Tunaoendesha 'Baby Walkers' specifically za 660cc tupenae uzoefu wa hizi gari

Tunaoendesha 'Baby Walkers' specifically za 660cc tupenae uzoefu wa hizi gari

ProBook

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2012
Posts
559
Reaction score
264
Wakuu Habari

Personally nimenunua babywalker Daihatsu Terios Kid cc 660 na hivi ndivyo nlivyoviaona mpaka sasa;

Gari:
kwanza lina turbo(bila
Intercooler), max speed 140kph, tank capacity ni 40lts, sio 4WD, gari lipo juu nakatiza nalo popote bila shida

Ulaji wa Mafuta ,
ukiwa mjini na jam + AC ni 9.5km/l,(speed 40kph)
highway + AC ni 13.5km/l na (speed 120kph)
highway bila AC ni 16km/l (speed 120kph)

Comfortability:
Naona lipo comfortable sanah maana hata kwenye kona naweza kata kwa speed yoyote bila shida

Spacing:
Halina buti kubwa kabisah unaweza hifadhi vitu vichache

Spea:
Spea zake zapatikana na bei zake ni reasonable

Matatizo:
Mpaka sasa sijaona tatizo lolote

Nakaribisha wadau tushare uzoefu, especially kwa safari ndefu je vinaweza kuhimili safari nyingi!?
 
1. Hujui kuendesha kwa hiyo gari ulipaswa kwenda kwa 20km/l1 ya mafuta.

2. Hiyo siyo gari. Baada ya muda itaanza kuchemsha labda ibaki ya kufuatia nyanya sokoni. Gari za kukusaidia angalaua anxa na cc1290.

3. Hongera kumiliki magurudumu manne.
 
Hata mimi nimeshangaa yaa cc660 bado inaenda k 16 per ltr kweli hajui endesha au imetoboka tank
 
Wakuu Habari

Personally nimenunua babywalker Daihatsu Terios Kid cc 660 na hivi ndivyo nlivyoviaona mpaka sasa;

Gari:
kwanza lina turbo(bila
Intercooler),
Kwa ninavyofahamu, turbocharger zote zinakuwa na intercooler. Kwani haina lile tundu kwenye bonnet?
 
Ukiwa unataka kusema uongo jaribu basi hata kuwa na details kamili ambazo zitafanania na ukweli......

Sasa wewe kagari kama Terrios Kid.....cc 660 kanamalizaje lita moja kwa kutembea km 13.5?!

Kwa hizo cc 660 kama ulikuwa haufahamu, hiyo gari ingeweza tembea hadi km 26+/litre na sio km 13.

Sasa wewe unatunga vitu halafu unakuja kutuambiaje hapa.....!
 
Mi nyuzi za hivi hua sitoki napata uzoefu ili siku nikipata pesa nifanye uchaguzi vizuri. Hilo gari mkononi shilingi ngapi?
Mwenyekiti unaanzaje kufikiria vibaby walker wakati 8Mil-9Mil unapata Brevis matata tu!.. Au unadanganyika na keyless ignition system!?.🙂
 
Mwenyekiti unaanzaje kufikiria vibaby walker wakati 8Mil-9Mil unapata Brevis matata tu!.. Au unadanganyika na keyless ignition system!?.🙂
Quality Assurance hizo CC na running cost zinanidanganya
 
Back
Top Bottom