Tunaosimama na Sabaya hatuipingi Serikali, tunapambana dhidi ya dhuluma na uonevu kwa waliojitolea kupambania Taifa

Tunaosimama na Sabaya hatuipingi Serikali, tunapambana dhidi ya dhuluma na uonevu kwa waliojitolea kupambania Taifa

Kesho Bashite anaweza kuwa mkubwa zaidi kuliko wewe na Gwajima wako
Aaah wapi laws of nature hairuhusu.
Alishafutwa kwenye ulimwengu wa roho,atarudia Kazi yake ya awali kukataa mkaa mbezi.
Uliona wapi gunia la misumari likabebeka
 
Ngoja nikuonyeshe "UNYAMA" angalau huu tu wa Ole Sabaya kisha utasema ni wangapi wengine wameshauriwa kujitokeza kueleza walivyotendwa.
 
Hii ndiyo 255 ukifinya nawe unafinywa mwisho wa siku unakuwa mfinyano tu.
 
Hivi kumbe Ole sabaya alikua anapamba ia Taifa🙄
 
SABAYA FOR CHANGE (S4C)

Another day, better than Yesterday. Katika simu na jumbe nyingi nilizopokea swali lililojirudia mara nyingi ni "Iwapo Sabaya anashtakiwa na Serikali, je nyinyi mliosimama kwa upande wa sabaya mmeamua kupambana na Serikali?"

UFAFANUZI WA KWANZA:
Well, Hatupambani na Serikali, Taasisi, wala Mtu Binafsi. Tunapambana dhidi dhuluma na kile Tunachoamini ni uonevu na kurudishwa Nyuma kwa wale wachache waliojitolea kupambania Taifa hili.

Jambo la kwanza watu waelewe kuwa Sabaya ameshtakiwa kwa tuhuma za Uhujumu Uchumi, kuunda Magenge ya Uhalifu na unyang'anyi wa kutumia Silaha (armed robbery). Makosa haya kisheria ni JAMUHURI dhidi ya MTUHUMIWA na sio Mtu binafsi dhidi ýa Mtuhumiwa, watu binafsi hapa wata- appear Mahakamani kama Mashahidi tu wa upande wa Jamuhuri na hii sio kwa Sabaya pekee bali ni kwa Mtuhumiwa ambaye tuhuma dhidi yake zinadondokea kwenye makosa hayo kwa hivyo hapa serikali imetimiza wajibu wake na sasa ni wajibu wa kila anayeamini Sabaya hana hatia kusimama nae na yule ambaye anaamini ana hatia asimame upande wa Jamuhuri, Machaguo yote Mawili yanaruhusiwa kisheria. Sisi tumechagua "Sabaya" .

MIPANGO:
Katika Dunia hii, Afrika hii na Tanzania hii, mara nyingi wanasiasa Mashupavu kama akina Sabaya hupitia katika masahibu mengi sana na hata kufungwa jela hata kunusurika kuuawa lakini hiyo haiwezi kuzima ndoto zao za kupigania vile vitu vya Msingi wanavyoviamini. Mapambano ya Kisiasa ni kufa na kupona wakati mwingine hata kupoteza Maisha. Wale walileta tuhuma hizi dhidi ya Sabaya sio wajinga, wanajua asili ya makosa hayo na adhabu zake, wanajua wakishinda watakuwa Wamemkomoa na kurudisha nyuma na kukatisha Tamaa watu wote Majasiri aina ya Sabaya.

Ipo dhahiri Tuhuma dhidi ya Sabaya, kuitwa jambazi n.k zilianza kusambazawa na Chadema na Mbunge wa jimbo hilo Mh Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) Tangu Rais Magufuli akiwa Madarakani lakini zimekuja kutekelezwa Mahakamani mara baada Rais Magufuli kufariki. Tumeshuhudia wote namna mambo yalivyokwenda haraka kuanzia Tuhuma mpaka super sonic speed ya DPP Kweka katika swala hili, tena akisafiri mwenyewe kwenda Arusha.

Hakuna asiyejua kuwa Vita ya Sabaya sio Sabaya na Wananchi wa Hai bali ilikuwa ni vita ya Sabaya dhidi ya Wahujumu uchumi wa Hai..Majambazi wa Hai..Magenge ya Uhalifu hai..Wakwepa kodi wa Hai.

MAKOSA MAKUBWA KUMI YA OLE SABAYA
Kosa la kwanza la Sabaya Pale Hai ni kurejesha Ardhi ya Waislam waliyoporwa na Matajiri wa Hai na kuirudisha kwa Bakwata

Kosa la pili la Sabaya ni kurejesha Mashamba ya Ushirika iliyoporwa na matajiri wa Hai na kuwapa wananchi wanyonge walime na kujipatia mlo wao badala ya kukodishwa na Matajiri.

Kosa la tatu la Sabaya ni kufukua mapango ya majambazi wa Magari Arusha, Moshi, Mererani na Dar es salaam yaliyokuwa yanajificha wilayani Hai,

Kosa la nne la Sabaya ni kuwarejeshea Waalimu wanyonge waliyodhulumiwa Pesa zao na Qnet.

Kosa la tano la Sabaya ni kuwapigania wananchi wanyonge waliyoporwa Ardhi yao pale Hai na matajiri wa Kimachame,

Kosa la sita la Sabaya ni kurejesha Jimbo la Hai, Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Vijiji mikononi mwa CCM, na Mbowe kukataliwa na wananchi ktk sanduku la Kura.

Kosa la Saba la Sabaya ni kuongeza makusanyo ya Kodi ya TRA na Kodi ya Halmashauri ya Wilaya na kuwadhibiti wakwepa Kodi huko Hai,

Kosa la nane la Sabaya ni kuitoa Hai toka nambari 64 ktk ukusanyaji wa Mapato mpaka nambari 6 Kitaifa mwaka 2019.

Kosa la tisa la Sabaya ni kufuatilia wanufaika hewa na feki wa fedha za Tasaf pale hai na kukuta Mpaka Marehemu wanafaidika wakiwa kaburini akauliza maofisa wa Tasaf, je huwa wanakutana wapi na Marehemu kuwapatia fedha?

Kosa la kumi la Sabaya ni kuwafanya Wananchi wa Hai waishi bila hofu ya Ujambazi na Magenge ya vibaka na wahalifu.

Sasa Kama huu ndiyo Ujambazi wa Lengai Ole Sabaya basi pengine tukawahitaji majambazi wengi zaidi wa aina hii hapa Tanzania ili tuweze kusonga Mbele.

Watalaam wa Utambuzi wanasema ukimwamisha OCD au Mkuu wa Kituo mahali halafu wanaoshangilia sana ni wahalifu halafu wananchi wanyonge wanasikitika "Jitafakari mara Mbili".

Lengai Ole Sabaya kwetu sisi wengine ni shujaa aliyejitoa maisha na Uhai wake kupigania CCM na Taifa hata kabla hajawa Mkuu wa Wilaya, narudia Lengai ole Sabaya ni kati ya vijana wachache ndani ya CCM ambao wako tayari kupoteza Uhai wao kwa kupigania maslahi ya Chama Cha Mapinduzi.

UKIMYA WA CCM
Kuna akili moja inadhani kwamba kesi ikiwa ya Jamuhuri basi ukiwa Mwana-CCM hutakiwi kujitokeza kusimamia upande usio wa Jamuhuri. Leo tunashuhudia Wana-CCM wengi especially wasaka vyeo na teuzi, na wengine Walinda vyeo wapo kimya wakidhani kuuchuna ni kuifurahisha Jamuhuri!

Sina hakika kama Shaka atakaa ofisini kusoma Magazeti kwa amani wakati Comrade Sabaya yupo Selo kwa Tuhuma zenye Mashaka Makubwa. Siamini kama atasahau kuwa anayopitia Sabaya na yeye alipitia wakati akiwa Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro pale aliposimamishwa kwa Uchunguzi kwa Tuhuma za Uongo aliyopandikiziwa na wabaya wake wa Kisiasa, baada ya uchunguzi akaonekana hana hatia Leo hii ndiyo Katibu Mwenezi wetu Taifa.

Viongozi wetu chama lazima watambue kuwa hakuna siku wapinzani wa CCM watamfurahia kiongozi shupavu wa CCM, viongozi wetu wa chama watambue kuwalinda vijana wanaopigania chama kwa gharama yoyote ili kuwatia Moyo vijana wengine wanaopigania chama kama kuna changamoto za Kimaadili chama chetu kina idara maalum ya Usalama na Maadili kwa Viongozi na wanachama wake warekebishane huko. Kusimamishwa kazi kwa Lengai Ole Sabaya inawezekana ikawa ni njia Bora zaidi ya Kumuimarisha kisiasa.

#Note: Leo wakati huu ambao Sabaya anatuhumiwa tunasikia Mbowe na Chadema yake wanashangilia na kuipongeza sana Serikali, ila kesho Sabaya atakaposhinda Kesi hii kwa kishindo utasikia "Serikali imembeba mtu wakee sio hakiii" na hii ni kwa sababu Watu wana Mikeka mifukoni. Chawa promax Mpo? S4C.
Crap.

Una uhuru wa kusimama na watu wema au na jambazi Sabaya.
 
Mleta mada hivi uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu/ujambazi ni kupambania taifa?
Tuwe serious kidogo akikutwa na hatia, sheria ichukue mkondo wake tu.
 
Nenda kamtetee mahakamani. Hii setikali iliyomuweka ndio inamshitaki wewe ni nani uone anaonewa. Hukosi kuwa ni mnufaika wa matendo ya Sabaya. Hata Hitler na Id Amini walikuwa na mashabiki wao pia haishangazi.
 
Mimi sijui mengi kuhusu uhalifu wake,!! Ila ninachojua, huyu ni mwana ccm, kijana, aliyehudumu kipindi cha magu(marehem).

Ambaye ndo alikua ni mtaji wa kisiasa kwa ccm kwa walio wanyonge
 
Hakuna kesi hapo kwa maslahi mapana ya chama pendwa
 
Kuna clip nyingi zinatokea kwenye mitandao zikimuonyesha Sabaya kama mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akichukua hatua za kutetea umma kwa kuwakamata wahujumu uchumumi na watu dhulumati kwa wanyonge.

Binafsi naamini hatua za kumsimamisha kazi na baadae kumburuza mahakamani sabaya mara baada ya kifo cha Magufuli ni hatua ya mwanzo tu ya kuwarejeshea fisadi na watu dhulumati furaha na ni ishara samia hakuja kwa wanyonge kama alivyokua Magufuli.

Haiwezekani kiongozi aliyekua anatetea maslahi ya umma kama Sabaya aondolewe na kuburuzwa hapohapo mahakamani kwa uzushi tu wa watu wenye kisasi kutokana na utumishi wake.

Picha iliyotokea ni furaha kwa mabwanyenye na watumishi wala rushwa waliyokua wanadhulumu haki za raia wa kawaida. Pia watu hao wanaonekana wanaamini samia ni mtu wao yeye na CCM yake sio tena ya kutetea umma wa wananchi ila wafanyabiashara na fisadi wapenda rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.

Anyway time will tell 2025 wanaccm wataamua tena nani awaongoze maana kura za wananchi kwa magufuli zimeenda naye. So sad.
 
Pole wewe ndio yule baunsa wake mmoja ambaye hatujakukamata. Mpelekee Hennesy Kisongo.
 
Kuna clip nyingi zinatokea kwenye mitandao zikimuonyesha sabaya kama mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akichukua hatua za kutetea umma kwa kuwakamata wahujumu uchumumi na watu dhulumati kwa wanyonge...
Tapeli, jambazi, mbakaji, muuaji, mtesi mahali pake pa kuishi ni gerezani
 
Back
Top Bottom