Tunaoendesha 'Baby Walkers' specifically za 660cc tupenae uzoefu wa hizi gari

Tunaoendesha 'Baby Walkers' specifically za 660cc tupenae uzoefu wa hizi gari

Kigari gani hicho ambacho hupeleki hata car wash! ukitaka kuosha unampa dada wa kazi anakimix na vyombo anakiosha then anakitia kwenye beseni.
Acha madharau mbweha kabisa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huwa najaribu tu kuwaza kama ndio unamiliki Baby walker halafu umekwenda kwenye tafrija ambayo kila mtu pale ana magari yenye label kubwa kubwa ,unaweza kujikuta umeipaki mtaa wa pili ukaingia mwenyewe on foot...
Hata makampuni ya lebo kubwa wana vi-baby walker lakini
 
Hakuna kitu napenda kama Jimny Land Venture...niko najichanga kama ni 15M au 20 lakini ntaipaki uwani Mungu akijaalia
 
Mimi ninayo Suzuki jimny 658cc huwa natumia 12km/l
Mkuu unaweza kutupatia feedback zaidi kuhusu Suzuki jimny 658cc. Nina plan ya kuinunua ningependa kujua mazuri na mabaya yake.
Upatikanaji wa spare na mengineyo
 
View attachment 886816

Mimi baby walker wangu ni wa dizaini hii... Hizi gari kwa huko Japan zinaitwa KEI cars... Yani gari zote zenye engine chini ya 650cc ziko categorized as KEI car. Hii ilikuwa ni kuwasaidia watu wa kipato cha chini ambao wanaweza kumudu kutumia piki piki waweze kutumia gari.

Kuhusu Pajero Mini, this is a super car on its class. Huwa nina uwezo wa kusimama toka spidi sitini hadi 0 ndani ya sekunde chace tu na kwa umbali usiozidi mita mbili.
Kuhusu kiwese, hizi Jeep hazikuundwa kuwa fuel efficient. Japo ni cc 650 lakini Vitz ina ulaji mdogo wa mafuta kuliko hii gari.
Kwa jinsi kalivyo stable, huwa sikati kona, nalala nako kwenye kona. Huwa sipunguzi mwendo kwenye matuta naruka nako hivyo hivyo. Ukiniona niko kwenye hii gari, kaa mbali na mimi. Nitakupita kama unyoya.
This is one of the best cars to have kwa njia zetu hizi.
kuna hyo ya milango mi5 sasa daah ukiiona kwq mbele kama range vile
 
Back
Top Bottom