DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Inaendelea👇🏽

Yule Shahidi wa Pili Tulifkiri ni Mteja tu wa Mahakamani, ila Mmoja wetu alikaa Benchi moja nao na akamsikia akimuuliza Mlinzi “Una uhakika bosi wako atatulipa Vizuri au tumekuja Kujichoresha tu hapa Mahakamani?

Mlinzi akampa Ishara ya Kunyamaza kwakua Yule Shahidi Hatujui ila Mlinzi ndie anaetujua.

Yule Bosi na Mashahidi wake wakatoa Ushahidi wao wa Uongo kwamba Sisi Tulivamia tu Mgahawa asubuhi na Kuanza Kuzuia Wateja wasiingie Mgahawani, Mlinzi akadai tulikua Tunapiga Mpaka Bodi Za Magari ya Wateja, na wote walimtupia Lawama Supervisor kwamba ndie aliturubuni Tusiingie Kazini Tufanye Fujo, pia Tukio liliotokea Usiku Baina ya Mkewe na Wafanyakazi Walijifanya Hawalitambui na Muda wa Kuuliza Maswali Bosi alikataa kwamba Hakuna Polisi aliewasiliana nae na Kumuamuru tukutane asubuhi,

Nashkuru Mungu kwa Kujiamini Mmoja wetu akatoa simu na Kumwambia Mheshimiwa Hakimu tuna Ushahidi wa Voice baina ya Askari na Bosi wetu, Yule Bosi alitahayari akakiri kweli aliambiwa Tuonane asubuhi.

Mmoja wetu nae kwa Kujiamini aliomba Mahakama Itume Wataalam wakachunguze CCTV CAMERA WAJIONEE TUKIO LILIOTOKEA USIKU HUO, yule Bosi akajibu Camera Mbovu, na Mheshimiwa Hakimu akatueleza kwamba “Mahakama ya Mwanzo haichukui Ushahidi wa Kielectronic”.

Mmoja wetu aliuliza Mgahawa Unafunguliwa saa ngapi? Bosi akajibu saa 4 asubuhi, akamuuliza tena, mbona kwenye Matangazo na Ratiba mitandaoni imeandikwa Mgahawa unafunguliwa saa 6 mchana? Bosi akajibu “Tumeandika tu hivo”
 
Naogopa Nisije pata Matatizo, Mkinihakikishia sitopata Tatizo Nitapost hapa Mgahawa, Comments za Wateja Google kuhusu Mistreatment zao kwa Wafanyakazi, Instagram pia waliwahi kupata Comments mbaya juu ya Kunyanyasa Wafanyakazi ila wanafuta. Pia wakija kua Exposed kwenye Media mashahidi wengi sana Tutajitokeza ambao tulifanya kazi kwao na Kudhulumiwa haki zetu
Oya jomba ugĂ li wako ushamwagwa wewe unaogopa nini kumwaga mboga?
 
NAWASHAURI JIACHAGUENI VIONGOZ 3 NENDENI MKAFUNGUE KESI KITUO CHA POLISI, WAKUBALI AU WAKATAE KUFUNGUA KESI, NENDENI PIA KWA RPC MKAMPE TAARIFA YA SHIDA YENU...
Yakishindikana yote haya kama police wataamua kukaa upande wa hao ngurue wa kigeni... Chomeni moto huo mgahawa au wekeni hata sumu wateja waharishe tu bila kufa...
USIKUBALI kuonewa ktk ardhi ya nyumban kwako...
Ni sahihi. Yaani mtu atoke alipotoka aje kuninyanyasa nchini kwangu. Nilichotakaga kumfanya Witzer Solomons wa Enza Zaden Afrika kule Arusha Mungu pekee ndio anajua. Yaani nipo kwenye ardhi ya Mama yangu Tanzania alafu [emoji200][emoji200] moja limetoka Uholanzi aje kunyanyasa. Eti leo Wachina, waarabu sijui wazungu wanakuchapa hadi fimbo kisa kazi. Si bora nikauze figo zangu kuliko kudharirishwa kwenye ardhi yetu. Mnashindwa hata kuuchoma moto huo Mgahawa alafu mnakuja kulalamika huku.
 
Inaendelea Hapa👇🏽

Hatimae Zamu yetu ya Utetezi ikafika, Mnamo mwezi wa April-2022, Tulikua tunaskiliZwa Wanne Wanne.

Mmoja wetu alileta Uthibitisho kutoka vyanzo Vinne (4) Tofauti Kuprove kwamba Mgahawa Unafunguliwa saa 6 Mchana na Mgahawa hauna Huduma ya Breakfast hivo Tumesingiziwa kwamba Tulifukuza Wateja!

Mwisho tuliulizwa kama Tuna Mashahidi? Wengine walijibu Hapana ila Mmoja alisema Tunao, akamtaja Askari Polisi alietoa Amri ya Kukutana Siku hio ya Tukio, na Mfanyakazi mwenzetu Wakike ambae yy aliendelea na Kazi baada ya hilo Tukio.

Tukapatiwa Summons ya Kumuita yule Polisi,
Tulimpata kwa Tabu sababu Hatukua na Mazoea nae, Pili yy hakufatilia tena Kesi yetu baada ya Usiku ule, Osterbay Police tuliambiwa Tumpe Summons “OCS” ila alikataa Katakata Kuichukua akasema Tumtafute wenyewe huyo Askari. na Bosi nae alikua anamuwinda (Askari Alituonyesha Ushahidi wa Simu anazopogiwa na Bosi) baada ya Kufanikiwa Kumpata na Kupokea Summons.
 
Siku ya Hukumu yule Bosi hakutokea ila sisi washtakiwa wote 12 Tulitokea, MUNGU ni Mwema Tulishinda Kesi na kuachiwa Huru!

Yule Bosi Kakata Rufaa July 23. Kesi Ikapangwa August 24 ila Kwa Bahati Mbaya hatukusikia kesi yetu Kuitwa hivo Imesogezwa mpaka September Mwishoni.

Kule CMA matumaini ya Kulipwa hela zetu hakuna wanatusumbua sana na wanaapa Hatutopata hata 100. Wanasema Kheri wahonge kuliko kutupa Sisi Haki zetu.

Na pia Wafanyakazi Wapya Pale Mgahawani baada ya Sisi kuondoka wanatishiwa kwamba kuna wenzenu hapa walijidai kwenda Kutufungulia kesi Mahakamani, Kesi imeisha na Hela zao wamekosa!! Na anasema kila Tukishinda Atakata Rufaa mpaka Tuchoke wenyewe Tusamehe hela zetu ila Yeye Hatulipi Ng’o!

Wakuu tunaomba Msaada wenu Hapa miongoni mwetu kuna watu wa Vitengo tofauti kulikua na Supervisor,Cashier,Waiter/Waitress, & Cleaners. Wengine Mpaka Leo Hatuna kazi, maisha Magumu tuna watoto, mmoja Single Mother ukiskia story yake machozi yatakutoka, huku tunasumbuliwa Mahakamani, Polisi Walitutenda Kutufungulia Jalada la Kesi wakati Ukweli wanaujua Hatuna Hatia, Watu wengi sana wamedhulumiwa na Hawa Bosi zetu kabla Yetu Sisi na wengine wamelipwa Mishahara Pungufu wakamuachia Mungu
 
Nia yake atufunge Jela, kule Kazini wanawaambia Wafanyakazi Wapya wenzenu Wapo Gerezani Tumewafunga.

Wanajiamini 100% hawatulipi hela zetu hata twende wapi, na Hofu Yetu wasije kufanikiwa Kutufunga while hatuna Hatia na Hukumu Ilithibitisha hivo. Roho zinatuuma Tulikua tunafanya kazi Mpaka saa 8 Usiku, Maana wana huduma ya Shisha ndo wateja walikua wanachelewa Kuondoka, Kweli Mtu unanyimwa Jasho lako uliolitafuta kwa tabu kurudi Nyumbani usiku wa manane Tunaogopa Kupishana na Vibaka na Mateja, anatukomesha kutunyima haki zetu kisa tu ana hela? Tuende wapi Sauti zetu zisikike? Tukifungwa Jela Wazee wetu na Watoto wetu watakua kwenye hali gani? Hawana Huruma ni Makatili mno hawana Urafiki na mtu hata huyo Mlinzi alietusaliti na Kutoa Ushahidi wa Uongo Alisimamishwa Kazi akabembeleza sana arudishwe maana Maisha yake hana hata sehem ya Kulala, sshv anajuta na muda wowote anaondoka mambo yamemgeukia.
 
Naogopa Nisije pata Matatizo, Mkinihakikishia sitopata Tatizo Nitapost hapa Mgahawa, Comments za Wateja Google kuhusu Mistreatment zao kwa Wafanyakazi, Instagram pia waliwahi kupata Comments mbaya juu ya Kunyanyasa Wafanyakazi ila wanafuta. Pia wakija kua Exposed kwenye Media mashahidi wengi sana Tutajitokeza ambao tulifanya kazi kwao na Kudhulumiwa haki zetu
Acha uoga wa kindezi. Watanzania sisi tuna uoga sana wa kijinga ndio maana tunadhulumiwa na kusagwa kama mang'ombe. Yote hayo uliyofanyiwa, na baadhi ya ushahidi unao, kwa nini tu usimwage kila kitu? Weka kila kiambatanisho, acha uoga wa kipumbavu. Mwaga hadi hiyo voice note ya mazungumzo ya polisi na bosi wa kiume kama kweli ipo. You dont have anything to lose..!! Ukikaa kimya utapoteza haki zako zote, bora upambane tu kiume. JF hii ni kubwa usiichukulie poa, ukimwaga na kuweka kila kitu hadharani pamoja na hizo google na insta reviews za wateja, ni rahisi sana uzi wako kuchukuliwa serious na u never know mtu mwenye madaraka ni rahisi zaidi ku chip in na kuwasaidia. Endelea na uoga wako wa kipumbavu ufe mkia matakoni kama mbwa koko.
 
Acha uoga wa kindezi. Watanzania sisi tuna uoga sana wa kijinga ndio maana tunadhulumiwa na kusagwa kama mang'ombe. Yote hayo uliyofanyiwa, na baadhi ya ushahidi unao, kwa nini tu usimwage kila kitu? Weka kila kiambatanisho, acha uoga wa kipumbavu. Mwaga hadi hiyo voice note ya mazungumzo ya polisi na bosi wa kiume kama kweli ipo. You dont have anything to lose..!! Ukikaa kimya utapoteza haki zako zote, bora upambane tu kiume. JF hii ni kubwaz usiichukulie poa, ukimwaga na kuweka kila kitu hadharani pamoja na hizo google na insta reviews za wateja, ni rahisi sana uzi wako kuchukuliwa serious na u never know mtu mwenye madaraka ni rahisi zaidi ku chip in na kuwasaidia. Endelea na uoga wako wa kipumbavu ufe mkia matakoni kama mbwa koko.
Si haoni mwigulu jana kaja kutetea kiwa hana magari 60 na kaalika mawaziri wake kumtetea na kutetea tozo. Kimsingi JF ni kubwa sana na hata mama anapitia humu.
 
Habari Zenu Wakuu.

Mimi na wenzangu 11 tulikua tukifanya kazi mgahawa ambao upo Masaki, unamilikiwa na waarabu wa Yemen. Tarehe 28 January, 2022 ilitokea mzozo kazini majira ya saa 7usiku, baina ya bosi wakike na wafanyakazi huyo mama alitutukana matusi ya nguoni mbele ya wateja wachache waliokuwepo wanamalizia kuvuta shisha, na akasema hatomlipa mbwa yoyote mshahara! Popote tutapoenda kudai haki zetu atasema “hatufahamu” na ataaminiwa sababu hakuna mwenye mkataba nae pia yeye ana hela.

Hio sio mara ya kwanza huyu mama kutukana wafanyakazi wake matusi ya nguoni, alikua akitutukana mara kwa mara tena mbele ya wateja bila kujali chochote. Wateja wengine walichukizwa kwa jinsi huyu mama anavyo mistreat wafanyakazi wake hivo baadhi ya wateja wamekua wakiacha comments mbaya juu ya mistreatment za wafanyakazi huko Google Review kwa muda tofauti tofauti. Ushahidi upo.

Huo usiku wa tukio supervisor alimuomba bosi asituadhibu kwa kutunyima haki zetu za mishahara, sababu wengi wanategemea mshahara huohuo kuendesha maisha yao.

Yule mama alimtukana matusi ya nguoni supervisor na akamfukuza kazi usiku huohuo na kuamriwa atoke nje ya mgahawa. Supervisor akasema ataondoka baada kulipwa mshahara wake yule mama akasema hamlipi hata aende wapi, hana mkataba na yoyote kati yetu huku akicheka! Wafanyakazi wote usiku huo tukawa upande wa Supervisor sababu ni kweli hakuna mwenye mkataba pale na tulichoshwa kutukanwa matusi.

Yule mama akasema subirini hapahapa hamna kuondoka leo nitawaonyesha mie ni nani. Baada ya muda defender la polisi likafika na askari mmoja akatufata na kuuliza kama kuna fujo? Sababu wamepigiwa simu kuja kutuliza fujo na wameambiwa mali zimevunjwa pale mgahawani ila anashangaa kukuta hali ni shwari na hamna dalili ya kitu kuvunjwa.

Naendelea hapo chini kwenye comments[emoji1427]
Nipe details jina la mgahawa na
Majina ya wamiliki.

Angalizo
Usiwe umeongeza Wal kupunguza chumvi na muwe na ushahidi wa UHAKIKA.
 
Unashindwa kusaidika sababu unawaficha wasomaji uliowakusudia hapa, upo JF una I'd fake pili wewe unasema uhalisia wenyewe alafu hutaki kutaja jina la mgahawa Yan zile key points unazificha na ogopa asije akatokea mpinzani wako yaan anaenufaika na hyo kesi akakoment kwenye magep uliiacha hapa utakuja kuonekana wewe ulikuwa muhuni tuu na unastahili hayo unayopitia.

Ukweli una njia fupi sema ndo hvyo huwa unauma DUNIA HAINA USAWA.

Unanjaa Kali anatokea Simba Nate njaa Kali umepata nafasi ya kumuua unasema eti siwezi kumuua Simba hata nikimuua siwezi kumla.

Yeye Simba anasema hapa ndio nimepata nyama wacha nipambane nimle huyu.

Au akitokea swala mbele yako wewe nasimba unafikiria Simba atakuachia upate nyama kidogo kwa swala?
 
Kuna mtu alitufanya watanzania kuwa MAZUZU, binafsi sio zuzu issue hii ndio utaelewa wazulu ni watu wa namna gani, burn burn burn hiyo restaurant yao next time hawatarudia ushenzi huo na watawahasidia wenzao kuwa watanzania sio wa kuchezewa haki zao, sasa unakimbilia huku kwenye soft touch kama mbwa koko, fight
 
Back
Top Bottom