Kafara ni sadaka ya kufidia kosa. Katika Agano la Kale watu walileta wanyama kama mbuzi au kondoo kuwa kafara ya dhambi zao. Lakini hiyo kafara ilikuwa ya muda tu, na kila mara walirudia tena kwa sababu haingeweza kufuta dhambi kabisa.
Ndiyo maana Yesu alikuja na akatolewa kama Kafara ya mwisho na kamili. Yeye hakuwa na dhambi, lakini alibeba adhabu ya makosa yetu. Kwa hiyo, wokovu hauji kwa kushika sheria au kuhesabu matendo mema, bali kwa kukubali kafara ya Yesu Kristo msalabani.
Sheria inaweza kukuonyesha kosa lako, lakini haina uwezo wa kukusamehe. Imani kwa Yesu pekee ndiyo inakuunganisha na ile kafara yake, ambayo ndiyo msingi wa msamaha na wokovu. Ndiyo maana tunasema: Tunaokolewa kwa imani, si kwa sheria. Kwa sababu kafara tayari imetolewa jukumu letu sasa ni kutubu na kumwamini Yeye.
Kafara ni neno la
Kiarabu (
Kafirr) au (
Kafiri) linalomaanisha
Faini au
Fidia
Ushasikiasikia kuna watu wanawaita wenzao
Makafiri yaan
Makafara sasa hicho ndicho wanachomaanisha yaan hawa ni kuwatoa
Kafara hawa ni kuwapigia
Faini hawa ni wa kuwapigia
Fidia.
Ukiugua Ugonjwa (hapa inabidi utulie ili unielewe) Mungu amekupa Mwili uutumie kwa Kumuabudu yeye pekee na usiutumie mwili kwa mengine yasiyo ya Mungu, tuelewane hapo, tusiende kwenye sheria ya Imani kwanza, sasa ukiufanya Mwili tofauti na Maelekezo ya Mungu Mungu anakupiga na Ugonjwa (rejea Agano la Kale Musa na Farao), akishakupiga na Ugonjwa unachotakiwa kufanya ili Upone ni kulipa
Fidia au kulipa
Faini ili Ugonjwa Uondoke ili Upone unatakiwa utoe
Kafara (rejea tena Agano la Kale Musa na Farao yaan Firauni), ushaelewa?
Sasa tukirudi kwenye Kafara hapo ukipigwa na Gonjwa km la Zinaa kwa mfano Gonorrhea, mwili unaanza kua tofauti, ili upone inabidi ulipe Fidia ulipe Faini ulipe Gharama ya Dhambi zako utoe ulizozifanya utoe
Kafara ili Mungu akusikie na akusamehe na unaapa hautorudia tena kufanya tena hio Dhambi mbele za Mungu maana ulishapata fundisho, na ili Upone inakubidi ulipie matibabu ya Ugonjwa wako (
Fedha ya Matibabu inatoka katika mfano wa
Fidia au
Faini au
Kafara sio Njiwa, sio Mbuzi, sio Kondoo, sio Ng'ombe, sio Ngamia ni Fedha km Fedha) Fedha inatoka wapi? Kauze Njiwa, kauze Ng'ombe, Kauze kondoo, kajitumikishe uwe Mtumwa wa watu (Mtumishi) ili wewe uweze kupona na kutakasika na Mungu anakuokoa baada ya hapo unatubu na hutaki tena kutenda ile Dhambi iliyomkasirisha Mungu. Kwa hio Fedha za Matibabu unazolipa hospitali ili Upone ni sawa na Kafara maana unalipa Fidia au Faini kwa Mungu wako kwa Ugonjwa wako unaoutesa Mwili wako ili Upone.
Ukiona umelipa Fidia umelipa Faini umetoa Kafara Umelipia Fedha za Matibabu na haujapona maana yake Kafara yako imegoma imekataliwa bado Mungu amechukizwa tena na Kafara yako hajaipenda kwa hio basi utaendelea Kuteseka tu mpaka pale utakapomtolea Mungu Kafara atakayoikubari na kukusamehe na kukuponya na kukuondolea kile kinachokusumbua, sawa km ilivyokataliwa Kafara aliyoitoa Kaini.
Unaweza ukatoa Kafara ikakubariwa na Mungu ukiwa unashangilia baraka za Mwenyezi watu wakaona km Mungu amepokea Kafara yako ya Mbuzi ila yeye mwingine amempa Mungu matikiti na machenza na mabibo na mbogamboga, Mungu akachukua Mbuzi akakataa yule alimpa Matunda na mbogamboga, mwenye mbogamboga na matunda akasema km Mungu hataki mbogamboga na matunda anataka nyama basi ngoja nimtoe huyu ambae Kafara lake la Mbuzi limekubariwa (Yesu Msalabani), Abeli ukimtizamia km Yesu wa Agano la Kale maana alipendwa na Mungu na akauawa kwa sababu ya Dhambi za Nduguye Kaini Dhambi ya Mauaji cha kustaajabu pamoja na yote hayo Mungu wa Agano la Kale alimsamehe Kaini kwa kumuua Abeli akawaambia watu wasimuue Kaini pamoja na kwamba amemuua Nduguye Abeli Mungu hakulipa kisasi, Abeli akauawa na Nduguye Kaini huku Kaini akiwa na lengo la kumtoa Abeli kwa Mungu km
Kafara, makanisa ya siku hizi yanaita
Sadaka wengine wanasilibia wanaita
Sadaka ya Kuteketeza na Kujimaliza yote ikimaanisha
Kafara.