Habari Zenu Wakuu.
Mimi na wenzangu 11 tulikua tukifanya kazi mgahawa ambao upo Masaki, unaitwa “
LE MARAHEB RESTAURANT & more” unamilikiwa na waarabu wa Yemen. Tarehe 28 January, 2022 ilitokea mzozo kazini majira ya saa 7usiku, baina ya bosi wakike na wafanyakazi huyo mama alitutukana matusi ya nguoni mbele ya wateja wachache waliokuwepo wanamalizia kuvuta shisha, na akasema hatomlipa mbwa yoyote mshahara! Popote tutapoenda kudai haki zetu atasema “
hatufahamu” na ataaminiwa sababu hakuna mwenye mkataba nae pia yeye ana hela.
Hio sio mara ya kwanza huyu mama kutukana wafanyakazi wake matusi ya nguoni, alikua akitutukana mara kwa mara tena mbele ya wateja bila kujali chochote. Wateja wengine walichukizwa kwa jinsi huyu mama anavyo mistreat wafanyakazi wake hivo baadhi ya wateja wamekua wakiacha comments mbaya juu ya mistreatment za wafanyakazi huko Google Review kwa muda tofauti tofauti. Ushahidi upo.
Huo usiku wa tukio supervisor alimuomba bosi asituadhibu kwa kutunyima haki zetu za mishahara, sababu wengi wanategemea mshahara huohuo kuendesha maisha yao.
Yule mama alimtukana matusi ya nguoni supervisor na akamfukuza kazi usiku huohuo na kuamriwa atoke nje ya mgahawa. Supervisor akasema ataondoka baada kulipwa mshahara wake yule mama akasema hamlipi hata aende wapi, hana mkataba na yoyote kati yetu huku akicheka! Wafanyakazi wote usiku huo tukawa upande wa Supervisor sababu ni kweli hakuna mwenye mkataba pale na tulichoshwa kutukanwa matusi.
Yule mama akasema subirini hapahapa hamna kuondoka leo nitawaonyesha mie ni nani. Baada ya muda defender la polisi likafika na askari mmoja akatufata na kuuliza kama kuna fujo? Sababu wamepigiwa simu kuja kutuliza fujo na wameambiwa mali zimevunjwa pale mgahawani ila anashangaa kukuta hali ni shwari na hamna dalili ya kitu kuvunjwa.
Naendelea hapo chini kwenye comments[emoji1427]
View attachment 2343514