Wale wamiliki na wanapoenda kumiliki magari ya Mzungu tukutane hapa Kwa ushauri na kubadilishana mawazo. Najua ni changamoto Sana kumiliki haya magari hapa Tz kuanzia mafundi,spare na uchumi vile vile. Nina uzoefu mkubwa sana kwenye haya magari. Nimetumia BMW,Mercedes,Audi, Volvo na sasa hivi natumia VW Golf Mk5 2.0FSi. Niulize chochote kuhusu magari haya nitakujibu kwa uzoefu wangu. Karibuni tujadiliane. Jitahidi kununua gari isiozidi miaka 10 kwasababu vitu vingi kwenye gari vinachoka baada ya miaka kumi.