Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
- Thread starter
-
- #21
Hapo unapo amua kubadilika lazima kuna lifestyle unabadirisha lazima kuna utaratibu unabadirisha
mfano
ulihukumiwa ukiwa unauwa, sasa umeamua kubadilisha life style ukawa au uwi watu unakuwa tayari unashika sheria au utaratibu flani
Kazi kweli kweli, kwahiyo umekuja kutuambia tuzikatae mari zinazo sema usiuwe, uszini ambazo hazina ubaya wowote, unapozishika amri hizo unakuwa sio mzinzi unakuwa sio muuwaji sasa unakuwa mtakatifu usio na dhambi ndipo unatakiwa umfuate yesu achana na mafundisho ambayo yanapingana na maandiko.Ni kweli Yesu alisema mkinipenda mtazishika amri zangu. Sasa unavyojiuliza ‘I don’t know how to love,’ fahamu kwamba kumpenda Yesu si jambo la hisia pekee, bali ni kumwamini na kumkubali katika maisha yako. Upendo kwa Yesu unamaanisha imani ya kweli kwake, na imani hiyo ndiyo inayozaa nguvu ya kuacha dhambi zile zilizo katwazwa na sheria.
Unaposema moyoni unampenda Yesu kwa sababu ni Mkombozi wako, hiyo ni hatua nzuri sana. Lakini shida ni kwamba unajikuta bado unasumbuliwa na uasherati. Hapa ujue huendi kinyume na maneno ya Yesu, bali unaonyesha kwamba bado unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu. Kwa sababu kwa nguvu zako binafsi huwezi kuacha, lakini ukimruhusu Yesu akuongoze, anakupa nguvu ya kushinda.
Mfano mdogo: mtoto mdogo anapompenda mzazi wake, si lazima akazunguke kila siku akisema ‘nakupenda.’ Badala yake, upendo wake unaonekana kwa vitendo kusikiliza na kufanya anachoambiwa. Lakini mtoto huyo hawezi kufanikiwa peke yake, mzazi wake humsaidia, humwelekeza na hata kumsamehe anapokosea. Ndivyo ilivyo kwa Yesu: upendo wetu kwake siyo maneno tu, bali ni imani inayojitokeza katika matendo mapya na matendo hayo hutokea kwa msaada wake.
Kwa hiyo, usiogope wala kujiita hujui kumpenda. Ukimpenda Yesu kwa moyo wa dhati, amri zake unajikuta unazifuata kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Hata hilo tatizo la uasherati, kadri unavyomkaribia Yesu, ndivyo unavyozidi kupata nguvu ya kuachana nalo. Sio mara moja, bali hatua kwa hatua. Upendo wa kweli kwa Yesu unabadilisha tabia yako, hadi unajikuta unaacha yale uliyoshindwa kuyaacha kwa nguvu zako.
Unabii unasema pia watakao okolewa ni wale wazishikao amri za mungu basi ndivyo itakavyokuwa sasa kama unaendelea kujizima data na kutaka kubadilisha maandiko yawe vile unavyotaka wewe na kuweka yako unakuwa unakosea, maandiko yameweka wazi ukimpenda mungu utazishika amri zakeUpo sawa, unapoamua kubadilika lazima kuna lifestyle unabadili, kuna utaratibu mpya unaanza kuishi. Lakini tofauti ya maisha ya sheria na maisha ya imani ni hii; Sheria inakulazimisha usifanye jambo fulani kwa nguvu zako, huku ukiishi kwa woga wa adhabu. Lakini imani inakupa nguvu ya ndani ya moyo, unabadilika si kwa shuruti, bali kwa hiari kwa sababu upo ndani ya Yesu.
Ukipewa mfano wa muuaji aliyebadilika, sheria itamwambia: ‘Usiue tena, ukikiuka utakufa.’ Hiyo ni kulazimishwa. Lakini imani inamjenga mtu ndani ya moyo mpya. Anaacha kuua sio tu kwa sababu anaogopa adhabu, bali kwa sababu upendo wa Kristo ndani yake umemgeuza. Anaanza kuona thamani ya maisha ya binadamu na kuishi kwa upendo. Hapo ndiyo tofauti.
Kwa hiyo kubadilika kunaonekana kwa lifestyle mpya, lakini lifestyle ya imani haianzi nje, inaanzia ndani. Ukimpenda Yesu kweli, lifestyle yako inabadilika bila kulazimishwa na sheria, bali kwa nguvu ya upendo ulio ndani yako. Ndiyo maana Yesu alisema, Mkinipenda mtazishika amri zangu. Kwa sababu upendo huo unazaa utiifu wa hiari, si wa lazima.
Alitolewa KAFARA unajua nini maana ya Kafara?Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.
Kazi kweli kweli, kwahiyo umekuja kutuambia tuzikatae mari zinazo sema usiuwe, uszini ambazo hazina ubaya wowote, unapozishika amri hizo unakuwa sio mzinzi unakuwa sio muuwaji sasa unakuwa mtakatifu usio na dhambi ndipo unatakiwa umfuate yesu achana na mafundisho ambayo yanapingana na maandiko.
Kama maandiko yamesema ukinipenda utazishika amri zangu basi fanya hivyo kuzishika amri zake kwani amri zake sii nzito yesu amesema, shetani anajua siku ukizishika utakuwa umemfuata yesu ipaswavyo ndio maana anakudanganya na hao wachungaji wako mbumbumbu.
Lakini kama maandiko hayasemi usizishike pia unaweza kufanya hivyo sawa
Unabii unasema pia watakao okolewa ni wale wazishikao amri za mungu basi ndivyo itakavyokuwa sasa kama unaendelea kujizima data na kutaka kubadilisha maandiko yawe vile unavyotaka wewe na kuweka yako unakuwa unakosea, maandiko yameweka wazi ukimpenda mungu utazishika amri zake
amriz za mungu sii nzito yesu amesema mwenyewe wala hakubani chochote amri hizo ndio tabia ya waishio mbinguni jenge utaratibu wa kuzifuata ufanane na malaika watiifu wa mungu
unapozishika unakuwa mtiifu usipo zishika unakuwa muasi
Alitolewa KAFARA unajua nini maana ya Kafara?
Naona unatafuta kichaka cha kuzikataa bado ngoja nikupe fungu hiliNi kweli maandiko yanasema Mkinipenda mtazishika amri zangu. Lakini kumbuka kuna tofauti kubwa kati ya kushika amri kwa nguvu zako mwenyewe na kushika amri kwa msaada wa imani ndani ya Kristo. Sheria inasema usizini, usiue, usiibe, na hizo zote ni kweli na ni njema. Hakuna anayekataa kuwa kuyashika ni sahihi. Tatizo ni hili: mwanadamu kwa asili yake ameshindwa kuzishika kikamilifu kwa nguvu zake mwenyewe. Hata Biblia inasema aliyeanguka kwenye kosa moja amevunja yote. Yaani, hata kama huui na hufanyi uasherati, ukisema uongo mmoja tu tayari umevunja sheria yote. Hapo ndipo tatizo la sheria linapoonekana; inataka ukamilifu wa asilimia mia moja, kitu ambacho binadamu hana uwezo wa kukitimiza.
Ndiyo maana Yesu alikuja. Siyo kufuta sheria, bali kuitimiza. Alikuja kuonyesha kwamba sasa msamaha na wokovu havitokani tena na mtu kushika sheria kwa nguvu zake mwenyewe, bali kwa imani kwake. Na mtu akimwamini Yesu kwa dhati, amri zake anazishika kwa hiari, kwa sababu upendo wa Kristo ndani yake unamgeuza. Hapo ndipo tunaposema tunaokolewa kwa imani, si kwa sheria, si kwa sababu amri si nzuri, bali kwa sababu imani ndiyo inatupa nguvu ya kweli ya kuishi hizo amri.”
Kwa ufupi, hakuna anayekataa amri za Mungu. Tofauti ni hii: Sheria pekee haiwezi kukufanya mtakatifu, bali imani kwa Yesu inakuweka huru kisha Roho Mtakatifu anakusaidia kushika amri hizo bila kulazimishwa. Ndiyo maana Yesu alisema, nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Kwa hiyo nimekuja kuwaambia watu wote watambue kwamba ili waokolewe na kusamehewa dhambi zao, hawana budi kutubu na kumwamini Yesu Kristo, yaani kumpenda kwa dhati. Wokovu haupatikani kwa kuishi kwa kufuata sheria au kwa kujitahidi tu kutenda mema ilhali bado hawajamwamini Yesu Kristo. Kwa njia hiyo hawawezi kusamehewa makosa yao ya nyuma. Msamaha wa kweli na wokovu kamili unapatikana kwa imani ndani ya Kristo pekee.
“Mkinipenda, mtazishika amri zangu.”
“Kwa maana kumpenda Mungu ndiko huku, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.”
2 Wafalme 5Ukipewa mfano wa muuaji aliyebadilika, sheria itamwambia: ‘Usiue tena, ukikiuka utakufa.’ Hiyo ni kulazimishwa. Lakini imani inamjenga mtu ndani ya moyo mpya. Anaacha kuua sio tu kwa sababu anaogopa adhabu, bali kwa sababu upendo wa Kristo ndani yake umemgeuza. Anaanza kuona thamani ya maisha ya binadamu na kuishi kwa upendo. Hapo ndiyo tofauti.
Wewe bado sana endelea kujifunza maandiko sio unajifunza kiduchu alafu unakuja hapa kupotosha watuNaona unatafuta kichaka cha kuzikataa bado ngoja nikupe fungu hili
Yesu mwenyewe kuhusu kushika amri zake
📖 Yohana 14:15
2. Mtume Yohana akifafanua kwamba amri si nzito
📖 1 Yohana 5:3
Hivyo kifungu cha kwanza (Yohana 14:15) ni maneno ya Yesu, na cha pili (1 Yohana 5:3) ni ufafanuzi wa Yohana kuhusu amri za Mungu.
naona unahitaji darasa zaidi kuhusu amri za mungu na kuhiana na utii wa sheria na maagizo.
Mbinguni kuna malaika wanaopokea maagizo kama sisi tulivyopewa maagizo ya sheria na wanatii na kutekeleza amri au sheria ndio tabia ya mbinguni usipo zifuata hustahili kuingia mbinguni kwasababu utakuwa sio mtiifu utakuwa mtu wa kulalamika sijui mungu anatubebesha mizigo ya kufanya hivyo huwendi mbinguni
Hii ndio inaweza kuwa sababu ya shetani kumuasi mungu alikuwa anakiburi kwa kweli kitoshika amri za aliye mkuu ni kibuti
Ibrahim aliambiwa ametoe mwanae wa pekee kafara alikubali vipi wewe unae zikataa amri za mungu kuwa ni mizigo ungelubari kumchinja mwanao
Lazima uone maluelue,maanake ni jambo linalopingana na akili ya mwanadamu,mambo ya kufikirika,kinyume na maumbile ya mwanadamu!Ni neema kubwa sana kuelewa hili somo, Wakristo kwenye hili wanaona malue lue
this knowledge will lift up your spiritual lank from one level to another
Kafara ni neno la Kiarabu (Kafirr) au (Kafiri) linalomaanisha Faini au FidiaKafara ni sadaka ya kufidia kosa. Katika Agano la Kale watu walileta wanyama kama mbuzi au kondoo kuwa kafara ya dhambi zao. Lakini hiyo kafara ilikuwa ya muda tu, na kila mara walirudia tena kwa sababu haingeweza kufuta dhambi kabisa.
Ndiyo maana Yesu alikuja na akatolewa kama Kafara ya mwisho na kamili. Yeye hakuwa na dhambi, lakini alibeba adhabu ya makosa yetu. Kwa hiyo, wokovu hauji kwa kushika sheria au kuhesabu matendo mema, bali kwa kukubali kafara ya Yesu Kristo msalabani.
Sheria inaweza kukuonyesha kosa lako, lakini haina uwezo wa kukusamehe. Imani kwa Yesu pekee ndiyo inakuunganisha na ile kafara yake, ambayo ndiyo msingi wa msamaha na wokovu. Ndiyo maana tunasema: Tunaokolewa kwa imani, si kwa sheria. Kwa sababu kafara tayari imetolewa jukumu letu sasa ni kutubu na kumwamini Yeye.
Wangapi wanampenda Yesu na dhambi hiyo hawaiachi? Tena wanaifanya ndani ya madhabahu?Mpende Yesu awe rafiki yako hiyo dhambi utaacha
Hekaya za kufikirika!
Ukiona dini ina maneno ya kusadikika yanayosigana na akili na maumbile ya binadamu ujue hiyo ni dini ya uongo.
Wangapi wanampenda Yesu na dhambi hiyo hawaiachi? Tena wanaifanya ndani ya madhabahu?
Mbinguni ni mwendo wa utii tu na mari kutoka kwa mungu unaposikia shetani alimuasi mungu unaelewaje kwanza ? unaposikia shetani alikuwa mkaidi na kiburi unaelewaje ?Kile kinachozidi akili si lazima kiwe uongo. Mara nyingi ndicho kinachothibitisha mipaka ya mwanadamu na kutufundisha kwamba kuna nguvu kubwa kuliko sisi. Imani ya kweli inajulikana kwa matunda yake na msingi wake katika historia, si kwa kuitwa hekaya za kufikirika.
Sasa tumalizeHii inamaanisha kumpenda Yesu si maneno ya mdomoni pekee. Kama mtu anaendelea kuishi ndani ya dhambi bila majuto wala kupambana nayo, basi ule “upendo” wake ni maneno, si upendo wa kweli.
Pia kuna tofauti kati ya mtu anayejikuta akianguka kwa udhaifu, lakini ndani yake anajuta na kupambana kuacha, na mtu anayekaa kwa makusudi kwenye dhambi huku akijidai “anamfuata Yesu.” Wa kwanza bado ana nafasi kubwa ya msaada wa neema ya Kristo; wa pili yupo kwenye hali ya hatari, maana amezoea dhambi.
Kama tungeokolewa kwa matendo yetu, hakuna anayeweza kusimama. Lakini kupitia imani kwa Yesu, mtu anapata msamaha na nguvu ya kushinda tamaa ya dhambi. Hata wale wanaodai wanampenda Yesu lakini bado wako ndani ya dhambi suluhisho lao si kujificha kwenye dini, bali ni kutubu kweli na kuruhusu Yesu abadilishe maisha yao.
Kwa hiyo, wako wengi wanaosema wanampenda Yesu lakini bado wako utumwani mwa dhambi, hata kwenye madhabahu. Hii inaonyesha upendo wao bado ni wa maneno tu. Upendo wa kweli kwa Yesu huonekana pale mtu anapopokea neema yake, kutubu, na kujikuta akiacha dhambi kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Sasa tumalize
endelea kujifunza biblia uelewa wako ni mdogo sana ba hao walimu uliokuwa nao ni waongo
tumalize kwa kusema nakushauri muamini yesu na pamoja na kuzishika amri zake kwa pamoja tangu umesema kuwa amri zake sio mbaya zinakatza mambo mabaya na machafu zishike utaokolewa mara moja kama vile ndoto yako ilivyo.
Hata kwenye Mathematics wengi wanaona malue lue, lakini aimaanishi ni formula za uwongo.Lazima uone maluelue,maanake ni jambo linalopingana na akili ya mwanadamu,mambo ya kufikirika,kinyume na maumbile ya mwanadamu!