Nia yake atufunge Jela, kule Kazini wanawaambia Wafanyakazi Wapya wenzenu Wapo Gerezani Tumewafunga.
Wanajiamini 100% hawatulipi hela zetu hata twende wapi, na Hofu Yetu wasije kufanikiwa Kutufunga while hatuna Hatia na Hukumu Ilithibitisha hivo. Roho zinatuuma Tulikua tunafanya kazi Mpaka saa 8 Usiku, Maana wana huduma ya Shisha ndo wateja walikua wanachelewa Kuondoka, Kweli Mtu unanyimwa Jasho lako uliolitafuta kwa tabu kurudi Nyumbani usiku wa manane Tunaogopa Kupishana na Vibaka na Mateja, anatukomesha kutunyima haki zetu kisa tu ana hela? Tuende wapi Sauti zetu zisikike? Tukifungwa Jela Wazee wetu na Watoto wetu watakua kwenye hali gani? Hawana Huruma ni Makatili mno hawana Urafiki na mtu hata huyo Mlinzi alietusaliti na Kutoa Ushahidi wa Uongo Alisimamishwa Kazi akabembeleza sana arudishwe maana Maisha yake hana hata sehem ya Kulala, sshv anajuta na muda wowote anaondoka mambo yamemgeukia.