Tunaosimama na Sabaya hatuipingi Serikali, tunapambana dhidi ya dhuluma na uonevu kwa waliojitolea kupambania Taifa

Kwanza mm nashangaa sana, inawezekanaje DC sabaya akafanya yote haya? Ili Hali kuna RC,RSO DGTISS na mamlaka ya uteuze wake ikiwepo? Inamaana hawa wote walikuwa hawajuwi alichokuwa anafanya Kama ni kweli? . Acheni kuwafanya watu hawana akili,, WAACHE KUMTOA MBUZI WA KAFARA BWANA SABAYA.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wote wanaomuongelea vibaya sabaya ni kwamba wanaongea kwa chuki na mihemko ya kisiasa
 
Naona umeamua kutapika upuuzi mtupu
Waliofaidika na matendo maovu ya Ole sasa wanatafuta namna ya kumsafisha. Hakuna aina ya sabuni yeyote unaweza kutumia kumsafisha huyu mtesi wa watu wasiokuwa na makosa. Alishalikoroga, basi na alinywe.
 
Waliofaidika na matendo maovu ya Ole sasa wanatafuta namna ya kumsafisha. Hakuna aina ya sabuni yeyote unaweza kutumia kumsafisha huyu mtesi wa watu wasiokuwa na makosa. Alishalikoroga, basi na alinywe.
Upo sahihi kabisa kiongozi mwacheni anufaike na matendo yake.
 
kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Kila mmoja abebe msalaba wake.
 
Dogo anatoa ruhusa mtu atobolewe miguu kwa misumari kama alivyofanyiwa Yesu halafu mleta uzi anajaribu kujenga hoja kwamba kaonewa!!.

Akifanyacho binadamu siku zote kina ukomo wake.
 
Dogo anatoa ruhusa mtu atobolewe miguu kwa misumari kama alivyofanyiwa Yesu halafu mleta uzi anajaribu kujenga hoja kwamba kaonewa!!.

Akifanyacho binadamu siku zote kina ukomo wake.
Naona leo umeamua kujitenga na kundi haramu la mungiki.
Hongera sana kwa kujikomboa kimawazo.
 
Hivi nyie CCM hamuwezi kushughulikia mambo yenu bila kumtaja Mbowe? Kwani nyie CCM Mbowe aliwafanya nini? Yaani leo mwanaCCM ashughulikiwe halafu sababu iwe Mbowe! Amepata wapi Mbowe hizo nguvu zakuamuru vyombo vya dola vimrushe kichura Sabaya na kumsweka ndani? Amepata wapi hizo nguvu huyu Mbowe tunayemjua, ambaye amefilisiwa mali zake, vitega uchumi vyake mmeviharibu, mlifunga hadi akaunti za familia na biashara zake, halafu leo Ghafla vyombo vya dola vinaitika kwa Mbowe. Basi haya ni mapinduzi makubwa sana. Binafsi nafikiri lile chozi alilotia Sabaya baada ya Mwendazake kufa lilikuwa la hofu ya kuondoka kwa kinga ya maovu yake. alijijua fika kwamba hali itakuwa mbaya kwake.
 
Kumbe ana makosa mengi kiasi hicho. hadi kosa la kulikomboa Jimbo la hai toka utumwani Chadema hadi Kaanani CCM. Ina maana wana CCM wengi walitamani hilo Jimbo liendelee kubaki Chadema? Hoja zingine ni za watoto wa Chekechea
 
Sabaya hawezi kukosa bush lawyers wa kumtetea, hata shetani 😈 anao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…