Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA, nimeshangazwa na kuvunjwa moyo na kauli ya Baadhi ya makada wa chama

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA, nimeshangazwa na kuvunjwa moyo na kauli ya Baadhi ya makada wa chama

Vegetarian

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
654
Reaction score
509
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi mkuu wa chama nimeshangazwa na kuvunjwa moyo na kauli ya Baadhi ya makada wa chama.

Hususan Yeriko, Boniface, Kigaila miongoni mwa wengine. Tangu makamu mwenyekiti TL alivyotangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti hao makada wamejitokeza hadharani na kumshambulia vikali huyo wakili msomi.

Kufuatia kauli hizi zinazoonesha chuki za wazi binafsi zimenishangaza sana na kunivunja moyo na ninadhani Siasa za upinzani hapa mchini bado zina safari ndefu sana.

Kauli ya Yeriko kudai kuwa Uenyekiti wa Chama ni mkubwa kuliko Urais wa nchi ni kauli ya kukatisha tamaa kudhihirisha kuwa CHADEMA wamechagua kuwa wapinzani wa kudumu na hawana ndoto ya kushika dola kamwe.
 
Kauli ya Yeriko kudai kuwa Uenyekiti wa Chama ni mkubwa kuliko Urais
Hata ile kauli ya Yericko Nyerere inayosema kwamba Lisu hana hela kama Mbowe hivyo hawezi kuwa mwenyekiti ni kauli ya kijinga sana.

Huyu Boni Yai naye nilikuwa nadhani ni mpigania haki lkn kumbe ni Kupe (Tick) wa wa Mbowe.

Warogwe kumtoa Lisu waone kama hawajabaki na mbao tu. Lisu ana damu ya kipekee sana.
 
Kiukweli huu uchaguzi umetufunulia sura halisi za viongozi wengi wa CHADEMA ni wachache sana wana moral authority za kupinga kinachofanywa na CCM .CCM wana mapungufu yao lakini angalau kuna balance of power ,kama hizi ndio sura zao halisi viongozi wengi wa CHADEMA itachukua miaka mingi sana CCM kutoka madarakani
 
Hata ile kauli ya Yericko Nyerere inayosema kwamba Lisu hana hela kama Mbowe hivyo hawezi kuwa mwenyekiti ni kauli ya kijinga sana.

Huyu Boni Yai naye nilikuwa nadhani ni mpigania haki lkn kumbe ni Kupe (Tick) wa wa Mbowe.

Warogwe kumtoa Lisu waone kama hawajabaki na mbao tu. Lisu ana damu ya kipekee sana

Hata ile kauli ya Yericko Nyerere inayosema kwamba Lisu hana hela kama Mbowe hivyo hawezi kuwa mwenyekiti ni kauli ya kijinga sana.

Huyu Boni Yai naye nilikuwa nadhani ni mpigania haki lkn kumbe ni Kupe (Tick) wa wa Mbowe.

Warogwe kumtoa Lisu waone kama hawajabaki na mbao tu. Lisu ana damu ya kipekee sana.
Moja kati ya Reasoning ya Kijinga kabisa ,Ni either yeye na wenzake ni watu wa MFUMO wamewekwa kwa Project maalumu pale CDM au wananufaika kifedha kwa kuwepo kwa Mbowe pale
 
Kufuatia kauli hizi zinazoonesha chuki za wazi binafsi zimenishangaza sana na kunivunja moyo na ninadhani Siasa za upinzani hapa mchini bado zina safari ndefu sana.

Kauli ya Yeriko kudai kuwa Uenyekiti wa Chama ni mkubwa kuliko Urais wa nchi ni kauli ya kukatisha tamaa kudhihirisha kuwa CHADEMA wamechagua kuwa wapinzani wa kudumu na hawana ndoto ya kushika dola kamwe.
Mkuu 'Vegetarian', kunradhi sana, kwani mimi nina kushangaa wewe kwa "kuvunjwa moyo" kwa sababu tu watu hohe hahe kama hao wamekuwa na fikra tofauti kuhusu Tundu Lissu.
Hivi wewe hawa unawatambua kuwa ni akina nani hasa katika maswala mazima ya nchi yetu? Kuna mambo yapi ya kipekee unayo yaona wewe kuwa hawa watu wanastahili kuheshimiwa juu yake; na kwamba msimamo wao unahatarisha kwa vyovyote mabadiliko anayo yatafuta Tundu Lissu.

Kuna unalo lijuwa wewe, kwamba bila ya kuungwa mkono na hawa wachumia tumbo Tundu Lissu hawezi kushika nafasi anayo ipigania ndani ya chama? Tujuze basi nasi tuyajue na kuyajadili namna ya kuyatupilia pembeni.

Unajipa presha ya bure tu bila ya sababu yoyote.

Hata hivyo, lakini; wewe huoni faida ya watu wa namna hii kujitokeza mbele kungali mapema kuonyesha uhayawani wao kuliko kujificha na kuendelea kuvuruga chama ndani kwa ndani?
 
Nimeshangaa sana tumepinga sana JPM kuongezewa muda kipindi kile Kessy anpigia chapuo ila sisi tunasema Mbowe aendelee tu maana "hakuna wa kuvaa viatu vyake" yaani chama kina miaka 30 hakina mtu ambaye anaweza kuwa mwenyekiti?

Cha ajabu tulipinga sana CCM kutoa fomu moja ya urais ile 2020 na kusimamisha mgombea mmoja tu wa uenyekiti wa CCM ambaye ni Rais!! Cha ajabu na sisi tunapinga Lissu kuchukua fomu ili Mbowe apite bila kupingwa.

Yaani mambo tunayokosoa CCM ndio tunayafanya huku? Kesho wagombea wa CCM wakipita wote bila kupingwa tutatoa wapi nguvu ya kupinga hilo?
 
Lakini hao jamaa ndio wanaonesha Taswira halisi ya Kamati Kuu
Hiyo "Kamati Kuu" isiyo zingatia matakwa ya wanachama wa chama itakuwa ni kamati kuu ya aina gani hiyo?
Hata hivyo, tusi isingizie Kamati Kuu mambo ambayo tunayahisi tu. Hao wajumbe hawawezi kuwa watu wa kuagizwa tu na watu pembeni wafanye kinyume cha maslahi ya chama chao.
Hata kama waliwekwa kwenye nafasi hiyo kwa mizengwe wakati huo, hali iliyopo sasa itawalazimu watumie akili zao, kuliko za kuazima.
 
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi mkuu wa chama nimeshangazwa na kuvunjwa moyo na kauli ya Baadhi ya makada wa chama.

Hususan Yeriko, Boniface, Kigaila miongoni mwa wengine. Tangu makamu mwenyekiti TL alivyotangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti hao makada wamejitokeza hadharani na kumshambulia vikali huyo wakili msomi.

Kufuatia kauli hizi zinazoonesha chuki za wazi binafsi zimenishangaza sana na kunivunja moyo na ninadhani Siasa za upinzani hapa mchini bado zina safari ndefu sana.

Kauli ya Yeriko kudai kuwa Uenyekiti wa Chama ni mkubwa kuliko Urais wa nchi ni kauli ya kukatisha tamaa kudhihirisha kuwa CHADEMA wamechagua kuwa wapinzani wa kudumu na hawana ndoto ya kushika dola kamwe.
Unakatishwaje tamaa na wajinga hawa ndugu...?

Kinachotakiwa, ni kuwapuuza hao wajinga na kisha kusonga mbele Ili mradi mmesimama kwenye taratibu zinazotakiwa...

Tundu Lissu hawezekaniki wala kubabaishwa na wajinga hao..

Tundu Lissu ni mtu makini mno anapoamua jambo lake....

Akiamua kufanya kitu, hukifanya kwa uzuri na utaratibu wa hali ya juu na huna mahali pa kumkamatia kuwa hapa umekosea....

Mwaka 2020 Magufuli na ubabe wake wote huo alijaribu kila njia kumzuia huyu mwamba asipambane naye kugombea u - Rais....

System nzima ilishindwa kumzuia na wakakutana naye kwenye kampeni na mwisho kwenye sanduku la kura na mwamba (Tundu Lissu) alimwekewa Pombe Magufuli pingamizi kwa kukosea utaratibu wa kujaza fomu kuomba kuteuliwa kuwa mgombea u - Rais....

Ndani ya CHADEMA hii ya leo nani ana uthubutu huo...?

Na katika sanduku la kura la uchaguzi wa 2020, Magufuli aligaragazwa vibaya na mwamba huyu na ushahidi ni kuwa mpaka leo hii hakuna matokeo ya kura za u - Rais Jimbo kwa Jimbo Tanzania nzima kama inavyotakiwa na sheria...!!

Magufuli alitangazwa kibabe tu lakini hakuwa na hajawahi kuwa mshindi kwenye sanduku la kura..!!

Sasa ndani ya chama tu watamwezea wapi huyu jamaa aisee...?

Wawe wanataka au hawaitaki, Tundu Lissu ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA (T) baada ya Freeman Mbowe....
 
Hata ile kauli ya @Yericko Nyerere inayosema kwamba Lisu hana hela kama Mbowe hivyo hawezi kuwa mwenyekiti ni kauli ya kijinga sana.
Sasa mtu mwenye kauli mbovu kama hii utamwelewa kwa kitu gani cha maana maishani mwake.

Kwa bahati nzuri hata siku moja sijapata kumtambua Yericko kwa jambo lolote la maana. Namfahamu tu kwa hilo jina la Nyerere alilo jipachika mwenyewe. Sasa sijui kama hilo nalo alitaka kulitumia kujivimbisha aonekane kuwa mtu wa maana!
 
Lissu asipopita aanzishe Chama chake, sisi tupo tayari.

Lissu ndie mpinzani wa kweli pekee ndani ya Tanzania.
 
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi mkuu wa chama nimeshangazwa na kuvunjwa moyo na kauli ya Baadhi ya makada wa chama.

Hususan Yeriko, Boniface, Kigaila miongoni mwa wengine. Tangu makamu mwenyekiti TL alivyotangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti hao makada wamejitokeza hadharani na kumshambulia vikali huyo wakili msomi.

Kufuatia kauli hizi zinazoonesha chuki za wazi binafsi zimenishangaza sana na kunivunja moyo na ninadhani Siasa za upinzani hapa mchini bado zina safari ndefu sana.

Kauli ya Yeriko kudai kuwa Uenyekiti wa Chama ni mkubwa kuliko Urais wa nchi ni kauli ya kukatisha tamaa kudhihirisha kuwa CHADEMA wamechagua kuwa wapinzani wa kudumu na hawana ndoto ya kushika dola kamwe.
This time tumeweza kuwajua wajasiliamali na wazalendo halisi
 
Back
Top Bottom