Mkandara,
Unayakana maandishi yako mwenyewe! Now i know wat kind of person ur! Hivi haya huku yaandika wewe?
"Hata hivyo haimfanyi yeye kuwa mjinga, kiongozi mbaya ama mpumbavu. Mwaka 2000 pia nilikuwepo na kama wewe upo ktk vijiwe vyetu utakumbuka kuwa niliwahi kuandika mengi ya wakati ule kule bcstimes. Kwa hiyo haya nayoyaona leo ni mageni kabisa. Mkapa alikuwa na nguvu kubwa sana kama rais na hakuna maamuzi yasiyokuwa na mkono wake ikiwa ni pamoja na mikataba yote."
Ukaendelea kusema yafuatayo;
"Leo hii migawanyo ya mali zote imeisha kamilika, kila kiongozi ana nafasi yake ktk miundombinu, vitega uchumi na kadhalika. Vodafone kashika Rostam na Lowassa, mpumbavu kama mimi huwezi tena kuleta shirika la kupinga unyonywaji wa wananchi ktk muundombinu huo, haikuwa hivyo miaka mitano iliyopita. Umeyasikia ya Citywater, Richmond, n.k ni mambo ambayo yametengenezwa miaka mitano tu ya utawala wa Mkapa na leo hii ndio matunda tunayaona na lawama zetu zinaanzia kwa JK".
Halafu unakana kuwa "hukusema" kuwa Mkapa anahusika na richmond! hata kama kauli hii Umeyasikia ya Citywater, Richmond, n.k ni mambo ambayo yametengenezwa miaka mitano tu ya utawala wa Mkapa na leo hii ndio matunda tunayaona na lawama zetu zinaanzia kwa JK" unayolazimisha tukubali kuwa deal "ilianza" wakati wa Mkapa, je hiyo kauli kuwa mikataba yote ya wakati wa Mkapa ilikuwa na mkono wake nayo haitoshi kumuingiza Mkapa ktk Richmond "iliyoanza" wakati wa Mkapa?
Haya ndio matatizo ya kukurupuka bila kufikiri unajikukuta unachekesha watu.
Kuhusu Sykes ulidai hivi;
"Ndugu Kanda 2, deal la Richmond limjeanza wakati Kreist akiwa Mayor wa jiji. Huyo mhindi aliyewafunga goli amekulia mtaa wa Kipata ambao leo unaitwa Kreist, namjua vizuri - sasa wewe nambie huo ulikuwa wakati gani?.."
Haya! wapi na wapi!
Mie kama mlinda geti wala sina haja ya kujua yaliyojiri ndani, muhimu kwangu ni kuhakikisha hakuna ma- gate-crashers na mwisho wa mwezi navuta!