Tunamuomba Mungu atukinge na Corona, kesho watalii wanatua KIA, AKIA, JNIA huku nchi ikiwa wazi mipakani

Hapa hakuna kumzuia mtu kisa corona, hujasikia kuna mechi ya mamelody, na warabu wanakuja kucheza hapa?waarabu wameogopa virusi vipya vya south!!wameomba mechi ichezwe TZ?Na wamekubaliwa?!!hapa hata kupima ni geresha tu,
NgojA tupige hela zao
 
Kama uliandikiwa na kupangiwa utapata Corona hata ufanyejee

Bora mkono unakwenda kinywani na unaqunyer ni jambo jema na la kumshukuru Mungu.
Kwani mkono kwenda kinywani haujaandikiwa ?

Kwanini usilale tu chakula kiingie by diffusion after all (usipokula) umeandikiwa ila kama umeandikiwa utakula (hata usile) si utakula tu ?
Au?
 
Kwani mkono kwenda kinywani haujaandikiwa ?

Kwanini usilale tu chakula kiingie by diffusion after all (usipokula) umeandikiwa ila kama umeandikiwa utakula (hata usile) si utakula tu ?
Au?
Mna vituko nyinyiπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
tusiigeuze corona Kama wimbo wa taifa.Tanzania tuna mengi ya kufanya.ilikuja ,itaondoka.hakuna Jambo lisilokuwa na e dot(.)
Nzige wameingia na tayari wananchi wameanza kulia huko Longido, nini kifanyike?
 
Corona ipo kila mahali, hata Tz ipo, wakija au wasije, hawaongezi wala kupunguza chochote katika idadi ya wagonjwa, walete mapesa hayo.
 
Corona ipo kila mahali, hata Tz ipo, wakija au wasije, hawaongezi wala kupunguza chochote katika idadi ya wagonjwa, walete mapesa hayo.
Nikupe mfano Francis, kuna mafuriko eneo mnaloishi, jirani zako wamekaa juu ya paa kusubiri msaada, wewe umekomaa ndani unasikia sauti ikitaka utoke nje kuepuka madhara unajibu "mvua ipo tu hata isiponyesha muda ukifika itanyesha"

Hao wanaokuja huko kwao wameweka tahadhari kubwa sana na lengo ni kujaribu kupunguza vifo na madhara kwa raia wao au wao hawajui huu ugonjwa upo na utaendelea kuwepo?
 
Wakifanya kama tunavyofanya sisi chanjo watamuuzia nani? Au hujui hii ni biashara unasaidia kuwatangazia watu?
 
Wakifanya kama tunavyofanya sisi chanjo watamuuzia nani? Au hujui hii ni biashara unasaidia kuwatangazia watu?
So leo unataka kutunisha misuli kwa mabeberu kuwa huwezi kununua chanjo zao kisa created virus, siyo?.

πŸ‘‰πŸΎ UNA HUO UWEZO KWELI?
 
Huwa siamini kauli eti ukipangiwa kufa kwa corona eti ni Mungu kapanga ufe kwa corona, hii sio kweli,Mungu ninayemfahamu Mimi in Mungu mwaminifu hanaa hila wala husuda,jina lake jingine ni
Jehovah.

Tuliletwa humu Duniani tumtukuze yeye hasa kwa uumbaji wake,ila kwenye suala la kufa katupa allowance ya kuishi miaka 70/na bonus juu .
 
Picnic Arusha

aiseeeh .....Mkuu salutimingisasa...
 
Oh watalii sio mabeberu
 
Wewe peke ako ndo umeongea la maana.

Watu wanajisahau kuwa kila kifo hakiji bure bali ni kwa mpango wa Mungu.

Na ikumbukwe kwamba kuna malaika maalumu wa idara ya kutoa roho,.

Roho haitoki yenyewe yenyewe tu.
Sasa kwanini watu wengi wanaoenda india kutibiwa na hospital za juu wanapona magonjwa fulani ambayo bongo yanaonekana kushindikana na mtu anaeza poteza uhai asipopata msaada wa haraka?
 
Sasa kwanini watu wengi wanaoenda india kutibiwa na hospital za juu wanapona magonjwa fulani ambayo bongo yanaonekana kushindikana na mtu anaeza poteza uhai asipopata msaada wa haraka?
Iliandikwa,.

Ukiona mtu kaenda india na kapona basi ujue iliandikwa apone.

Kwani waindi hawafi?
 
Iliandikwa,.

Ukiona mtu kaenda india na kapona basi ujue iliandikwa apone.

Kwani waindi hawafi?
Ko unaamini ccorona ni pigo la kiimani wakati Syansi nd imetengeneza? Usilinganishe mapigo ya nyoka kwenye bible na haya ya kidunia. Ukifuatilia historia ya dunia ukiacha dini utagundua kulkuwa kuna maisha mengine yanaendelea. Mtu amchome kisu mwenzie uanze kumsingizia Mungu utani huo jamani. Yani Mungu akataze kuua then ampangie mtu aje kuuawa kweli?
 
Kuna mengi hatuyatambui kwenye huu ulimwengu,.

#mwenda pole hajikwai,
#Chelewa chelewa utakuta mwana si wako,.

#Haraka haraka haina baraka,
#Ngoja ngoja yaumiza matumbo.

Utajiuliza mwenyewe hapo kwanini wazee kama wanajichanganya hivi:-

Ila ukweli ni utabaki ni dunia haina tafsiri.
 
Nilicho fundishwa IMANI BILA MATENDO NI SAWA SAWA NA BURE. Nyie salini wanao funga wafunge wanao lia walie vizuri tu kama huto muomba Mungu huku mna onyesha ushirikiano wa kujikinga ni BURE. Mna kuja kulia lia watu wanakufa ooh watu wanaumwa oooh hospitali zimejaa pita vituo vya daladala sasa watu hawana mda na barakoa, hamna anaye nawa, hamna anaye kaa mbali na mwingine.
Sasa kama nyie wenyewe hamtaki jisaidia MUNGU mna mtaka afanye miujiza gani? Jibu wote mta angamia kwa kukosa maarifa. You need Help, Help yourself first.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…