Uchaguzi 2020 Tunaoona mbali tulionya jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa

Uchaguzi 2020 Tunaoona mbali tulionya jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa

Kama mada yako haujaileta kwa milengo ya kisiasa/kichama, nachangia kama ifuatavyo;
Kitu nitachoelewa ni kwamba chama cha siasa kinapata rudhuku kadili kinapokuwa na idadi kubwa ya wabunge sina uhakika kama CCM itakuwa imepoteza kuliko kugain.

Lakini pia si mkakati wa kubeza kwa sababu:

1. Imani ya kuchaguliwa kwa chama ambacho mbunge wake amekwenda upande wa pili kuunga juhudi inapungua kutoka kwa wapiga kura.

2. Inaondoa morali miongoni mwa wanachama wa chama cha siasa.

NOTE:
1. SIASA NI SEKTA YA AJIRA KAMA ZILIVYO SEKTA ZINGINE SUALA LA KUANGALIA PROFIT AND LOSS HALIEPUKIKI NA KAMA TUNAVYOONA BAADHI YA WAGOMBEA WAKIJIENGUA NA KUMUACHA MWINGINE KUPITA BILA KUPINGWA.
 
Wadau,

Kuna kipindi ambacho Press conference zilifanyika kwa wingi na nyingi zikiwa kuwatangaza watu waliounga mkono Juhudi JUHUDI. Tunasikia (hatuna ushahidi bado) kuwa kuna watu walilipiwa madeni na wengine kuahidiwa vyeo ili waunge mkono juhudi.

Halmashauri zilivurugwa, mameya wa majiji waliondolewa kwa nguvu, chaguzi ndogo zilifanyika na wabunge walirudishwa kwa hila za wazi (Mollel huko Hai, Mtulia na wengine)

Tunaoona mbali tulionya ya kuwa jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa lakini waliotaka kumfurahisha mkuu walitukejeli. Sasa tufanye evaluation ya uwekezaji huu ulifanywa na Polepole na timu yake kwa kujibu maswali machache yafuatayo,
  1. Je, umerahisisha kampeni?
  2. Tuliowanunua watarudi?
  3. Tumependwa zaidi?

Nadhani wote ni mashahidi wa usemi huu ambao jamaa yetu, ameutumia kuwalaghai wananchi kuwa yeye ni msema kweli. Mtu huyu ni wa ajabu sana maana amekuwa akisahau sana kuwa yeye ni mtakatifu ambaye ataongoza malaika mbinguni, huku akisahau kuwa anawafanya wale wote wanaoishi kama malaika wawe kama mashetani.

Msema kweli mpenzi wa Mungu amekuwa akibadilisha ukweli kuwa ulaghai, kwa mfano, alipokuwa mahali fulani, alisema mgombea Urais wa chama fulani aache kusaka Urais atampa kazi. Huyo aliyeambiwa maneno hayo akamjibu kwamba awape kazi wale anaowaokota majalalani. Msema kweli mpenzi wa Mungu, kama kawaida yake katengeneza ulaghai wake kwamba, jamaa amewaita wafanyakazi wote wa umma wameokotwa majalalani......huyu msema kweli mpenzi wa Mungu ni mlaghai sana sana.
 
Huyo mama ni kondoo alievaa ngozi ya mbwa mwitu. Wao lao ni moja.Nilishangaa sana mnamsifu eti mnyenyekevu.utaishije na shetani alafu wew uwe malaika.

Amedhihirisha rangi zake halisi
 
Nyie maccm Bado tuna mafaili 120 tumefungulia mafaili 10 tu ndani ya siku kumi, mmepoteana, Sasa baada ya uzindui wa Kanda tunaenda kuzunguka nchi rasimi, na kufinguliwa mafaili 110 yaliyobaki
😂😂😂😂 Ila nyie watu bn..!
 
Imetusaidia kuelewa kuwa chadema wananunulika hivyo hawafai kupewa nchi. Kwani mijawapo ya sera yao ni kununulika.

Wagombea uraisi wawili waliyoitikisa CCM ambao ni Lowasa na Slaa ambao ndiyo ilikuwa tegemeo la cdm walinunuliwa kwa kupewa kazi na kupewa ahadi ya kulindiwa mali zao. Hivyo hiyo ilitoa taswila sahihi ya cdm kuwa shida yao ni pesa na si vinginevyo

Wakati tunastaajabu wanunulikaji, tusijisahaulishe mnunuaji nae. Hao wanaonunua nao sio wakyaminiwa hasa hasa ikiwa mkakati unaratibiwa kuanzia juu.

Kwa upande wa wanaonunuliwa linabaki kuwa suala la mtu binafsi.

Msingi imara nnaouamini siku zote ni huu, Usimwamini mwanasiasa yeyote.
 
Niliwahi kusema kuwa wanachofanya ccm kuwanunua wabunge na madiwani ni kutaka kukausha bahari kwa kutumia ndoo ya maji!
Nilisema kuwa upinzani utazidi kukua kila uchwao na ndio ukweli ulivyo!
Ccm wanatumia nguvu kubwa kuliko kipindi chote kuomba ridhaa wakitumia maguvu ya kutisha ili kukusanya watu!
 
Sasa tufanye evaluation ya uwekezaji huu ulifanywa na Polepole na timu yake kwa kujibu maswali machache yafuatayo,
  1. Je, umerahisisha kampeni?
  2. Tuliowanunua watarudi?
  3. Tumependwa zaidi?
Wakikupa majibu ya maswali yako. Unitag.

Kwa maoni yangu uwekezaji huu ni hasara tupu.
 
Niliwahi kusema kuwa wanachofanya ccm kuwanunua wabunge na madiwani ni kutaka kukausha bahari kwa kutumia ndoo ya maji!
Nilisema kuwa upinzani utazidi kukua kila uchwao na ndio ukweli ulivyo!
Ccm wanatumia nguvu kubwa kuliko kipindi chote kuomba ridhaa wakitumia maguvu ya kutisha ili kukusanya watu!
Kama hawataki upinzani, watoe ajira, huduma za kijamii za uhakika, waache upendeleo, wapandishe madaraja watumishi na mishahara, soko la uhakika wa mazao ya wakulima, miundombinu ya uhakika, mikopo kwa wanafunzi n.k upinzani hautakuwepo
 
Mie siongelei atapata kura ngapi, na kuchuja au kutokuchuja, hilo wataamua wananchi. Nimeandika kauli ya mama mwenye wadhifa aliyoutoa hivi majuzi.

Na huu uzi unajadili baadhi ya mambo yaliyofanywa kwa lengo la kuhujumu upinzani.
Unatumia kipimo gani kujua maamuzi ya watu watakayoyafanya?
Kuna watu wana matokeo yao nahisi
 
Kubwa zaidi ni waliopanga mkakati wa kumuondoa TAL, wakajua wameshamaliza mchezo. Hawakuwahi kuwaza kwamba angesalimika na kuja kuwa mwiba wakati huu.

Nimesikitika Mama ambae kidogo alikua na heshima kwa mbali kuropoka kwamba askari waliopitia mafunzo wakikosa mtu kwa risasi tatu wanawajibishwa. Hivi serikali yao yenye dhamana ya usalama wa raia kushindwa kuwatia hatiani au kuwakamata hao wazembe waliofyatua risasi 16 sio fedheha zaidi kwa serikali?
Alafu akasema risasi 16 apingwe mtu amekuwa tembo?. Sasa Nairobi alienda kumuona tembo?. Siasa zimenifanya kugundua kuwa nilikuwa naheshimu asiyestahili hata chembe ya heshima
 
Hii inadhihirisha kuwa elimu ya hapa Tanzania ni ya vyeti na sio maarifa.
Kuna waziri frani aliwahi kusema kuwa"Namshukuru mheshimiwa kwa kunipa nafasi hii, maana nilikuwa jaralani".so ninaimani huwezi kwenda kusomea nje Nchi kama hujapitia pale jaralani. Na bado jaralani inaendelea kutoa sijui niweke neno gani (............)ili liendane na wale waliotwambia umma.

Viongozi hawana maarifa,
 
Tukutane oktoba yatajibika hayo na mengine lukuki.
 
Mnadai Jiwe kapiga vita ufisadi wakati ndiye alikuwa mbele kwenye rushwa na ufisadi wa kununua wanasiasa

i have every reason to prove hakuna mwanasiasa alinunuliwa lakini at the same time inaonyesha jinsi gan chama chenu ni hovyo! kama mada ni kununua then kama mngekua na ushawishi hela zisingewarubuni ila kama mada ni ela basi chama chenu ni hovyo kwamba watu wananunulika na pesa, siasa za dunia pia viongozi wanarubuniwa na pesa wanauza nchi kwahio mkipewa nchi ela ni tosha kuuza nchi!
 
aliyesuka huu mpango sijui nimuitaje. yaani ulikuwa ni mpango wa hovyo ambao haujawatokea katika ulingo wa siasa
 
Wadau,

Kuna kipindi ambacho Press conference zilifanyika kwa wingi na nyingi zikiwa kuwatangaza watu waliounga mkono Juhudi JUHUDI. Tunasikia (hatuna ushahidi bado) kuwa kuna watu walilipiwa madeni na wengine kuahidiwa vyeo ili waunge mkono juhudi.

Halmashauri zilivurugwa, mameya wa majiji waliondolewa kwa nguvu, chaguzi ndogo zilifanyika na wabunge walirudishwa kwa hila za wazi (Mollel huko Hai, Mtulia na wengine)

Tunaoona mbali tulionya ya kuwa jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa lakini waliotaka kumfurahisha mkuu walitukejeli. Sasa tufanye evaluation ya uwekezaji huu ulifanywa na Polepole na timu yake kwa kujibu maswali machache yafuatayo,
  1. Je, umerahisisha kampeni?
  2. Tuliowanunua watarudi?
  3. Tumependwa zaidi?
Hili zoezi lilikuwa la kihuni tu na lilitupotezea fedha za kurudia uchaguzi, hawa watu hawana influence yeyote, kibaya zaidi ni hawa waliopitishwa na ccm kugombea ndani ya ccm wanaonekana wahuni na nje ya ccm wanaonekana washenzi yaani hawauziki,
 
i have every reason to prove hakuna mwanasiasa alinunuliwa lakini at the same time inaonyesha jinsi gan chama chenu ni hovyo! kama mada ni kununua then kama mngekua na ushawishi hela zisingewarubuni ila kama mada ni ela basi chama chenu ni hovyo kwamba watu wananunulika na pesa, siasa za dunia pia viongozi wanarubuniwa na pesa wanauza nchi kwahio mkipewa nchi ela ni tosha kuuza nchi!
mnatumia sana nguvu kuktetea lakini haihitajiki hata degree kujua kama ccm ilinunua wanachama wa upinzani ili kuonesha ni kiasi gani watu wanaunga juhudi za rais. aliyesuka huo mpango atakuwa anajilaumu sana kwa ujinga alioufanya maana uliudhihirishia umma kwamba upinzani umekufa kwasababu ya hao wanaohama
 
Itoshe tu kusema Magufuli ndiye rais wa miaka mitano mingine ijayo
 
Back
Top Bottom