Tunaomba msaada jamani tumekwama na basi Dodoma tangu Saa 8 Usiku

Amekuambia wametelekezwa porini na dereva/konda wa basi. Sasa unamwambia atumie google map ndio italeta basi jingine au?
Imebidi nicheke tu, mtu analalamika katelekezwa then mpuuzi mmoja anamshauri atumie google map! Ili iweje?
 
pole sana,hii bsu imechakaaa mnooo
 
Dereva na konda wake inaonekana ni wahuni hawana utu kabisa,
Wameshindwa kuthamini abiria wao yaani bora lichomwe moto liteketee huko maana hawana maadili ya kuthamini utu wa watu
 
Dah poleni Sana naamini mpaka sasa mmeshaondoka tujuze,Hilo basi niliwahi kupanda linatoka Mbeya Singida Mbeya
 
Duuh poleni sana,hapo mbona Pana maduka mkuu,Mimi nipo Dodoma na gari ni Nyingi njia hiyo!
 
Poleni Mkuu.

Pamoja na ushauri wa wadau hapo Juu,

Ila siku nyingine,

Kama route yako ya One way haina Gari nzuri basi jaribu kuunga unga kwenye gari nzuri.

Mfano
Hapo Mbeya mpaka Dodoma kuna Shabiby. Jamaa wapo vizuri.

Ukifika Dodoma unapata gari za kutoka Dar Singida (Ester) au Dar Mwanza kuna gari nyingi za Maana ( Katarama, Chakaby, Ally's Star ) na nyinginezo. Unashukia Singida hapo safi kabisa bila tatizo.

Unaepusha Usumbufu usiokuwa wa lazima na kuokoa Muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…