DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wewe n mjinga Sana

Umenyanyaswa

Umenyimwa stahiki zako

Lakin unatetea upuuzi wa kutoitaja hyo ofisi uliyokuwa unafanyia kazi

Endelea kunyanyaswa hvyo hvyo sababu ya ujinga wako

TAJA HUO MGAHAWA TUCHUKUE HATUA



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Watanzania wanaonewa sio Kwa sababu waajiri ni waonevu Bali ni kwasababu wao ndio wanaruhusu kuonewa
 
Habari Zenu Wakuu.

Mimi na wenzangu 11 tulikua tukifanya kazi mgahawa ambao upo Masaki, unamilikiwa na waarabu wa Yemen. Tarehe 28 January, 2022 ilitokea mzozo kazini majira ya saa 7usiku, baina ya bosi wakike na wafanyakazi huyo mama alitutukana matusi ya nguoni mbele ya wateja wachache waliokuwepo wanamalizia kuvuta shisha, na akasema hatomlipa mbwa yoyote mshahara! Popote tutapoenda kudai haki zetu atasema “hatufahamu” na ataaminiwa sababu hakuna mwenye mkataba nae pia yeye ana hela.

Hio sio mara ya kwanza huyu mama kutukana wafanyakazi wake matusi ya nguoni, alikua akitutukana mara kwa mara tena mbele ya wateja bila kujali chochote. Wateja wengine walichukizwa kwa jinsi huyu mama anavyo mistreat wafanyakazi wake hivo baadhi ya wateja wamekua wakiacha comments mbaya juu ya mistreatment za wafanyakazi huko Google Review kwa muda tofauti tofauti. Ushahidi upo.

Huo usiku wa tukio supervisor alimuomba bosi asituadhibu kwa kutunyima haki zetu za mishahara, sababu wengi wanategemea mshahara huohuo kuendesha maisha yao.

Yule mama alimtukana matusi ya nguoni supervisor na akamfukuza kazi usiku huohuo na kuamriwa atoke nje ya mgahawa. Supervisor akasema ataondoka baada kulipwa mshahara wake yule mama akasema hamlipi hata aende wapi, hana mkataba na yoyote kati yetu huku akicheka! Wafanyakazi wote usiku huo tukawa upande wa Supervisor sababu ni kweli hakuna mwenye mkataba pale na tulichoshwa kutukanwa matusi.

Yule mama akasema subirini hapahapa hamna kuondoka leo nitawaonyesha mie ni nani. Baada ya muda defender la polisi likafika na askari mmoja akatufata na kuuliza kama kuna fujo? Sababu wamepigiwa simu kuja kutuliza fujo na wameambiwa mali zimevunjwa pale mgahawani ila anashangaa kukuta hali ni shwari na hamna dalili ya kitu kuvunjwa.

Naendelea hapo chini kwenye comments👇🏽
Poleni mkuu. Haya mambo kuna kaandiko langu niliongelea umuhimu wa mikataba. Haka hapa 👇🏻👇🏻

Thread 'Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini' SoC 2022 - Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini



Mkuu kwa ushauri nyie kwa pamoja nendeni kwenye vyombo vya kisheria. Maana hwa matajiri wananyanyasa saana watu hususani ukiwa huna mktaba na wanafanya hivyo kuwanyima mikataba wafanyakazi.ili waweze kuwafukuza au kuwaondoa kwa urahisi hili jambo liangaliwe kwa upana zaidi kwa faida ya pande zote.
 
Unashindwa kusaidika sababu unawaficha wasomaji uliowakusudia hapa, upo JF una I'd fake pili wewe unasema uhalisia wenyewe alafu hutaki kutaja jina la mgahawa Yan zile key points unazificha na ogopa asije akatokea mpinzani wako yaan anaenufaika na hyo kesi akakoment kwenye magep uliiacha hapa utakuja kuonekana wewe ulikuwa muhuni tuu na unastahili hayo unayopitia.

Ukweli una njia fupi sema ndo hvyo huwa unauma DUNIA HAINA USAWA.

Unanjaa Kali anatokea Simba Nate njaa Kali umepata nafasi ya kumuua unasema eti siwezi kumuua Simba hata nikimuua siwezi kumla.

Yeye Simba anasema hapa ndio nimepata nyama wacha nipambane nimle huyu.

Au akitokea swala mbele yako wewe nasimba unafikiria Simba atakuachia upate nyama kidogo kwa swala?
Okay Jina La Mgahawa ni “Le Maraheb Restaurant & More” upo Masaki/ Chole Road.

Nimeambatanisha Picha za Mgahawa hapo Chini👇🏽

Tukio Lilitokea January Mwishoni, Osterbay Police Askari wengi wanajua Mkasa wetu, pale Osterbay Police ukisema tu kesi ya wale Vijana 12 walionyimwa Mishahara yao na Bosi wao Mwarabu mwenye Mgahawa Masaki Chole Wanakumbuka!
 

Attachments

  • F015870E-19B4-4DF3-A679-958435E9E6A3.jpeg
    F015870E-19B4-4DF3-A679-958435E9E6A3.jpeg
    39.9 KB · Views: 4
  • FDF9484B-4FCA-4E8D-AF01-7FA564E6A30E.jpeg
    FDF9484B-4FCA-4E8D-AF01-7FA564E6A30E.jpeg
    63.4 KB · Views: 4
Wewe Taja mgahawa Acha uoga.

Unakumbuka kuna demu mnaigeria alisema amebakwa Zanzibar? Hotel ghafla Tu ikashuka ratings kutokana na kelele za watu.

Hichi ndo kinatakiwa kufanyika hapo. Taja mgahawa Sisi twende nao sambamba au ndo ule Le Maraheb?
Ndio huohuo Mkuu nimeambatanisha na Picha za Mgahawa. Waliofanya Kazi Pale ndo Watakua Mashahidi Siku wakiwa Exposed kwenye Media. Wengi wamedhulumiwa hadi Wapishi wa Kibongo. Kutwa watu wanaacha kazi Pale
 
Nia yake atufunge Jela, kule Kazini wanawaambia Wafanyakazi Wapya wenzenu Wapo Gerezani Tumewafunga.

Wanajiamini 100% hawatulipi hela zetu hata twende wapi, na Hofu Yetu wasije kufanikiwa Kutufunga while hatuna Hatia na Hukumu Ilithibitisha hivo. Roho zinatuuma Tulikua tunafanya kazi Mpaka saa 8 Usiku, Maana wana huduma ya Shisha ndo wateja walikua wanachelewa Kuondoka, Kweli Mtu unanyimwa Jasho lako uliolitafuta kwa tabu kurudi Nyumbani usiku wa manane Tunaogopa Kupishana na Vibaka na Mateja, anatukomesha kutunyima haki zetu kisa tu ana hela? Tuende wapi Sauti zetu zisikike? Tukifungwa Jela Wazee wetu na Watoto wetu watakua kwenye hali gani? Hawana Huruma ni Makatili mno hawana Urafiki na mtu hata huyo Mlinzi alietusaliti na Kutoa Ushahidi wa Uongo Alisimamishwa Kazi akabembeleza sana arudishwe maana Maisha yake hana hata sehem ya Kulala, sshv anajuta na muda wowote anaondoka mambo yamemgeukia.
Kwanza pole Sana,haya ndio maisha ya watz kwasasa mwenye pesa ndio Kila kitu,sasa unganisheni nguvu zenu wote 12,shirikisha wanasiasa sasa kwa mkuu wa wilaya,kwa das,kwa RC,barua wizarani Kama zote,yupo tuu ataogopa kumwagiwa ugari wake atasimama na nyinyi mtapata tuu,naongea kwa ushaidi niliwahi kufanya kazi kampuni flani tunakatwa nssf wakti huo kwenye mfuko hakuna kitu inawekwa,tukienda kuliza nssf danadana Kama zote,tulikaa chini tukawaza tukaja na andiko Kali Sana,nakala kwa Kama zote mbona jaamaa aliona kuwapoza wote hawa Bora watupe ela yetuu.utakuja kunishukiru kiongozi.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Aiseeee Mimi huwa sivumiliagi huo Ujinga, Kuna NGO iliwahi kuwa kubwa sana sana Tanza-nia, nilichowafanya.......basi niishie hapa.
Hahahahaha!! Kumbe wewe ndo uliwapasua wale jamaa? Yule aliekua CoP hadi leo anazurura, hana pa kupata kazi sema wakubwa wenzie wizarani wanamtupia vi consultancy vya hapa na pale ndo anaishi.
 
Yule Bosi alivopelekewa Summons ya CMA alishikwa Hasira akasema Hatulipi. Baada siku Kadhaa tukaitwa Polisi Osterbay Jioni, Tukaambiwa Tujiandae kupelekwa Mahakamani kwa Kosa la Kutukana Matusi ya Nguoni na sio kufanya Fujo tena! Tulishangaa matusi gani wakati Sisi ndio Tuliotukanwa Matusi, Siku iliofata Tukapelekwa Mahakamani Kusomewa Mashtaka Kwa Bahati Nzuri Askari Magereza wa Kike wa Mahakama ya Kinondoni aligoma Kubadilisha Mashtaka from kufanya Fujo to Kutukana Matusi.. mpelelezi alidai eti alikosea Kuandika badala ya Matusi akaandika Fujo, Yule Askari wa Kike alimwambia kama umekosea Ingia nao Mahakamani umueleze Hakimu mimi usinitfutie Matatizo!!!
Askari magereza wa kike alisoma hati ya mashtaka mbele ya mheshimiwa hakimu....
 
Back
Top Bottom