DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mgahawa wa Kinyanyasi ā€œLE MARAHEBā€ unaendelea Kubadilisha wafanyakazi kila kukicha. Nafasi zote zipo! Hakuna mfanyakazi anaedumu
4E11247F-56CD-4FE3-AE7B-DF94951FA864.jpeg
 

Attachments

  • 651B5E5E-2409-4E53-AAB4-862E5DBB3DB5.jpeg
    651B5E5E-2409-4E53-AAB4-862E5DBB3DB5.jpeg
    147.4 KB · Views: 7
Sikuhizi Wahudumu wanadhulumiwa Tipu zao na Tip anachukua Cashier ambae ni Ndugu yao.
04E62B4E-398A-470E-81D2-E709F4440831.jpeg
 

Attachments

  • DFE6F1CA-CEBE-4E6B-BA03-2CECECF3B2DF.jpeg
    DFE6F1CA-CEBE-4E6B-BA03-2CECECF3B2DF.jpeg
    85.3 KB · Views: 6
Siku ya Hukumu yule Bosi hakutokea ila sisi washtakiwa wote 12 Tulitokea, MUNGU ni Mwema Tulishinda Kesi na kuachiwa Huru!

Yule Bosi Kakata Rufaa July 23. Kesi Ikapangwa August 24 ila Kwa Bahati Mbaya hatukusikia kesi yetu Kuitwa hivo Imesogezwa mpaka September Mwishoni.

Kule CMA matumaini ya Kulipwa hela zetu hakuna wanatusumbua sana na wanaapa Hatutopata hata 100. Wanasema Kheri wahonge kuliko kutupa Sisi Haki zetu.

Na pia Wafanyakazi Wapya Pale Mgahawani baada ya Sisi kuondoka wanatishiwa kwamba kuna wenzenu hapa walijidai kwenda Kutufungulia kesi Mahakamani, Kesi imeisha na Hela zao wamekosa!! Na anasema kila Tukishinda Atakata Rufaa mpaka Tuchoke wenyewe Tusamehe hela zetu ila Yeye Hatulipi Ng’o!

Wakuu tunaomba Msaada wenu Hapa miongoni mwetu kuna watu wa Vitengo tofauti kulikua na Supervisor,Cashier,Waiter/Waitress, & Cleaners. Wengine Mpaka Leo Hatuna kazi, maisha Magumu tuna watoto, mmoja Single Mother ukiskia story yake machozi yatakutoka, huku tunasumbuliwa Mahakamani, Polisi Walitutenda Kutufungulia Jalada la Kesi wakati Ukweli wanaujua Hatuna Hatia, Watu wengi sana wamedhulumiwa na Hawa Bosi zetu kabla Yetu Sisi na wengine wamelipwa Mishahara Pungufu wakamuachia Mungu
Uliposema single mother nimejiskia vibaya, af ni kama namjua! Jina lake halianzi na herufi M kweli? Sio Muislam?
 
Back
Top Bottom