Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Walio kufa kwa amri ya Nyerere{hapa wakuu namaanisha yeye kama amiri jeshi mkuu msinihukumu} labda ni wale wa vita ya Kagera nasikia watu walikufa sana kuliko inavyo tangazwa na ilivyo andikwa....wazee wa huko wanajua nini kilicho tokea enzi hizo.
 
Walio kufa kwa amri ya Nyerere{hapa wakuu namaanisha yeye kama amiri jeshi mkuu msinihukumu} labda ni wale wa vita ya Kagera nasikia watu walikufa sana kuliko inavyo tangazwa na ilivyo andikwa....wazee wa huko wanajua nini kilicho tokea enzi hizo.

fidel.. askari kufa vitani ni sehemu ya kazi yake. Unless unataka kusema Nyerere aliwapangisha mstari na akiwa Amiri Jeshi Mkuu akaamuru wapigwe risasi.

Ndiyo hicho unachomaannisha? Kaama kama ni kufia vitani au kazini basi Urais watu wangekuwa hawautaki.
 
Baba Wangapi Waliliwa Na Fisi Wakati Wa Vijiji Vya Ujamaa?kasimu Hanga,twala,sokoine,karume. Sasa Jaza
 
watajeni basi jamani hatakama ni wafununu watajeni tuu

Yep..Kabla ya mauti kumkumba, Sokoine alishakamata barua mbili kutoka kwa Msuya na Kawawa wakipanga mpango wa kumuua .Akamtaarifu Nyerere, naye Nyerere akamuhakikishia kuwa hakuna baya litakalompata.

Sasa sijui kama hawa wawili walikuja maliza hilo deal lao au kuna wengine walikuja kuli-implement kabla yao.
 
Moja Ameuwa Ufahamu Wako Only Have Now Is Highly Claiming Capasity Wisdom And Understanding Zero.pili Jamaa Kakujibu Hapo Juu


Baba Wangapi Waliliwa Na Fisi Wakati Wa Vijiji Vya Ujamaa?kasimu Hanga,twala,sokoine,karume. Sasa Jaza

Pezzo,

Labda wengine wanakuelewa - mimi nimeshindwa, duh. Hata hivyo kwa ufahamisho wako aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar si mwingine bali Field Marshall Okelo na ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi 1964. Wakati huo akina Karume, Babu na wengineo waliikimbia Zanzibar na kupata hifadhi Tanganyika. Ni Nyerere huyo huyo aliyeweza kuhakikisha kuwa Mamluki Okelo hatwai Uraisi wa Zanzibar na hivyo Karume kuukwaa uongozi on a silver platter.

Sokoine alikuwa kipenzi wa Nyerere na kama kuna kilichomfanya Mwalimu kusalimu amri na kukubali kung'atuka ni hicho kifo. Matumaini ya Mwalimu kwa Tanzania kupata kiongozi bora baada yake yalikufa siku hiyo. Kusema alihusika na kifo cha Sokoine ni kuonyesha utaahira mkubwa wa akili.
 
Pezzo,

Labda Wengine Wanakuelewa - Mimi Nimeshindwa, Duh. Hata Hivyo Kwa Ufahamisho Wako Aliyeongoza Mapinduzi Ya Zanzibar Si Mwingine Bali field Marshall Okelo Na Ndiye Alikuwa Mwenyekiti Wa Kwanza Wa Baraza La Mapinduzi 1964. Wakati Huo Akina Karume, Babu Na Wengineo Waliikimbia Zanzibar Na Kupata Hifadhi Tanganyika. Ni Nyerere Huyo Huyo Aliyeweza Kuhakikisha Kuwa Mamluki Okelo Hatwai Uraisi Wa Zanzibar Na Hivyo karume Kuukwaa Uongozi On A Silver Platter.

Sokoine Alikuwa Kipenzi Wa Nyerere Na Kama Kuna Kilichomfanya Mwalimu Kusalimu Amri Na Kukubali Kung'atuka Ni Hicho Kifo. Matumaini Ya Mwalimu Kwa Tanzania Kupata Kiongozi Bora Baada Yake Yalikufa Siku Hiyo. Kusema Alihusika Na Kifo Cha Sokoine Ni Kuonyesha Utaahira Mkubwa Wa Akili.

Sorry Sir Kwa Kuweka Jina La Sokoine Kwenye Wale Elfu Waliokufa Wakati Wa Callya Nyerere, lakini Wakatiti Nyerere Akiwa Raisi Wa Jamuhuri Ndipo Kassim Hanga, sarehe Twala, idrissa, Na Wengine Wengi Waliuwawa,naluda Tena Jina La Sokoine Niliteleza.
 
jamani mshutumuni mwalimu kwa mengine, lakini hili la sokoine mmmh naona vigumu kuamini.

hata hivyo siku zote nimekuwa najiuliza "kwa nini hakuvalia njuga wazi wazi (huenda alifanya hivyo kimya kimya) hizi fununu za mkono wa mtu katika kifo cha sokoine?" huenda kwa busara zake aliona kuchokonoa kuhusu kifo hicho kungekuwa na madhara zaidi kwa nchi kuliko kwa kukaa kimya.
 
Mimi napingana na hoja hii kwa sababu hizi:
1. Nyerere alikuwa anamuandaa Sokoine achukue nchi baada yake kwa hiyo hakukukuwa na sabau ya kutishika kwa umashuhuri wa Sokoine. Sokoine aliuawa 1984 na Nyerere aling'atuka 1985 na akamuachia Mwinyi kwa hiyo utaona ni kweli Nyerere alikuwa anajiandaa kuondoka hivyo Sokoine si tishio
2. Sokoine hakuwahi kupingana na sera za ujamaa na kujitegemea wala hakuwahi kutofautiana na sera za Nyerere. Kwanini basi Nyerere amuue? Hakuna sababu
3. Sokoine aliuawa na wahujumu uchumu ambao kwao Sokoine alikuwa tishio

Hivi nani kasema mwalimu alikuwa anamuandaa sokoine?

Kama nyerere alijua anauwa kweli angeshindwa kutoa maamuzi na kuhakikisha marehemu anapanda ndege na hata kuwatumia intelligency agents wake?

Napata kigugumizi hapa.
 
Sio Pope tu; nimejaribu kuisoma hiyo thread na kurudia sijaielewa. Kiswahili sio na kiingereza sio.

Hicho ni kiswahili lakini ni vigumu sana kujua ni cha wapi. Kinafanana na kiswahili cha Congo DRC, lakini ujumbe wake unaeleweka. Anataka kujua kama ni kweli Nyerere alibariki kuuawa kwa Sokoine.

Did he? If yes why? If not why and why did it happen under his watch what did he do afterwards? Naona hayo ni maswali yake inagwa kiswahili kimempiga chenga kidogo.
 
Baba Wangapi Waliliwa Na Fisi Wakati Wa Vijiji Vya Ujamaa?kasimu Hanga,twala,sokoine,karume. Sasa Jaza

wenzio walijaribu hiyo gear ya "vijiji vya ujamaa"; hadi leo hajajitokeza mtu hata mmoja ambaye ameweza kutoa madai au uthibitisho kuwa:

a. Ndugu yake aliliwa na fisa au simba
b. Huyo ndugu yake aliwahi kuwepo!
c. Hakuna mtu mwenye idadi ya kusema ni wangapi waliliwa na wanyama na wapi.

Nimesikia habari hizi siku nyingi kweli lakini hadi leo hakuna ushahidi wa kuonesha kama kuna mtu aliliwa na simba au fisa ni sababu ya vijiji vya ujamaa kwani hadi leo hii kuna maeneo bado watu wanaliwa na fisi, simba na sungura!! na hakuna harakati za vijiji vya ujamaa. So, kama una ushahidi angalau wa mtu, kijiji, au mahali ambapo watu "maelfu" waliliwa na wanyama useme au nipe contacts mimi nitafuatilia.
 
Sorry Sir Kwa Kuweka Jina La Sokoine Kwenye Wale Elfu Waliokufa Wakati Wa Callya Nyerere,lakini Wakatiti Nyerere Akiwa Raisi Wa Jamuhuri Ndipo Kassim Hanga,sarehe Twala,idrissa, Na Wengine Wengi Waliuwawa,naluda Tena Jina La Sokoine Niliteleza.

Basi tuwe tunahakiki maandishi, mi sijaelewa au ndio kukaa Italy muda mrefu tunasahau maneno ya kiswahili, hapo nimetoka bila mkuu.
 
wenzio walijaribu hiyo gear ya "vijiji vya ujamaa"; hadi leo hajajitokeza mtu hata mmoja ambaye ameweza kutoa madai au uthibitisho kuwa:

a. Ndugu yake aliliwa na fisa au simba
b. Huyo ndugu yake aliwahi kuwepo!
c. Hakuna mtu mwenye idadi ya kusema ni wangapi waliliwa na wanyama na wapi.

Nimesikia habari hizi siku nyingi kweli lakini hadi leo hakuna ushahidi wa kuonesha kama kuna mtu aliliwa na simba au fisa ni sababu ya vijiji vya ujamaa kwani hadi leo hii kuna maeneo bado watu wanaliwa na fisi, simba na sungura!! na hakuna harakati za vijiji vya ujamaa. So, kama una ushahidi angalau wa mtu, kijiji, au mahali ambapo watu "maelfu" waliliwa na wanyama useme au nipe contacts mimi nitafuatilia.

Vita ya ufisadi imetukaa sana, lazima tushinde hata kwa fikra, maana fisa di ni adui wa maendeleo ya watanzania
 
Mimi sina 'uvumi' wo wote kumhusisha Nyerere na kifo cha Sokoine ambaye walaji wa enzi hizo walimwua kwani alivalia njuga kukamatwa, kunyang'anywa mali/pesa na kushitakiwa watu katika Mahakama ya John Nzunda kwa kile kilichokaitwa "wahujumu uchumi". Kwa wale wanaokumbuka, hii ilikuwa mara ya kwanza nchini Bongo WATUHUMIWA KUTIWA RUMANDE "KABLA" YA SHERIA YA UHUJUMU HAIJAPITISHWA BUNGENI!! Ni wazi Nyerere ndiye aliyehusika kwa kuruhusu huo UKIUKWAJI WA HAKI ZA RAIA basi wananchi wakakasirika....

Mada ya Nyerere na idadi ya watu alioua ni rahisi kuijibu na ndio maana hata Papa anasita kumpa "Utakatifu".

1) Akiwa Kamanda anawajibika moja kwa moja kwa mauaji yanayofanywa na Wanajeshi wake. Yeye ndiye ALIYEIDHINISHA UVAMIZI WA UGANDA (bila idhini ya OAU), NIGERIA KWA KUISAIDIA BIAFRA, NA SHELISHELI (ndege za ATC zilibeba Wanajeshi na silaha kinyume cha sheria za ICAO/IATA) - mote humo walikufa Watanzania na "maadui".

2) Alisaini KUNYONGWA KWA MWANDIMU, MKULIMA WA KIHESA, IRINGA aliyemwua Dk. Kleruu "aliyemchokoza mara nyingi na kumnyang'anya mashamba yake kwa nguvu" - hiyo ni provocation haki yake angehukumiwa kwa manslaughter lakini kwa sababu za kisiasa (kupinga vijiji vya ujamaa) Nyerere akamwua!

Hawa wanatosha hata bila ya kuwataja waliofia "kizuizini" (detention) bila kushitakiwa au wengine walioozea jela kwa MAJARIBIO MAWILI YA KUMPINDUA (Army mutiny aliyo-msave Kambona na Mapinduzi ya "Kamandoo wa Mkwajuni", akina Roderick Roberts na MacGhee!! AU MMESAHAU??
 
...

Mada ya Nyerere na idadi ya watu alioua ni rahisi kuijibu na ndio maana hata Papa anasita kumpa "Utakatifu". 1) Akiwa Kamanda anawajibika moja kwa moja kwa mauaji yanayofanywa na Wanajeshi wake. Yeye ndiye ALIYEIDHINISHA UVAMIZI WA UGANDA (bila idhini ya OAU), NIGERIA KWA KUISAIDIA BIAFRA, NA SHELISHELI (ndege za ATC zilibeba Wanajeshi na silaha kinyume cha sheria za ICAO/IATA) - mote humo walikufa Watanzania na "maadui".

Hivi Rais wa Tanzania katika kutangaza vita au kuamuru vikosi vyake kupigana yuko chini ya Katiba ya nchi gani? Je anahitaji OAU kubariki vita hivyo? Hoja yako ingekuwa na nguvu kama ungeonesha ni kipengele gani cha Katiba YETU alichokivunja. Yaani, Tanzania ivamiwe na nchi nyingine halafu sisi tukae na kuipigia magoti OAU kuomba ruhusu ya kumtimua mvamizi kutoka ardhi yetu?



2) Alisaini KUNYONGWA KWA MWANDIMU, MKULIMA WA KIHESA, IRINGA aliyemwua Dk. Kleruu "aliyemchokoza mara nyingi na kumnyang'anya mashamba yake kwa nguvu" - hiyo ni provocation haki yake angehukumiwa kwa manslaughter lakini kwa sababu za kisiasa (kupinga vijiji vya ujamaa) Nyerere akamwua! [/quote]

Mahakama ilitoa hukumu, na Rais Nyerere baadaye aliidhinisha kifo hicho. Yeye mwenyewe alizungumzia ugumu wa kutoa sahihi hizo wakati anastaafu mwaka 1985. Jaribu kulinganisha kesi alizotia sahihi Nyerere watu wanyongwe na zile zilizotiwa sahihi na Mwinyi au Mkapa. Na hata hivi sasa sijui Kikwete amesharidhia wangapi Wanyongwe. Lakini zaidi bado hujasema ni sheria yetu ipi au kipengele gani cha Katiba Nyerere alivunja. Siyo suala la vionjo tu.

Hawa wanatosha hata bila ya kuwataja waliofia "kizuizini" (detention) bila kushitakiwa au wengine walioozea jela kwa MAJARIBIO MAWILI YA KUMPINDUA (Army mutiny aliyo-msave Kambona na Mapinduzi ya "Kamandoo wa Mkwajuni", akina Roderick Roberts na MacGhee!! AU MMESAHAU??

Bado hujafanikiwa; jaribu kutuambia ni ki nani hawa "maelfu waliouawa kwa amri" ya Nyerere. Taja watu waliouawa kwa amri ya Nyerere siyo waliokuwa katika utekelezaji wa tendo la kisheria au amri halali ya mahakama. Mtu anaposema kwa amri ya "fulani" ina maana amri ya kidikteta ambayo ni extra judicial. Sasa, naomba ujaribu tena kuorodhesha orodha ya watu ambao Mwalimu aliamuru wauawe.
 
Mjadala wa kilichomuua Edward Sokoine ni wa siku nyingi ila mimi naona ni katika mwendelezo wa "nasikia eti" za Watanzania.

My suspiciuos minds tends to believe:
1: Kama wana-nadharia wa kundi la kwanza wanavyosema... kama mwalimu J. K. Nyerere alikuwa anamchukia na akaona anakuwa tishio; Nyerere akiwa kama rais alikuwa na njia nyingi tu za kumdhooofisha bila kumuua.

2. Kama wana-nadharia wa kundi la pili wanavyosema... kama Cleopa Msuya na Rashidi Kawawa (and/or others) walikuwa wanamchukia na wakaona anakuwa tishio... na WAKAHAKIKISHA AMEUAWA.... mwalimu Nyerere lazima angefahamu... Na asingenyamaza... lazima kungekuwa na some sort of displinary action kwa hao wahusika.
Assignment:

1.Naomba mnieleze kwa nini Nyerere aliamua kuuchuna (kama kweli Sokoine aliuawa na kina Kawawa/Others???
 
1. Charles Taylor yuko Hague kwa mauaji ya Sierra Leone ambako wala "hakushiriki yeye binafsi" - ni amri yake tu kwa vikosi vyake.

2. Nyerere mbona alimsamehe Mwalimu wa Kike aliyeua watoto wake watatu (akabaki mmoja - mtangazaji kijana maarufu, jina ninalo) baada ya kuombwa na UWT (akina Ms Mongela) mwaka 1977?

3. Nimezungumzia UVAMIZI an sio vita. Nyerere aliyaingiza majeshi yetu Uganda na wla hakumfukuza Idi Amini mpakani tu ila alihakikisha anmng'oa kabisa ATAWALE RAFIKI YAKE OBOTE. Hivi hamkumbuki alivyowachezea akina LUKLE NA BINAISA kama watoto wadogo amri zikitoka Msasani?

HEBU WEE TUACHE TU .... UKIMPENDA MTU MADHAMBI YAKE HUYAONI!!
 
Mjadala wa kilichomuua Edward Sokoine ni wa siku nyingi ila mimi naona ni katika mwendelezo wa "nasikia eti" za Watanzania. My suspiciuos minds tends to believe:
1: Kama wana-nadharia wa kundi la kwanza wanavyosema... kama mwalimu J. K. Nyerere alikuwa anamchukia na akaona anakuwa tishio; Nyerere akiwa kama rais alikuwa na njia nyingi tu za kumdhooofisha bila kumuua.
2. Kama wana-nadharia wa kundi la pili wanavyosema... kama Cleopa Msuya na Rashidi Kawawa (and/or others) walikuwa wanamchukia na wakaona anakuwa tishio... na WAKAHAKIKISHA AMEUAWA.... mwalimu Nyerere lazima angefahamu... Na asingenyamaza... lazima kungekuwa na some sort of displinary action kwa hao wahusika.
Assignment:
1.Naomba mnieleze kwa nini Nyerere aliamua kuuchuna (kama kweli Sokoine aliuawa na kina Kawawa/Others???

Swali la hekima sijapata ona tena ...
 
1. Charles Taylor Yuko Hague Kwa Mauaji Ya Sierra Leone Ambako Wala "hakushiriki Yeye Binafsi" - Ni Amri Yake Tu Kwa Vikosi Vyake.

2. Nyerere Mbona Alimsamehe Mwalimu Wa Kike Aliyeua Watoto Wake Watatu (akabaki Mmoja - Mtangazaji Kijana Maarufu, Jina Ninalo) Baada Ya Kuombwa Na Uwt (akina Ms Mongela) Mwaka 1977?

3. Nimezungumzia Uvamizi An Sio Vita. Nyerere Aliyaingiza Majeshi Yetu Uganda Na Wla Hakumfukuza Idi Amini Mpakani Tu Ila Alihakikisha Anmng'oa Kabisa Atawale Rafiki Yake Obote. Hivi Hamkumbuki Alivyowachezea Akina Lukle Na Binaisa Kama Watoto Wadogo Amri Zikitoka Msasani?

Hebu Wee Tuache Tu .... Ukimpenda Mtu Madhambi Yake Huyaoni!!
unakumbuka Akina Kadego,macgee Na Wengine Walipo Kimbilia Nairobi, Nyerere Ali -trade Na Moi Maisha Ya Akina Ochuku Wale Makamanda Toka Jeshi La Anga Kenya ,nyerere Akawapa Akina Ochuku Na Moi Akampa Akina Macgee Jamaa Walipo Fika Tu Kenya Mzee Nyao Akawauwa Jamaa
 
Back
Top Bottom