Tunamtaka Joh Makini wa 'Hao', huyu wa ni-come ndugu zake njooni mumchukue

Tunamtaka Joh Makini wa 'Hao', huyu wa ni-come ndugu zake njooni mumchukue

Mimi ni mmoja wa mashabiki wa msanii Joh makini tangu anatoka akitengenezwa kuja kuchuana na msanii mwenye kipaji kuliko wote bongo (Chid benz).

Mwamba wa kaskazini alitikisa anga la mziki na kila mkwaju alioachia ulikuwa wa Moto ndio maana alipojiita Tz Jay z sikumbishia sana.

Nakumbuka ngoma zake kama Mfalme,Hao,muda,sijutii,Stimu zimelipiwa,Show za Joh,Kilimanjaro n.k, collabo alizopiga akangaa kama utaipenda ya Hussein machozi na nyinginezo.

Huyu Joh makini wa Weusi simuelewi kabisa yaan amepwaya katika uandishi kuliko zaman, hatumuoni kama Hip hop icon wa kaskazini yaani anakoelekea haeleweki kabisa.

Chondechonde tunamhitaj Joh Makini wa Hao, huyu wa madaraka,Nicome ndugu zake njooni mumchukue.
Ubongo wako mdogo ,unataka Joh akomae tuuu asiangalie masilai akuridhishe wewe,basi na wewe imba hip pop ya kaskazini tukuone.
 
kiukweli wanazingua hizo nyimbo zao sijui naliamsha dude, ni-come na zingine zenye falsafa kama hizo ni upuuzi na upumbavu tu wamekubali kuwa watumwa wa soko mwishowe wataanza kuwaimbia machoko. Much respect na Saluti nyingi kwa Chindo Man, Yuzzo, Kala Jerimiah, Nash Mc, Bonta Maarifa
Hao uliowataja huwa unawasapoti lakini mkuu, kuingia show zao na kununua kazi zao original?
 
Upepo umebadilika zile hardcore hiphop sasa zinaonekana "haziuzi" tena in the sense kwamba wale wanaobakia na hardcore hiphop ni wale walio na misingi yao "economic resilience"cheki watu kama Watengwa recs. wao wamebakia na hardcoreHiphop kutokana na mahaba yao sasa kwa sababu ya "njaa" hardcore hiphop inatupwa kando japo ni mziki wenye kutoa uhalisi wa maisha ya "watu wetu" nafikiri ndio chanzo cha Joh na wengine wengi kufanya hihop laini.
Umemaliza.
 
Aliekuambia hiphop ni mziki wa sokoni uupange kama mafungu ya nyanya na vitunguu nani?hiphop ni Dini na imani na mtu anaeamua kufanya mziki huu lazima ajikane nafsi yake ndio afanye mziki huu.Wanaoliangalia soko kama ndio fullforce lazima waangukie pua maana soko halitaki kuambiwa ukweli soko linataka fantasia na uwongo uwongo mwingi mahaba laini na kulegeza misimamo hayo ndio yaliyoko sokoni.
Mkuu kwa hiyo ili ufanye HIP HOP lazima uwe na kazi nyingine ya kufanya? Sasa hao wanaHip Hop tunaosikia wanauza copies za kutosha wanakosea?
 
oouh labda kweli maana siwezi jua lakini mafanikio hayajifichi.

Namfahamu john vizuri saana achana na JOh wa kwenye kideo kama utapajua 360 utanielewa na mtaa wa jaluo walipohamia. Asante.
Hahaha...kweli unamjua Joh vizuri aisee.

Umeutaja huo mtaa nikakumbuka kitu.
 
Et naliamsha dude [emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44]
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] haswaaa!
Binafsi nimemfahamu Joh kunako 2005/6 alipotoa wimbo wa Chochote Popote na Wameinama wameinuka. Kiukweli kuna tofauti kubwa kwa nyimbo zile na hizi za sasa anazosema "Kakaniomba Iphone nikakanulia apple. Kakatafuna kisha nikakatafuna". [emoji57] [emoji57] [emoji57]
Hahahahaha.....ila we jamaa umenichekesha sana hapo kwenye mistari ya mwisho hapo [emoji115]
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] haswaaa!
Binafsi nimemfahamu Joh kunako 2005/6 alipotoa wimbo wa Chochote Popote na Wameinama wameinuka. Kiukweli kuna tofauti kubwa kwa nyimbo zile na hizi za sasa anazosema "Kakaniomba Iphone nikakanulia apple. Kakatafuna kisha nikakatafuna". [emoji57] [emoji57] [emoji57]
" kakaniomba Iphone nikakanunulia Apple " maana yake ni nini?
 
Mkuu kwa hiyo ili ufanye HIP HOP lazima uwe na kazi nyingine ya kufanya? Sasa hao wanaHip Hop tunaosikia wanauza copies za kutosha wanakosea?
Hawakosei wako sawa lakini Mauzo sio primary task ya Hipohop na Kwenye misingi yake Mauzo sio moja ya msingi ni matokeo tu kama mauzo yana maana sana mbona "bible" imeuzwa sana?
 
Huyo Nick sijui huwa anaimba nini.... Sio msanii kabisa
"Oloshoroo Ngararumu, ugali maakande...Takwenya, Shimbonii, kamwene urewedi....." Ni ujamaa kama Azimio la Arusha...!!!
 
Msanii gani wa hip-hop anasuka anapaka lipstick na wanja anatoga maskio
 
Daaah Jo makini wa hao , ufalme nilikua namuelewa saana ila huyu wa sasa bureee kabisa
 
Back
Top Bottom