Its good to have you back.

watu wengi wanashindwa kuelewa, bongo hii yetu hii hii, dili za seriakli yetu zinaanzaje na mpaka unasikia majina ambayo wakati mwingine hata mahusiano ya mikataba unashangaa, Kutajwa kwa Kleist ktk hili dili si ajabu kabisa hata kama hayuko ktk mlolongo wa idara husika, bongo kuna kitu chaitwa "Deal Network" sasa wewe kama ofisa wa serikali jifanye mjanja na mwerevu, ndipo unapokanyaga maboya.

Nafikiri ni wachache wataelewa nichosema hapa, wengi yamewakuta tena kwa makusudi ya kutetea maslahi ya Taifa, kama huamini just for an example ULIZIA MRADI WA TWIN TOWERS BoT ULIANZA LINI na kwanini ulikuwa unapigwa tarehe, halafu ULIZIA THE FINAL DEAL ILIKUWAJE, HALAFU ULIZIA WAHUSIKA....ndio utashangaa, weee leo unashangaa kutajwa Kleist!!!, hivi uko bongo weweee au uko wapi, na kama uko bongo basi HUIJUI VYEMA SERIKALI YAKO

Anyway the MADA here is Tumkumbuke Sokoine, nahisi tungekuwa naye leo hii maupuuzi yote haya atleast tusingekuwa tunayashuhudia, kwani "angekula sahani moja" nao

Kyoma
Shusha vigongo vingine maana maswali ya DrWHO kuhusu vigongo vyako naona hayapo tena
 
Mwkjj,

Swali langu ni dogo tu je Mkapa na Kleist wanahusika na Richmond au hapana? if yes, then how! (kaushahidi) basi.

Mkandara,

Suala kwangu mimi ni muda na watu! Je Kleist na Mkapa wanahusika?

Ogah

Sitoshangaa kusikia kuwa fulani anahusika ktk deal fulani hata kama hiyo sio line yake ya kazi, lakini nitakapo thibitishiwa uhusika wa Kleist kwenye Richmond then tumemaliza! Tatizo hapa ni Mkandara ktk posts zake anajichanganya hii anasema yumo nyingine anasema hapana hayumo ni mfano tu wa viongozi wakati wa Mkapa which is which Mr Mkandara?
 
Kanda2,
Nionyeshe mahala niliposema Kreist anahusika na Richmond?
Nilichosema mimi Krest alikuwa meya na ndio wakati hata mimi nilisikia habari za Richmond kuwa ktk orodha ya Tender hiyo!
Mkapa anahusika akiwa rais wa nchi na labda niongezee kusema CCM wanahusika na mabalaa yote yanayotukumba. sasa niulize wapi CCM imehusika vipi?... mbona itachekesha!
 
Thats better now, kwa hiyo tunakubaliana kuwa Kleist hayumo! Kilichokuponza hapa ni statement yako kuwa deal la richmond lilianza wakati Kleist akiwa meya. By implication hapa ni kuwa Kleist nae anahusika if not kwa nini umtaje meya ambae hana dhamana yeyote katika wizara ya Nishati. Na suala la umeme ni la nchi wala sio la Jiji la Dar Es Salaam peke yake. At least ungemtaja waziri Yona basi mzee. Anyway ufupi ni Kleist hayumo.

Sasa turudi kwa Che Mkapa swali langu bado ni valid, to the best of my knowledge tarehe 23. June, 2006 uliposainiwa mkataba wa Richmond Mkapa alishatoka madarakani. Je ahusika vp hapo? Kama nitaichukua kauli yako ya mwisho kuwa CCM ndio wanahusika hapo sina tatizo. Je Mkapa anahusika vp na Richmond Mkandara pls
 
eeeh kanda2 naona wewe ni wakili maana inajua kweli kuwaweka watu kwenye kona. Labda niongezee hapo kaswali kidogo: hata kama mipango ya Richmond ilisukwa wakati wa Mkapa, je by the fact kwamba mkataba haukusainiwa hadi hiyo tarehe 23/06/06 wakati wa ndugu yetu muungwana msanii, sio sahihi kusema kwamba hawa wasanii walikuwa na uwezo wa kisheria na mamlaka kuacha kusaini? Kaswali kapili: kadri tulivyotaarifiwa na wasanii wetu, Richomond ilikuja kama njia ya dharura ya kukabiliana na tatizo la umeme, sasa iweje tena tusema kuwa mipango ilisukwa siku nyingi tangu enzi za Mkapa?

Haya leteni majibu wajemeni: Mwanakijiji na Mkandara
 
Kanda2 na Kitila,

Mwendo ni hatua ndugu zangu taratibu.

Hivi niambieni kila rais anapoingia madarakani huondoa hata watendakazi na deal zote zinazohusiana na maendeleo ya nchi?...
Nitarudia kusema Tanesco walilazimishwa kuweka mkataba ktk deal ambalo lilikwisha sukwa toka enzi ya Mkapa. Tanesco ni moja ya miundombinu ya taifa na Mkapa kama rais wanchi pamoja na JK wote ni wahusika kwa kukubali kuwepo kwa jina la kampuni ambayo ni ya uongo.

Kama tunavyozungumzia vyeti feki leo hii, wahusika wote walichukua mwanya ama nafasi iliyokuwepo wazi toka wakati wa Mkapa na ikiwa trend kwa viongozi wengi. Kwa hiyo basi yeyote anayefuzu mafunzo yake leo hii Pacific Open ni tunda la mbegu iliyopandwa toka enzi zile. laukama Mkapa angepiga marufuku kabisa shule hizo kuwepo ktk orodha ya vyuo vinavyotambulika basi leo hii tungekuwa tukizungumza habari tofauti. Serikali ya Mkapa ilifahamu kuwa Richmond ni kampuni feki akiwepo JK na Lowassa wote hawa chini ya CCM hata kama ilipoteza tender fulani na kuja pata nyingine kama vile msomi wa Pacific aliyekosa kazi Chuo kikuu akaja fundisha Mzumbe!..

Kanda2, kusainiwa Mkataba ni tarehe ya kupitisha kitu kile kama vile leo hii tunavyopendekeza muswada wa Rushwa ambao unaweza pitishwa na kuwekwa sahihi wakati wa Lowassa!

Nitarudia kusema kwamba ni wakati wa Nyerere tulipopitisha mfumo mpya wa soko huria nchini lakini sifa zote zinamfuata Mwinyi. July 1984 ilitangazwa hali muswada huo ulikuwepo bungeni miaka miwili nyuma yaani toka 1982.....bado mpo?
 
Mkandara,

Mfano wako wa Pacific Uni ni mzuri sana, lets extend the line of argument there.. Huyu msomi wa Pasicif aliputwa na UDSM na na baadae kupata kazi Mzumbe akija mtu akasema aliyehusika kumwajiri huyu msomi ni Prof Rwekaza Mukandara (sio wewe mzee ni yule msanii wa pale REDET) VC wa UDSM na sio Prof Warioba wa Mzumbe ina sound kuwa kweli? na Je Prof Warioba unataka kuniambia hakuwa na uwezo wa kusema hapana?

Ukweli utabaki kuwa Richmond ni ya JK, Lowassa na genge lao. Ben alishakamua kwenye Gulf Stream zamani!
 
Kanda2, ulipoamkia wewe ndiko nilikolala mimi majuzi!

huo mfano wako bado kabisa haujengi hoja zaidi ya kupotosha maana. nachojaribu kusema mimi hapa ni kwamba huyo Mukandala pamoja na kumkataa msomi kwa sababu zake binafsi haijengi hoja ya kuwa msomi huyo ni feki na hata kama warioba atakuja mwajiri huyo msomi bado hana makosa kwa sababu hizi hizo. yaani sheria haikubali kuwa cheti cha pacific ni feki!

Utata wangu unakuja pale Mukandala anapokubali kusajiliwa kwa msomi feki lakini kutokana na sababu zake binafsi amnyime ajira, kisha huyu msomi apate ajira sehemu nyingine lawama apewe Warioba wakati sii Warioba anayetoa ajira za mzumbe ila wapo watu waliojenga nafasi hiyo. Kwa maana hii ninasema sii wakati wa JK jina la Richmond limejitokeza kama mwekeshaji na wala sii JK anayetoa hukumu ya nani atakuwa mwekezaji wa tender ya Umeme nchini bali matokeo ya tender hiyo ni mipango mirefu iliyoandaliwa toka enzi za Mkapa.

Hii haina maana JK ni victim ama hana makosa ila kuhusika kwa Richmond na Umeme Dar kumejitokeza toka enzi za Mkapa na yawezekana kuwa msukaji ni huyo huyo Lowassa kama anavyoshikilia Vadafone ambayo mipango yake pia lianza toka enzi za Mkapa. Kifupi bob haya mambo yanajitokeza leo na yawezekana kabisa kuwa JK alionekana dhaifu na hivyo jina lake kuwa mbele ya macho yetu ili mipango mingi ipate nafasi. Kuna kila haja ya kurudia kutazama mikataba mingi nchini na nakuhakikishia kuwa kama itatokea hivyo basi Mkapa atakuwa rais wa kwanza kunyongwa hadharani!...

Lipeni bunge nafasi hiyo kisha mtajionea ya Mussa!
 
Kanda2.... unajua kwanini Balozi Daraja alikwenda Houston na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Richmond Development Co. Hii ilikuwa ni Julai 2003 (wakati huo Rais alikuwa ni... )
 
Kyoma
Shusha vigongo vingine maana maswali ya DrWHO kuhusu vigongo vyako naona hayapo tena

Mzee Ogah, heshima yako Baba!

Well, kwanza naungana na wewe kumkaribisha Mzee Mkandara na kumalumu kwa kutokunipitia hapa kwa Mfugwa Mbwa. Pili, nimekusikia na nitarudi kumalizia kiporo kilichobakia katika amamu nne tofauti. Kwanza nitamalizia mtililiko wa hoja ya Majangiri wa WB na IMF na mwishowe kutoa mapendekezo yangu ya nini kifanyike kujinusulu katika hiki kitanzi tulichojiingiza.

Ingawa Mzee Mkandara amesema huko nyuma kuwa hakuna umuhimu wa kumlinganisha Sokoine na Lowasa, lakini mimi naona umuhimu huo upo. Kwasababu hii hoja inamuhusu Sokoine, hakuna njia nzuri ya kumkumbuka kama tusipoelezea mazingira aliyofanyia kazi, alichosimamia, na jinsi alivyofanikiwa au shindwa.

Ni vema pia tukawachungulia baadhi ya viongozi, hasa wanaotaka kutughilibu kwa kujifananisha naye. Nadhani nina jukumu la kumalizia kiporo cha Lowasa na Sokoine kabla sijabwaga manyanga na kusubili mdongo kutoka kwa Mzee Mkandara ambaye mara nyingi hupendelea kunionea kwa kunifanya gunia la mazoezi. Ngoja kwanza niweke mkono kinywani, alafu nitarudi. Si unajua ajira ni haba?
 
Back
Top Bottom