DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mtanzania Mnyonge22

Senior Member
Joined
Sep 2, 2022
Posts
125
Reaction score
455
Habari Zenu Wakuu.

Mimi na wenzangu 11 tulikua tukifanya kazi mgahawa ambao upo Masaki, unaitwa “LE MARAHEB RESTAURANT & more” unamilikiwa na waarabu wa Yemen. Tarehe 28 January, 2022 ilitokea mzozo kazini majira ya saa 7usiku, baina ya bosi wakike na wafanyakazi huyo mama alitutukana matusi ya nguoni mbele ya wateja wachache waliokuwepo wanamalizia kuvuta shisha, na akasema hatomlipa mbwa yoyote mshahara! Popote tutapoenda kudai haki zetu atasema “hatufahamu” na ataaminiwa sababu hakuna mwenye mkataba nae pia yeye ana hela.

Hio sio mara ya kwanza huyu mama kutukana wafanyakazi wake matusi ya nguoni, alikua akitutukana mara kwa mara tena mbele ya wateja bila kujali chochote. Wateja wengine walichukizwa kwa jinsi huyu mama anavyo mistreat wafanyakazi wake hivo baadhi ya wateja wamekua wakiacha comments mbaya juu ya mistreatment za wafanyakazi huko Google Review kwa muda tofauti tofauti. Ushahidi upo.

Huo usiku wa tukio supervisor alimuomba bosi asituadhibu kwa kutunyima haki zetu za mishahara, sababu wengi wanategemea mshahara huohuo kuendesha maisha yao.

Yule mama alimtukana matusi ya nguoni supervisor na akamfukuza kazi usiku huohuo na kuamriwa atoke nje ya mgahawa. Supervisor akasema ataondoka baada kulipwa mshahara wake yule mama akasema hamlipi hata aende wapi, hana mkataba na yoyote kati yetu huku akicheka! Wafanyakazi wote usiku huo tukawa upande wa Supervisor sababu ni kweli hakuna mwenye mkataba pale na tulichoshwa kutukanwa matusi.

Yule mama akasema subirini hapahapa hamna kuondoka leo nitawaonyesha mie ni nani. Baada ya muda defender la polisi likafika na askari mmoja akatufata na kuuliza kama kuna fujo? Sababu wamepigiwa simu kuja kutuliza fujo na wameambiwa mali zimevunjwa pale mgahawani ila anashangaa kukuta hali ni shwari na hamna dalili ya kitu kuvunjwa.

Naendelea hapo chini kwenye comments👇🏽
4A41B08E-7DB2-45F8-9F09-213D40B46808.jpeg
CA3E6033-97E1-4CC7-9FBD-DC92ABE86534.jpeg
5522C38A-508C-42A4-A9AD-0F65C828EF44.jpeg
A454EA18-87AB-4CB2-BCDC-D375F4550B7F.jpeg
 
Ikabidi Wafanyakazi Tufunguke kwa Askari namna Tulivotukanwa na Kutishiwa hatulipwi Mishahara yetu, yule Askari akaamuru Bosi apigiwe simu, hivo akapigiwa simu(Bosi wa Kiume ambae ni Mume wa yule Mama) na Kwa Bahati nzuri Supervisor alifanya akili akarekodi Voice ya Mazungumzo baina ya Askari na Mwajiri Wetu.m hivo ushahidi wa Voice Tunao ambapo Yule Askari aliamuru Siku inayofata (29-January-2022) saa 2 asubuhi Bosi akutane na Wafanyakazi wote kusolve hili tatizo na Atulipe Mishahara Yetu lasivo tukishindwa Kuelewana Turipoti kituo cha Polisi ili Tuelekezwe wapi tutapata Msaada.

Ikabidi Tuwajulishe na Wenzetu ambao waliingia shift ya Mchana yaliojiri usiku huo ili wote Tukutane asubuhi.

Siku ya Pili tulifika Kazini asubuhi tukimsubiria Bosi kabla ya Muda wa kazi Kufika (Mgahawa unafunguliwa saa 6 Mchana),

Yeye na Mkewe waliwasili saa 5, Wakatuita Tuongee na sisi tukatii, Tulikua 15, Bosi wa Kiume akaomba Supervisor ajitokeze na alivojitokeza tu Gafla yule Bosi akamtukana Matusi na Kumsukuma. Sisi wote tukainuka na Kuondoka kwani tuliona Hamna Usalama.

Baada ya dakika Chache Likaja Defender likataka kumchukua Supervisor Pekee ila akajitetea ana madai yake ya Mshahara pamoja na Sisi wengine hivo Wote tukapanda kwenye Gari kasoro watu 3 walibaki waliona Sio Dalili nzuri.

Hilo ndo kosa Tuliofanya, baada kufika Polisi Tukaeleza Madai yetu ya Mishahara, yule Mama akadai sisi tuna wiki mojamoja Kazini hivo hawez kutulipa kitu ambacho ni Uongo!

Pia Ilivofika Saa 12 Jioni Mkuu wa Kituo akasema Tupo chini ya Ulinzi tusubiri Kupelekwa Lockup, na yy pamoja na Askari wake waliondoka Na Bosi zetu Wakidai wanaenda Kufanya Uchunguzi, ila ukweli ni kwamba walialikwa Mgahawani na Kupewa Dinner ya Nguvu (Wenzetu waliobaki Kazini walitutonya)

Polisi waliporejea Kituoni saa 3 Usiku tuliruhusiwa Kurudi nyumbani kwa Sharti kwamba iwe Siri kwamba Hatukulazwa Lockup hata Wenzetu waliobaki Kazini tusiwaambie Siri hii.

Hatimae wakaamriwa Watulipe Mishahara Yetu na wao wakasema Watatulipa siku ya Jumanne hapo Kituoni.
 
Siku ya Jumanne alivofika Kituoni akasema atatulipa Jioni Anamsubiri Wakili wake,

Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) akasema While tunamsubiri Wakili wa Bosi inabidi Tuchukuliwe Maelezo yetu ili ibaki kama kumbukumbu Pale Kituoni, Sisi tukakubali mara tunashangaa tunaulizwa “Kwanini ulifanya Fujo? Tukajibu Hatujafanya Fujo yyte na nyie si mmesema mlienda Kuchunguza na Pale kuna CCTV cameras zaidi ya 4 tizameni muone kama kuna Fujo iliotokea zaidi mtaona Yule Bosi wa kike alivokua anatutukana Matusi na Kusema Hatulipi Mishahara Yetu. Jioni ilivofika yule Bosi akarudi akasema Hatulipi Mishahara ila Anatupeleka Mahakamani tumemfanyia Fujo, Tukamwambia Pale Kazini kuna CCTV CAMERA ALETE CLIPS ZA FUJO, akasema CAMERA HAZIFANYI KAZI.

Basi akadanganywa Tunalazwa Mahabusu ila alivoondoka Tukaruhusiwa Kurudi Makwetu turipoti siku inayofata kwajil ya Kupelekwa Mahakamani. Siku iliofata Hawakutokea hivo na Sisi tukachoka ule Usumbufu, tulitaka Kwenda Ofisi ya OCD ila Tukazuiwa, Askari wengi walitushauri Twende CMA wakidai Tutapata Haki zetu huko nasi Tukaenda CMA kufungua Mashtaka
 
Yule Bosi alivopelekewa Summons ya CMA alishikwa Hasira akasema Hatulipi. Baada siku Kadhaa tukaitwa Polisi Osterbay Jioni, Tukaambiwa Tujiandae kupelekwa Mahakamani kwa Kosa la Kutukana Matusi ya Nguoni na sio kufanya Fujo tena! Tulishangaa matusi gani wakati Sisi ndio Tuliotukanwa Matusi, Siku iliofata Tukapelekwa Mahakamani Kusomewa Mashtaka Kwa Bahati Nzuri Askari Magereza wa Kike wa Mahakama ya Kinondoni aligoma Kubadilisha Mashtaka from kufanya Fujo to Kutukana Matusi.. mpelelezi alidai eti alikosea Kuandika badala ya Matusi akaandika Fujo, Yule Askari wa Kike alimwambia kama umekosea Ingia nao Mahakamani umueleze Hakimu mimi usinitfutie Matatizo!!!
 
Mabosi wakuda namna hii Ni wa kuwaanika tu mitandaoni...

Alaf hebu Andika jina la restaurant.
Majina ya hao maboss.
Rusha insta , Facebook, nk nk. Dunia ijue ushenzi waofanya. Hizo audio clips zirushe pia magroup ya WhatsApp.

Yaaan wafanyien ukuda pro max

Na mishahara alikuwa anaingizaje? Kwa bank au mkononi?. Kwan hamna ushahid wowote kuwa alishawah kuwalipa huko nyuma?. Ili ndio iwe udhibitisho kuwa amewaajiri muda kidogo na sio wiki?.

JF kuna mawakili , watetez wa haki za binadamu nk nk kwahiyo bila shaka utapata msaada uliouomba.

Aaagh!
 
NAWASHAURI JIACHAGUENI VIONGOZ 3 NENDENI MKAFUNGUE KESI KITUO CHA POLISI, WAKUBALI AU WAKATAE KUFUNGUA KESI, NENDENI PIA KWA RPC MKAMPE TAARIFA YA SHIDA YENU...
Yakishindikana yote haya kama police wataamua kukaa upande wa hao ngurue wa kigeni... Chomeni moto huo mgahawa au wekeni hata sumu wateja waharishe tu bila kufa...
USIKUBALI kuonewa ktk ardhi ya nyumban kwako...
 
Umetaja vituo vyote umeshindwa weka picha na jina la mgahawa. Ukute mimi pia ni mmoja niliokosa mshahara, tukashirikiana kutafuta suluhu yetu
Naogopa Nisije pata Matatizo, Mkinihakikishia sitopata Tatizo Nitapost hapa Mgahawa, Comments za Wateja Google kuhusu Mistreatment zao kwa Wafanyakazi, Instagram pia waliwahi kupata Comments mbaya juu ya Kunyanyasa Wafanyakazi ila wanafuta. Pia wakija kua Exposed kwenye Media mashahidi wengi sana Tutajitokeza ambao tulifanya kazi kwao na Kudhulumiwa haki zetu
 
NAWASHAURI JIACHAGUENI VIONGOZ 3 NENDENI MKAFUNGUE KESI KITUO CHA POLISI, WAKUBALI AU WAKATAE KUFUNGUA KESI, NENDENI PIA KWA RPC MKAMPE TAARIFA YA SHIDA YENU...
Yakishindikana yote haya kama police wataamua kukaa upande wa hao ngurue wa kigeni... Chomeni moto huo mgahawa au wekeni hata sumu wateja waharishe tu bila kufa...
USIKUBALI kuonewa ktk ardhi ya nyumban kwako...
Asante kwa Ushauri wako Mkuu, ila Kuchoma Moto Mhh mtihani huo, Nitafatilia khs RPC.
 
Inaendelea👇🏽

Tulisomewa Shitaka la Kufanya Fujo na Kufukuza Wateja eneo la Biashara Majira ya asubuhi

Wote 12 Tulikana Kosa kwamba sio kweli!! Wavulana (6) na Waschana (6),
Kesi ikasogezwa mbele wiki 2/3

Hakimu: Washtakiwa wote 12 wamekana Kosa, Je una Mashahidi?

Bosi: Ndio

Hakimu: utakua na Mashahidi wangapi?

Bosi: Mashahidi wapo wengi sana

Hakimu: Utakua na Mashahidi wangapi??

Bosi: watatu, wanne, Tano hivi,

Hakimu: Utakua ba Mashahidi wangapi??

Bosi: watano (5)

Baada ya Hapo sisi Tukarudishwa Lockup ya Mahakama tukisubiri Ndugu zetu watudhamini, Bosi wa Kike akaja Lockup akatucheka sana na Kuapa Watahakikisha Tunafungwa Japo mwezi mmoja mmoja, hatuwezi kushindana na Hela. Wote 12 ilikua ndio kesi ya Kwanza maishani mwetu tena ya Kusingiziwa! Hatuna Uzoefu wowote Woga ulitushika, Hakika tulikumbuka ule msemo “Wanaokwenda Jela sio wote wana Hatia” wengine wana Watoto wadogo Majumbani wengine Wanauguza Wazee wao Majumbani tunafkiria itakuaje Hatma yetu na Familia zetu.

Baada ya Hapo yule Bosi hakutokea Mahakamani Mara mbili (2). Tulivoitwa kwa mara ya Tatu (3) tukiamini Kesi inafutwa Alitokea Mahakamani siku hio na Mashahidi wawili (Mmoja Mlinzi, mwengine Hatumtambui)
 
Back
Top Bottom