Tunaoamini hakuna kinachoshindikana tuna jambo la kuongea

chiziwafursa

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2024
Posts
558
Reaction score
827
Natamani kufuga sangara ila vifaranga vya sangara sijui nitawapatia wapi? yeyote wakunieleza nakaribisha kwa moyo wote.

Na kama hakuna anae uza kwanini mtu asianze utafiti na kuzalisha vifaranga vya vya sangara atuuzie sisi wafugaji?
 
Wafugaji wapo na vifaranga wanapatikana ila utayari wako na pesa yako iwe mfuko wa shati na uwe na elimu kabla ya yoyote usije kulizwa.

Kitu Chochote kabla hujafanya tafuta maarifa walau kidogo ya kuanza nayo mambo yasiharibike
 
Egypt wanafuga sangara kwenye mabwawa harafu nilisikia tetesi eti wanauzwa zambia ,kuhusu elimu nilisoma sana research mbalimbali ni kagoogle wapi majibu hakuna .Nikaona isiwe tabu ngoja niingie jf labda angalau naweza pata a certain information walu nipate pakuanzia upya
 
I

I mean vifaranga vya samaki
 
Fuga KAMBALE ndugu, bado wana soko sana.
Mwezi November hadi December ingia KIGOMA na BUKOBA nunua kumbikumbi wa 1-2M hata ungekuwa na kambale laki tano watatosha kwa chakula hadi kuvuna. Kuhusu soko nadhani kila mtu anaweza kukusaidia jibu.
 
I

I mean vifaranga vya samaki
Mm Nina jamaa yangu anafuga kama unataka nikuunganiahe nae anafuga Kwa hiyo ñipe no zako au nimuulize kama ana hiyo elimu nikupe no na jinsi ya kupata ikiwa tayri utafanya utakacho
Egypt wanafuga sangara kwenye mabwawa harafu nilisikia tetesi eti wanauzwa zambia ,kuhusu elimu nilisoma sana research mbalimbali ni kagoogle wapi majibu hakuna .Nikaona isiwe tabu ngoja niingie jf labda angalau naweza pata a certain information walu nipate pakuanzia upya
Yeye ana Fuga samaki Kwa hiyo mtaongea vizuri wenyewe Mimi sio mtaalam kbisa wa ishu za samaki mm kilimo n ufundi wa umeme wa magari
 
Fuga KAMBALE ndugu, bado wana soko sana.
Mwezi November hadi December ingia KIGOMA na BUKOBA nunua kumbikumbi wa 1-2M hata ungekuwa na kambale laki tano watatosha kwa chakula hadi kuvuna. Kuhusu soko nadhani kila mtu anaweza kukusaidia jibu.
Mie interest yangu ni kufuga sangara nishajiapiza kabla sijafa niwe nishafuga sangara kabisa niwe expert wakuwa shauri ninyi muanze na kufuga maana hakuna mtanzania aliye thubutu sija msikia labda mdau umekwisha msikia unijuze
 
Sangara wanataka conditions ambazo ni ngumu sana kuweza kuzifanikisha ndugu yangu. Kama hujui sangara wote waliopandwa ziwa Tanganyika hawakuzaliana hadi leo.
NB nimesema conditions zake ni ngumu sijasema haziwezekani. Fanya kaka nasi tutaku join huko mbeleni
 
Sangara wanataka conditions ambazo ni ngumu sana kuweka kuzifanikisha ndugu yangu. Kama hujui sangara wote waliopandwa ziwa Tanganyika hawakuzaliana hadi leo.
NB nimesema conditions zake ni ngumu sijasema haziwezekani. Fanya kaka nasi tutaku join huko mbeleni
Nimesoma sana kuhusu Sangara ,yeye kwake muhimu ni hewa na joto la wastani ,sasa vingine kama stress,nk-- vina fanana na samaki wengine raha ya huyu samaki unaweza usimlishe kama kumfugia kwenye cage na pia huyu anakula samaki wenzie(ana take advantage ya aina ya samaki aliopo katika mazingira yake)
 
Na
Mie interest yangu ni kufuga sangara nishajiapiza kabla sijafa niwe nishafuga sangara kabisa niwe expert wakuwa shauri ninyi muanze na kufuga maana hakuna mtanzania aliye thubutu sija msikia labda mdau umekwisha msikia unijuze
Napenda hiyo passion yako mana ndio niliyo nayo mm kwenye kilimo na niliwahi kuwa nayo kwenye ufugaji kuku ila mambo yaliniendea vibaya kwenye kuku n stori fupi ila naweza Shea nawe upate somo kidogo.
Mwaka 2021 nilinunua kloira vifaranga wa mwezi kama 20 nilichukua wale wa mwezi mana mtaji niliomba Kwa wazee Kwa hiyo nilikuwa na kama laki tatu ila sikuwekeza yote nilinunua kifaranga wa mwezi mmoja na masiku ili waweze kutoboa mpka ukubwani hyo kifaranga mmoja anauzwa elfu 4 mm nilichukua kama 20+.kufika kule napo enda kufuga hapakuwa na umeme Wala vile vyungu vya joto ila walikuwa vizuri tu mana madirisha niliziba ili jua likipiga wapate joto la jua tu na sababu ni vifaranga wa mwezi wasinge kufa kama vifaranga wa siku wale wa tsh 1700 Kwa kimoja walienda enda changamoto zilianza mashine nilizo tegemea kupata pumba zikawa hazina pumba na mm mpka kufika eneo la kupata pumba n mbali lazima utumie nauli kwenda na kurudi na hakuna gari Kwa wakati huo ni bajaji tu na bajaji nauli n buku 😂😂nilipambana hivyo hivyo Kwa capital yangu kidogo wale kuku walikuwa japo magonjwa nayo yakanitembelea hasa mafua nikapambana kigumugumu mpka nafika miezi mitatu wako nilio wapoteza ila mpka mwezi wa Tano kuku walikuwa n wakubwa ila nje ya changamoto ya pumba mashineni chakula Chao maalum ule mwaka kikapanda na pumba zikawa bei juu ila nilikomaa mpaka kuku wale wakaanza kutaga n chotara hao.nikapata mayai kadhaa na mengine nilikuwa ila changamoto ilahamia kwenye ishu ya kulea vifaranga nilio watototolesha na mazingira nayo ishu hakuna umeme hapo nikapoteza vifaranga nilio watotolesha ila nilijifunza vingi katika ufugaji chotara.

Nimekuelewa tujifunze ww una passion ila hakikisha una maaarifa na taarifa sahihi pia uwe na akiba ya kuendesha mradi mradi wowote sio mtaji tu pia iwepo Hela ya ziada ya mambo yakienda vibaya una jazilizia yanasonga.

Nimependa msukumo wako usipoteze hiyo passion yako.fanya tu hata ukifeli ndio kujifunza kwenyew
 
Yaani hapa akitokea mtu kusema niache ndoto yangu sitomuelewa kabisa baba yangu na mama yangu walisema sitofanikiwa I want to prove to them they were wrong
 
Hpana usianze kitu ili kumliziaha mtu utapata stress sana mambo yakienda kombo fanya Kwa uwezo wako tu ulio jaaliwa ila ukitaka kufanya waone utakapo pitia changamoto za uwekezaji wako utapata over stress itakugalimu hata kuumwa n.k
 
No sio kwamba nafanya kwa ajili ya mtu napenda tu kufanya utafiti ambao bado hujafanya so nikaona hivi ni bora zaidi
 
Una uhakika na soko au unafugia kama chakula tu Cha nyumbani mana hata mm Nina watu wamelima dodoma wamekosa soko kufuga kwako hatua moja hatua ya mwisho soko lako unalijua sio Kwa kuambiwa nikwa kufika na kuona na kujifunza mwenyewe achana kabisa na maneno soko lipo hayo maneno yasikie ila hayana uhalisia kabisa ukisha kuwa na mzigo mwingi.

Passion ya kufuga unayo ila soko la ufugaji wako kuuzia samaki unalo.
 
Ndio nilikuwa nataka nianze kutafiti sasa ila kwa mawazo yangu target 🎯 yangu ni viwanda vya mwanza ambako hata baba yangu huwa anapeleka Sangara huko
 
Hongera kama ni hivyo una mzazi anae peleka eneo hilo vizuri pa kuanzia unapo aisee Kwa hiyo ni vizuri ukatafuta data zilizo Shiba ila kama una uhakika mzee wako atakupa ushirikano asilimia mia wew Fuga mana tayari una connection kupitia baba.ila Kwa ushauri wangu nenda na wew huko huko upate kudadisi labda wnanunu samaki wenye ubora gani na mengineyo uliyo nayo kichwani mwako Yale maswali ya muhimu na uwe na soko mbadala nje ya soko hilo la baba yako ikitokea limeleta hali ya sintofahamu usikwame kuuza mzigo so vizuri uwe na network kubwa na Pana ya masoko ili huku kukikwama unapeleka huku ni ushauri tu mkuu japo sio lazima ufanye nionalo mm
 
Kama soko lipo na unataarifa sahihi za soko Anza kupambana na vitendo sasa
 
Hongera kama ni hivyo una mzazi anae peleka eneo hilo vizuri pa kuanzia unapo aisee Kwa hiyo ni vizuri ukatafuta data zilizo Shiba ila kama una uhakika mzee wako atakupa ushirikano asilimia mia wew Fuga mana tayari una connection kupitia baba.ila Kwa ushauri wangu nenda na wew huko huko upate kudadisi labda wnanunu samaki wenye ubora gani na mengineyo uliyo nayo kichwani mwako Yale maswali ya muhimu na uwe na soko mbadala nje ya soko hilo la baba yako ikitokea limeleta hali ya sintofahamu usikwame kuuza mzigo so vizuri uwe na network kubwa na Pana ya masoko ili huku kukikwama unapeleka huku ni ushauri tu mkuu japo sio lazima ufanye nionalo mm
Tatizo baba kasha acha kupeleka huko maana alizinguiziwa kipindi cha Magu na kupelekwa jela biashara yake ikayumba kabisa ikarudi chini Mitumbwi yake yote zaidi ya hamsini zote zikaishia Rubondo bana
 
Nisha anza walu na kupata wapi pakuanzia ila kiukweli mimi kama mimi siwezi kabisa kukamilisha
Sawa huwezi Kwa nn na umesema awali una utayari n mengineyo mengi so what Tena wew kama ww huwezi kukamikisha mbona unapingana n maelezo yako ya awali
 
Back
Top Bottom