Tunamshukuru Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa kwa kuongelea ‘malengo’ ya ubinafsishaji wa bandari za Tanzania

Tumia akili, Bashugwa ni waziri ulitegemea aseme kinyume na maamuzi ya baraza la mawaziri ambayo mwekiti wake ni Rais? Tutumie akili sazingine.
Yaani badala ya kutekeleza majukumu yako ya ualimu huko Manyara,unahorojoka JF asubuhi asubuhi.
Kwa walimu kama wewe,elimu yetu kuwa hivi na kuwa na wajinga wengi waliopoteza muda kwenye vyumba viitwavyo madarasa ni halali.
 
Bandari, Licha ya kushughulika na upakiaji na upakuaji mizigo, bandari ni mpaka na lango kuu la nchi, hivyo bandari haipaswi kubinafsishwa kwa wageni.
Mapungufu ya utendaji pale bandarini ni matokeo ya ufisadi unaofanywa na kikundi cha watu wachache wanaofikiri wana akili zaidi ya wengine wanaofuata sheria. Bandari inaweza kuboreshwa kwa kufanya ubinafsishaji wa ndani kupitia soko letu la hisa.
Ifanyike tathmini ya mali za bandari, ina mashine ngapi za kupakulia mizigo? Mahitaji ya mashine yabainishwe na kama kuna mapungufu mashine zinunuliwe...Sio lazima tuikumbatie DPW hasa tukiwa taifa huru kwa miaka 60.
Nashauri, TPA ihamishiwe wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, iundwe kampuni ya Suma-TPA iorodheshwe kwenye soko letu la DSE ili mtaji utoke ndani ya nchi, kama itatulazimu kutafuta mwekezaji iwe ni baadhi ya gati, moja au mbili. Suma-TPA kama kampuni tanzu ya Jeshi iwezeshwe kununua winchi za kutosha. Kama tunanunua vifaru hatuwezi kushindwa kununua mitambo ya bandarini.
 
Bashungwa hana mawazo binafsi, yeye anafafanua maamuzi ya serikali inyaoongozwa na rais labda km una interest binafsi na Bashungwa

Tunachofanya hapa ni kazi ya "kuwaongoza viongozi" kwa njia ya hoja sanifu.

Ukweli kwamba Bashungwa yumo katika Baraza la Mawairi ni fursa muhimu kwa ajili ya kufanikisha lengo hili

Hatuna shida na siri za Baraza la Mawaziri
 

Sheria yetu ya ubinafsishaji inataja "Airports, Aviation, Shipping, Navigation" kama eneo mojawapo la ubinafsishaji.
 
Sheria yetu ya ubinafsishaji inataja "aviation" (bandari) kama eneo mojawapo la ubinafsishaji.
Sheria zinaweza kubadilishwa Kama zinahatarisha usalama nchi. Anga, bandari, mawasiliano, nishati, usafirishaji ni maeneo yanayopaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa. Ni maeneo tunayopaswa kuyahudumia wenyewe.
 
Bashungwa mdomo wake umeoimda, uko tenge hasa akiwa anaongea propaganda

Nashauri tujitofautishe na kina Mary Chatanda wasioheshimu tofauti kati ya valid and sound reasoning dhidi ya fallacious reasoning.

Tujadili hoja bila kumkwarua mleta hoja, tupokee ujumbe hata kama tunamkataa mjumbe
 
Unasoma vichwa vya habari tu



Halafu unabweka Kama mbwa mwenye kichaa. Stupid
Ndicho nilichokiona! Niliposoma kichwa Cha habari kidogo ni-gnore content lakini baada ya kusoma content Mama Amon ana hoja nzito inayohitaji majibu mazito! Nani wa kuyajibu? Wakati kwenye mfumo wamejaa vilaza wanaongalia matumbo yao Leo na sio future ya kizazi Cha Leo na kesho?
 
Nakuelewaga sana mama Amon.

JE umeupitia MKATABA WA DP world na SELIKALI ya Tanzania????

Unaweza ukaweka madhaifu yake pia.

NB. HAKUNA MTU ANAYEKATAA UWEKEZAJI/UBINAFSISHAJI, SHIDA NI HUO MKATABA.
Ukisoma bandiko la mama Amon ameainisha maeneo kama matatu yenye ukakasi. Tujitahidi kusoma kabla ya kujibu. Nadhani hata viongozi waliyosaini hiyo IGA hawakasoma na kutafakuri Kwa kina tena Kwa kutumia experts
 
Hata hii ilikuwa na malengo mazuri, hivyo hatutakiwi kuangalia upande huo Tu, Bali WA kisheria na matokeo yake.

Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260​

1 of 4Next Last
Jump to newWatch
•••

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member​

Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.
 
Kwa kuwa miradi yote ya bandari inatekelezwa ndani ya mipaka ya Tanzania hakuna sababu ya IGA.
Huo ndiyo ukweli ambao wanapaswa kuujua. Matatizo ya ufanisi wa bandari ya DSM hayaihusu serikali ya kifalme ya Dubai. They are not problems of mutual interest between the two governments as per definition of IGA.

Sababu inayotolewa na Hamza Johari, aliyekuwa mwenyekiti wa Negotiation Committee, ya kwamba DP World wamejenga bandari kavu huko Rwanda na DRC haina mashiko yo yote. Hizo bandari kavu alizojenga huko si mali yake, ni mali ya serikali za Rwanda na DRC. Yeye alikuwa ni mjenzi tu. Wenye kuamua watumie bandari ipi kupitisha mizigo yao ni serikali za Rwanda na DR Congo. Hivyo kama ni kuingia mkataba wa IGA, tunapaswa kuingia IGAs na nchi za Rwanda na DRC kwani ndizo nchi tulizo na mutual interest ya matatizo ya bandari ya DSM. Pia nchi ya Uganda. Huyu DP World sana sana tungeliweza kumpa kazi ya ujenzi wa bandari kavu la kisasa huko Mwanza kwa mizigo ya Uganda. Tungeweza kuwashawishi Uganda wampe kazi ya kujenga bandari kavu ya aina hiyo pale Port Bell ili mizigo yao ikishafika Dar Port iweze kusafirishwa haraka kwa SGR na meli yetu ya HKT (Hapa Kazi Tu) hadi Port Bell ndani ya saa kumi!
 
Kumradhi nilighadhibika nisamehe mwanangu. Nilikuwa na mambo mengi. Hivyo, sikujipa muda wa kusoma na kutafakari kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…