Tunaomba Dunia iongeze nguvu kuwasaidia Watanzania kupambana dhidi ya dhuluma ya Haki za msingi za binadamu

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Suala ya udhulumaji haki kwa wananchi wa Tanzania linalofanywa na watawala, lina uhalali na haki ya kupata msaada mkubwa kutoka jumuia ya kimataifa.

Ni mwendawazimu pekee ndiye anaweza kutamka kuwa eti udhulumaji wa haki, ikiwa ni pamoja na utekaji na mauaji ya wakosoaji, ni suala la ndani ya Tanzania, na halitakiwi kuingiliwa na watu, taasisi au mataifa ya nje.

Tamko la Umoja wa Mataifa, ambalo linafuatia falsafa ya Martin Luther King Junior, ni kuwa ukiukaji wowote wa haki za mwanadamu mahali popote Duniani ni ukiukaji wa haki dhidi ya Ulimwengu mzima:
"Injustice anywhere is a threat to justice everywhere"

Tamko hili linamaanisha kuwa dhuluma dhidi ya haki sehemu moja ya Dunia, inadhoofisha msingi wa haki kwa Ulimwengu mzima.

This statement emphasizes that when one group is denied justice, it weakens the foundation of justice for all.

Hivyo, ni muhimu wananchi wote wa Tanzania, kila mmoja kwa namna yake awezayo, tuunganishe nguvu kupambana na wote wanaodhulumu haki zetu. Viongozi hawakuchaguliwa ili wawaangamize wananchi kwa kuwateka, kuwatia ulemavu na kuwaua, au kuwaua ndugu zetu, majirani zetu na watanzania wenzetu kwa umma. Kodi zetu zinatakiwa zitumike kutulinda, siyo zitumike kuwateka watu, kuwaua au kuwatupa maporini.
WATANZANIA TUTAMKE, "DHULUMA NA UHARAMIA DHIDI YA MTANZANIA MMOJA NI DHULUMA DHIDI YA WATANZANIA WOTE.

ANAYEMDHULUMU MTANZANIA MMOJA NI ADUI WA WATANZANIA WOTE.

Kauli hii itaendana na ile iliyoridhiwa na Umoja wa mataifa kuwa, dhuluma ya mahali popote ni dhuluma dhidi ya Ulimwengu mzima, inamaanisha kuwa madhira anayofanyiwa mtu mmoja, directly or indirectly yanaugusa Ulimwengu wote.

"Idividuals are interconnected and that what affects one person affects everyone, indirectly."

Ni wito wa Umoja wa mataifa, kwa watu wote, taasisi zote, jamii zote, na mataifa yote Duniani, kuchukua hatua za kuzuia au kuondoa udhulumaji wa haki mahali popote Duniani, bila ya kujali mipaka ya nchi.

Wakenya waliokuja kufuatilia masuala ya udhulumaji wa haki nchini mwetu, Bunge la Ulaya lililokemea udhulumaji wa haki nchini Tanzania, taasisi mbalimbali kama Amnesty International, Human Rights Watch, vyama mbalimbali vya wanasheria Duniani na nchini, taasisi za Dini, na watu binafsi waliochukua hatua mbalimbali kukemea udhulumaji wa haki nchini Tanzania, wanastahili pongezi kubwa kwa kutekeleza tamko la Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala la haki za binadamu.

Kwa upande mwingine, ni aibu kubwa na laana kwa Taifa letu, kuona kuna watu wanathubutu kutamka kuwa eti jumuia ya kimataifa haistahili kuingilia masuala ya udhulumaji wa haki za binadamu unaofanyika nchini, na kwamba ni masuala ya ndani ya nchi na Tanzania ni Taifa huru. Hawa watu ni watu wa ajabu. Yaani Serikali yako iteke watu, iwatese watu, iue watu, halafu eti ni mambo ya ndani! Watu wa namna hii wanatakiwa wapelekwe shule wakafundishwe ili wajue kuwa ulinzi wa haki za binadamu hauna mpaka, na tamko la Umoja wa mataifa linahimiza mataifa ya nje kuzisaidia jamii zinazodhulumiwa hata nje ya mataifa yao kwa sababu mara nyingi wanaodhulumiwa, hasa wanaodhulumiwa na dola, wakati mwingine, huwa wamemalizwa nguvu na uwezi, kiasi cha kushindwa hata kujitetea.

KWA MH. RAIS MSTAAFU KIKWETE.
Wananchi tunamshangaa sana Rais wetu mstaafu Jakaya Kikwete, ndiye Rais mstaafu pekee anayeishi, anaweza kuwa na muda wa kuzunguka Dunia nzima kumtafutia kura Janabi, lakini hana muda wa kukemea udhulumaji wa haki unaotokea nchini. Tulitarajia, hata kabla jamii ya kimataifa kuinuka, mstaafu huyu angekuwa wa kwanza kuukemea huu uovu unaoendelea, kwani tuna uhakika wa 100%, anaujua.

Mwalimu Nyerere akiwa hai, polisi walipoanza kurusha mabomu ya machozi dhidi ya watu waliokuwa wakilisukuma gari la Mrema, alijitokeza na kukemea kwa nguvu zote. Tena kwa maneno yake alisema, "ninyi mnaumizwa na nini kama kuna watu wamejitolea kwa nguvu zao kulisukuma hilo gari. Waacheni, hata wakitaka kumbeba waacheni. Labda kuna watu wanapenda kubebwa kama maiti wakati wana uwezo wa kutembea". Baada ya pale ule upuuzi wa kupigapiga watu mabomu ya machozi, ukakoma. Hata sasa, kama Rais Kikwete, yalipoanza haya matukio ya kishetani ya kutesa, kuteka na kuua wanaomkosoa Rais, angetoa kauli kali ya kukemea, kama alivyofabya Mwalimu Nyerere wakati wa utawala wa Mwinyi, nchi isingefika hapa tulipo, na kauli yake tu ingekuwa imeokoa uhai wa wengi waliouawa.
Watanzania tuungane dhidi ya wanaodhulumu haki za binadamu. Tuweke tofauti zetu za kisiasa, za dini, za kikabila, kimaeneo, pembeni; tukabiliane na udui yetu mmoja, mdhulumaji wa haki, anayewatesa Watanzania (kuwapiga, kuwatia ulemavu na kuwatupa porini), anayeteka na kuwapoteza watanzania (watanzania wengi wamepotezwa, na hatujawahi hata kuiona miili yao), na wanaowaua watanzania na kuitupa miili yao porini. Hawa ni ndugu na ni wanafamilia wa binadamu watanzania wenzetu. Fikiria wangekuwa ni ndugu, Baba, kaka au wanao.

Hakuna 'mambo yetu ya ndani', kwenye kudhulumu haki za wanadamu wenzako. Tupaze sana sauti, tupeleke ujumbe na kuomba msaada kwa mataifa yote na taasisi zote Duniani, lakini nasi tusibweteke, tusimame kuukemea uovu huu.

Mungu ambariki sana Mzee Warioba, maana ndiye mzee mstaafu pekee ameweza kusimama na kuukemea uovu huu. Tunampongeza Gwajima, Kanisa Katoliki, TLS, Shura ya Maimamu, maana hawa wote angalao wamewahi kuukemea uovu huu. Kwa sababu sauti zao zimeo
Puuzwa na watawala, tunatakiwa kuchukua hatua kali zaidi, wadhulumaji wa haki hawastahili heshima wala staha. Wanastahili kuelezwa wazi kuwa hatuukubali uovu wao, na wao, kwa matendo yao hayo, wamekuwa maadui wa Taifa letu na wananchi wote kwa ujumla, isipokuwa waovu wenzao.

Quotes za Tamko la Haki za binadamu:
"that when injustice exists, it erodes the foundations of a just society and makes it harder to achieve justice for everyone.

"Injustice in any place should be a matter of concern for all who believe in a just world."

Pongezi nyingi sana kwa wanaharakati wa Kenya, mmetimiza wajibu wenu wa msingi kama binadamu, kama wanajumuia wa EAC na kama wajumbe wa Ulimwengu mzima. Bila shaka Mungu atawabariki kwa hiki mnachokisimamia, kupigania haki za wanadamu wenzenu mahali popote Duniani.

WITO KWA RAIS SAMIA:

Rais Samia, usidanganyike na waliokuzunguka. Katika suala hili la udhulumaji haki, kwenye suala hili la utekaji watu, kuwapiga watu na kuwatupa porini, kuwaua na kuwapoteza, hakuna anayesimama na wewe. Unaweza kuhadaiwa na hao wanaokuzunguka, lakini kuna siku utajiona umebakia pekee yako. Ni aheri utoke kwa wanaokuzunguka, uongee na watu wengine wenye hekima, nje ya uwigo wako wa Serikali, ili uupate ukweli. Utekaji, ubambikiaji watu kesi, utesaji watu, kuwaua na kauli za vitisho, kamwe haviwezi kuzuia watu kupambana na dhuluma, na kiukweli, yote hayo yatazidisha mapambano dhidi ya utawala wako, wewe mwenyewe binafsi na wanaokuzunguka.
 
Watanzania hawahawa wataigeukia dunia na kusema inaingilia mambo yao
Bado tuna kasumba ya UNYANI aliousema The Late Rev. Christopher Mtikila

View: https://web.facebook.com/reel/574643281672101
 
Huyu ndiyo nani naona amepostiwa huko

1748239995832.png
 
Watu wa nje hawatasaidia kama sisi wenyewe hatujipiganii.

Msimamo wa Lissu unahitaji kuungwa mkono na kila asiyependezwa na uhayawani huu wa wana Ccm kuwaona wasio wanachama wao kama wadudu wa kuangamizwa.
Tujitetee kwanza wa nje ndipo watakaposaidia kuwaweka mezani.
 
Huyu huyu Kikwete? Watu wa pwani wengi ni wa........ki sana!
 
Watu wa nje hawatasaidia kama sisi wenyewe hatujipiganii.

Msimamo wa Lissu unahitaji kuungwa mkono na kila asiyependezwa na uhayawani huu wa wana Ccm kuwaona wasio wanachama wao kama wadudu wa kuangamizwa.
Tujitetee kwanza wa nje ndipo watakaposaidia kuwaweka mezani.
Upo sahihi sana. Lazima sisi tuwe mstari wa mbele kupambania haki zetu, wengine ndipo watuumge mkono.
 
Back
Top Bottom