Tunaomtakia mema msanii Diamond

Tunaomtakia mema msanii Diamond

dogo kubwa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2016
Posts
798
Reaction score
695
Ni ukweli usiopingika kuwa msanii diamond platnumz ametuletea heshima kubwa nchini kitaifa na kimataifa.

Binafsi naona toka ametoka kuzindua miaka 10 ya diamond kwao kigoma, kuna jambo haliko sawa, ni kama kila analogusa halitoi majibu chanya.

Aidha ni kwakuwa Yope ilifunika sana so tunahukumu kutokana na yope, au ameingia kwenye biashara umakini unapingua kwenye sanaa ama vipaji vinaibuka kwa kasi.

Tukubaliane kuwa Diamond wa *I miss you* , *number one*, *iyena* sio huyu leo, kama kapoteza mvuto, aidha kiwango kimeshuka, hili nakiona toka atoke kigoma.

Siongei kwa unafiki, na appriciate juhudi kubwa amezofanya but naona kuna jambo haliko sawa, maana pia amekuwa na upinzani mkubwa kati yetu Watanzania tofauti na zamani, au kwakuwa amejiingiza kwenye siasa.

Ni kweli alipokuwa na zari, alivutia kuliko alivyokuwa na huyu Mkenya.

Tumsaidie vipi kijana wetu, ili atumikie vizuri zaidi kipaji chake, nasi tuendelee kuburudika kwa kazi zake.
Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyakati huwezi shindana na Nyakati.

Halafu sasa kwa kuna Harmonize media zote zilizokua na ugomvi na Diamond zinamsapoti harmonize,watesi wake wote wa zamani wapo na dogo na dogo amewakumbatia hili nadhani ndo kubwa linalomtesa maana siku zote bora akushambulie jirani wala hutaumia sana kuliko akikushambulia mwanao maana anakujua angle karibia zote anajua akuguse wapi utaumia.

Juzi Diamond alisapoti album ya Harmonize haijulikani ni kwa nia njema au kinafki lakini dogo wala hakurespond kabisa na hata alipoulizwa amejibu kuwa post na coment nyingi anashindwa kujibu zote lakini ukiangalia post za mwijaku na wengineo amezijibu ila ya boss wa zamani hajajibu tayari stress zinaongezeka kwa mzee chibu ni kitu alishawahi kuimba kwenye UTANIPENDA.

Pia Hamonize nahisi amejua ili azidi kuwa juu lazima autumie msuguano wake na Diamond kufika mbali ndani ya nchi, maana inajulikana wazi yeyote anayeingia bifu na Diamond lazima atapata busta rejea kwa Ali Kiba. Hii vita yao inamuumiza zaidi Ali kiba maana sasa ndo kwaheri atasikika ila si kama zamni watu umakini wameuhamishia kwa Harmonize na pia Diamond anapaswa kujua Harmonize sio kama Ali kiba aliyelala Harmonize ni mjanja anazojua fitna pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda ikawa ni target zake tu mkuu...wasanii wakubwa ni kama timu kubwa inaweza ikakupa matokeo hata katika wakati usiotegemea, kwani tulidhan kama angenunua yope na kutikisa?..though am not his fan but he knows nn afanye kwa wakati upi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnawazaga nini kabla ya kupost wazee?..katika akili ya kawaida aliyepo hatarini zaidi ni Diamond coz list ya wasiopatana nae inazidi kuwa kubwa, bt mnampaga u Mungu mtu kama vile hawezekaniki isn't true..Diamond mwenyewe akiamua kuwa mkweli huenda ALI KIBA ni mmoja wa role models wake (kama unafatilia Muziki tangu zamani itakuwa umeelewa)..mnataka kumfanya Diamond n kama dude kuuuuuuubwa lililoshindkana siyo kweli mzee, nadhani ulipaswa kumfikiria yeye zaidi kwamba vipi mkuu mbona Kila siku maadui wanaongezeka dhidi yako?..

Kiba mwaka wa 17 now kwenye game wamekuja watoto kibao akina jux,Ben pol,belle,Ommy dimpoz ambao kimsingi tulitegemea ndo wangemchallenge diamond bt haikuwah kuwa bt ikawa ALI KIBA ulishajiuliza why?..hata Diamond mwenyewe anajua HATARI na ATHARI za KIBA kwenye bongofleva industry na ndo maana alikuwa akimuandama bt jamaa anakausha Kiba hayupo kuu sababu ya bifu harmo Leo kaachia ngoma 18 yaani albam sasa ngoja Kiba atoe ngoma 1 afu uone impact yake ndo utaelewa vizuri nn namaanisha...mwambieni Mondi apunguze kuvimba hali inazidi kuwa tete.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mnataka Diamond apendwe kivipi zaidi ya sasa au kawaida?

Artist wako wangapi?
 
Mnawazaga nn kabla ya kupost wazee?..katika akili ya kawaida aliyepo hatarini zaidi ni Diamond coz list ya wasiopatana nae inazidi kuwa kubwa, bt mnampaga u Mungu mtu kama vile hawezekaniki isn't true..Diamond mwenyewe akiamua kuwa mkweli huenda ALI KIBA ni mmoja wa role models wake (kama unafatilia Muziki tangu zamani itakuwa umeelewa)..mnataka kumfanya Diamond n kama dude kuuuuuuubwa lililoshindkana siyo kweli mzee, nadhani ulipaswa kumfikiria yeye zaidi kwamba vipi mkuu mbona Kila siku maadui wanaongezeka dhidi yako?.. Kiba mwaka wa 17 now kwenye game wamekuja watoto kibao akina jux,Ben pol,belle,Ommy dimpoz ambao kimsingi tulitegemea ndo wangemchallenge diamond bt haikuwah kuwa bt ikawa ALI KIBA ulishajiuliza why?..hata Diamond mwenyewe anajua HATARI na ATHARI za KIBA kwenye bongofleva industry na ndo maana alikuwa akimuandama bt jamaa anakausha Kiba hayupo kuu sababu ya bifu harmo Leo kaachia ngoma 18 yaani albam sasa ngoja Kiba atoe ngoma 1 afu uone impact yake ndo utaelewa vizuri nn namaanisha...mwambieni Mondi apunguze kuvimba hali inazidi kuwa tete.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnawazaga nini kabla ya kupost wazee?..katika akili ya kawaida aliyepo hatarini zaidi ni Diamond coz list ya wasiopatana nae inazidi kuwa kubwa, bt mnampaga u Mungu mtu kama vile hawezekaniki isn't true..Diamond mwenyewe akiamua kuwa mkweli huenda ALI KIBA ni mmoja wa role models wake (kama unafatilia Muziki tangu zamani itakuwa umeelewa)..mnataka kumfanya Diamond n kama dude kuuuuuuubwa lililoshindkana siyo kweli mzee, nadhani ulipaswa kumfikiria yeye zaidi kwamba vipi mkuu mbona Kila siku maadui wanaongezeka dhidi yako?..

Kiba mwaka wa 17 now kwenye game wamekuja watoto kibao akina jux,Ben pol,belle,Ommy dimpoz ambao kimsingi tulitegemea ndo wangemchallenge diamond bt haikuwah kuwa bt ikawa ALI KIBA ulishajiuliza why?..hata Diamond mwenyewe anajua HATARI na ATHARI za KIBA kwenye bongofleva industry na ndo maana alikuwa akimuandama bt jamaa anakausha Kiba hayupo kuu sababu ya bifu harmo Leo kaachia ngoma 18 yaani albam sasa ngoja Kiba atoe ngoma 1 afu uone impact yake ndo utaelewa vizuri nn namaanisha...mwambieni Mondi apunguze kuvimba hali inazidi kuwa tete.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio uenda, ni ukweli ali kiba ni mwalimu na inspired many diamond akiwemo...juzi kaimba wimbo wa hadithi wa kiba, he has to

Diamond learned and inspired na hao akina Kiba, z anto, marlaw, soggy dog, suma lee... Voice wonder n. K

Ali kiba haendani na upepo ni mtu wa kanuni zake na hachoshi, creative na ana ile ladha halisi na bongo flavor

Ni ali kiba na bob junior ambao walimwambia diamond asi rap aimbe, ni ali kiba kamfundisha face face diamond punches zinakuwaje(tafuta interview ndefu ya ommy dimpo xxl)

Diamond kawekwa au kajiweka juu ambapo inamnyima raha, kiti cha moto... Maana yake kila siku wanakuja artist wapya hauwezi uka wa ignorw, aten, ndela, kusah, onesix... Hauwezi ukawaweka hapa na bado diamond akawa comfortable.. alitaka hilo linamuumiza

Ali kiba ka keep low ila tunaomjuq kutoka nakshi naksho, mac muga, hadithi.... Mpaka leo mshumaa sio wa kuongelewa au kwekwa level moja na akina Mond... kiba sio mtu wa publicity na kiki, kipaji na kazi zinamuweka pale. Haya mambo ya kukosa mvuto kwa sababu hayuko na ZARI ni uthibitisho tosha kuwa Diamond peke yake hawezi
 
mwambieni Mondi apunguze kuvimba hali inazidi kuwa tete.
Mondi alipomwacha Tanasha kuna uzi nilileta hapa na kusema Mondi siku zinavyokwenda kwa tabia zake ataonekana "fake" na itampotezea mashabiki kwenye ukanda wa EAST AFRIKA. Nilipigwa madongo sana hapa kwa hoja zile.

Sasa ukimuuliza Tanasha hili swali la dogo kubwa kwamba kuna jambo kwa Mondi haliko sawa atakupa jibu mpja tu - "Karma." Hii ishu ya Tanasha sasa anasuiri atoe ngoma mpya ndio aizungumzie. Kiki after kiki. Hizi kiki na umri wake na hadhi yake ya kukutana na marais, mawaziri, FIFA nk, haziendani nae tena. Na zinaweza kumpotezea ubalozi kwa baadhi ya makampuni !!!
 
Hii comment ina ukweli kwa zaidi ya 80%
Nyakati huwezi shindana na Nyakati.

Halafu sasa kwa kuna Harmonize media zote zilizokua na ugomvi na Diamond zinamsapoti harmonize,watesi wake wote wa zamani wapo na dogo na dogo amewakumbatia hili nadhani ndo kubwa linalomtesa maana siku zote bora akushambulie jirani wala hutaumia sana kuliko akikushambulia mwanao maana anakujua angle karibia zote anajua akuguse wapi utaumia.

Juzi Diamond alisapoti album ya Harmonize haijulikani ni kwa nia njema au kinafki lakini dogo wala hakurespond kabisa na hata alipoulizwa amejibu kuwa post na coment nyingi anashindwa kujibu zote lakini ukiangalia post za mwijaku na wengineo amezijibu ila ya boss wa zamani hajajibu tayari stress zinaongezeka kwa mzee chibu ni kitu alishawahi kuimba kwenye UTANIPENDA.

Pia Hamonize nahisi amejua ili azidi kuwa juu lazima autumie msuguano wake na Diamond kufika mbali ndani ya nchi, maana inajulikana wazi yeyote anayeingia bifu na Diamond lazima atapata busta rejea kwa Ali Kiba. Hii vita yao inamuumiza zaidi Ali kiba maana sasa ndo kwaheri atasikika ila si kama zamni watu umakini wameuhamishia kwa Harmonize na pia Diamond anapaswa kujua Harmonize sio kama Ali kiba aliyelala Harmonize ni mjanja anazojua fitna pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WCB acheni shobo kwa Harmo..kafanya event yake Elements Salam akaja Harmo na entourage yake wakajikata..tena Domo anapost album yake kamkataa..Harmo hapendagi jokes
 
Back
Top Bottom