Tunaomba majibu ya kuturidhisha Kimantiki ya kwanini Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kukosa kuhudhuria Sherehe za Muungano?

Tunaomba majibu ya kuturidhisha Kimantiki ya kwanini Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kukosa kuhudhuria Sherehe za Muungano?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kutokana na Umuhimu na Unyeti wa huu Muungano wa Bara na Visiwani nimeambiwa kuwa Watu wa Itifaki katika Awamu zote zilizopita walikuwa Wakihakikisha Ratiba za Rais kamwe haziingiliani na Siku hii ya Muungano na kwamba ni lazima Mheshimiwa Rais awepo kutokana na kuwa pia ni Moja ya Tunu ya Nchi ( Taifa )

Watetezi wake Mama ( Team Kutetea Kila Kitu ) nawaomba hakikisheni mkija Kulifafanua hili mje na Hoja za maana zenye Mantiki ( Logic ) kabisa juu ya Jambo hili ambalo hata Watu wengi wa Itifaki na Wazalendo wa Taifa limewashtua / limetushtua mno.

Wengine wanadai Muungano umetukanwa kutokana na hili lakini wengine wanadai taratibu Tunu za Taifa zinaanza Kupuuzwa huku wengine pia wakidai huenda limefanyika Kusudi ili Kuchochea zaidi Mzozo wa chini chini kuwa kuna Watu wanataka Wawe peke yao kwa Kujidanganya kuwa Wanajiweza wakisahau kuwa hata Umeme wao tu umetokea katika Nguzo za Tegeta Azania, zikazama Baharini na kuwafikia Kwao.
 
Inaonekana hiyo safari ya kwenda mambele alikwenda bila kujuwa anarejea lini na amekuwa mtu wa kuambiwa nini cha kufanya, yupo tu anasikiliza na kuambiwa.
 
Hamna jinsi, hiki kitu muungano umebaki jina tu na kutumia fedha kushereheka.

Mpaka head of state hajahudhulia hata kutuma salaam (sijaona mahali) basi kuna tatizo sehemu flani.

Umuhimu wa hivi vitu ni pale tu viongozi wanapoamua kufanya mabadiriko ya kimuundo in deeper.
 
Huyu kwa maoni yangu anaambiwa nini afanye na wapi, akae marekani mda gani na bila kuhoji yeye anakaa tu huko. Its a very long time for a president of a sovereign state kukaa nje ya nchi yake, unless kwa ugonjwa.

Kwa hali hii aliowaacha wataacha kuitafuna nchi kweli, I mean if the president herself doesn't care, who will?

Badae ndio mnasikia mambo yalipitishwa kimyakimya bila kujulikana who did what!
 
Back
Top Bottom