Tunaomba mnapojenga Chato tukumbukeni na siye huku Rungwe Mashariki. Barabara tunateseka sana wakati wa mvua

Tunaomba mnapojenga Chato tukumbukeni na siye huku Rungwe Mashariki. Barabara tunateseka sana wakati wa mvua

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Naweza sema hizi Barabara hasa hii inayoanzia Katumba - Mwakaleli- Rwangwa- hadi Kyela ni muhimu sana kiuchumi.

Huko ndiko inatolewa gesi ya carbon dioxide hiyo inayotumika kwenye vinywaji, mafridge nk.

Huko kuna mashamba makubwa ya chai na kiwanda cha chai. Hivyo utaona umuhimu wa eneo hilo kiuchumi.

Huko kuna mashamba makubwa ya zao la ndizi. Sehemu kubwa ya ndizi zinazoliwa Iringa, Dodoma , DSM zinatoka huko. Tatizo wakati wa mvua za masika ndizi zaozea mashambani maana gari hazifiki huko.

Rungwe Mashariki pia kuna ufugaji makubwa wa ng'ombe wa maziwa. Hata hivyo maziwa mengi yanayozalishwa huko yanakosa thamani na kuuzwa mbei ya chini kwani kuyasafirisha kwenda mjini Tukuyu it is expensive kwa sababu ya ubovu wa miundombinu ya barabara.

Wakati wa mvua za masika hizi barabara zinapitika kwa shida sana.

Hivyo tunaomba basi mnapo ijenga Chato, tukumbukeni na siye huku japo barabara tu.
 
Naweza sema hizi Barabara hasa hii inayoanzia Katumba - Mwakaleli- Rwangwa- hadi Kyela ni muhimu sana kiuchumi...
Airport ya Songwa mshukuruni Mwandosya. Ilikuwa ijengwe tangu zamani lakini Waziri Mkuu akazipeleka Arusha Airport. Barabara za kwenu ni mbaya sawa tu na za Chato na kwa Majaliwa, ni mbaya, maeneo mengi yaliachwa nyuma.

Ajabu ni kuwa naeneo yaliyopendekewa disorder yamekuwa kiini cha wapinzani, sasa mnatumiwa nyie kugombana nyie kwa nyie.
 
Mtasubiri sana maana chato hadi iwe uraya
Sio Michato tena ni Mirere kabisa.....
Uchumi wa kati....
Nchi hii ni tajiri sana....
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu....

Nyie Mnayajua mavieitee!!!
Huku chato tunatembelea mavieitee...!!!!
 
Nimepakumbuka dah mwakaleli parachichi kama zote, hizo barabara dah utadhani njia za mifugo

Subilieni awamu ya 6 saivi wapinzani walitucheleweshea sana maendeleo ya chato
 
20210112_195909.jpg

Tukimaliza chato tunakuja wilaya jirani, nyinyi ni baada ya miaka mitano. Nalori kange..
 
Naweza sema hizi Barabara hasa hii inayoanzia Katumba - Mwakaleli- Rwangwa- hadi Kyela ni muhimu sana kiuchumi....

Tulia keki itagawanywa sawia: Tanzania ni Tajiriiiii, tuchape kazi, Lima maparachichi, ndizi huko busolokelo lipa kodi tuijenge tanzania.
 
Naweza sema hizi Barabara hasa hii inayoanzia Katumba - Mwakaleli- Rwangwa- hadi Kyela ni muhimu sana kiuchumi.

Huko ndiko inatolewa gesi ya carbon dioxide hiyo inayotumika kwenye vinywaji, mafridge nk..
Huko kwa miaka hii sidhani kama hiyo barabara itajengwa; wananchi na viongozi wao wajaribu kutumia mbinu nyingine kuweza kutengeneza hiyo barabara.

Ingawa JIWE alipotembelea huko aliahidi kuitengeneza ,lakini sioni kama mbunge muhusika wa eneo hilo ana clout ya kuinfluence fedha zipatikane za kujenga hiyo barabara!!
 
Mwandosya ame disappoint sana hio Rungwe Mashariki. Hio barabara itajengwa labda Yesu akaribie kurudi. Since 1995 naanza kujitambua watu wameipigia kelele lakin hakuna la maana
 
Back
Top Bottom