Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Hatari sana

Ugonjwa huu si wa kwanza kwetu. Umekuwapo mataifa mengine. Ni mjinga kweli kweli anayeweza kuamini kuwa hadi sasa hakuna taarifa mpya eti kwamba ni wagonjwa wale 8 na vifo vile 5 vilivyotokea na tatizo liliishia hapo.
 
Nchi inaongozwa na chama cha Mazezeta unatajia nini? Usishangae maelfu ya maji ya upako yamepelekwa huko
 
Mama anaupiga mwingi ujue
 
Ebola na Marburg kisayansi (yaani in scientific details) ni magonjwa mawili tofauti. Malaria na Plasmodium kisayansi ni vitu viwili tofauti. Uswahilini plasmodium haina maana yoyote ila malaria.
Ndiyo,ni magonjwa mawili tofauti yasababishwayo na viruses wa aina mbili tofauti,yaani Ebola virus na Marburg virus.
Malaria ni ugonjwa na Plasmodium ni mdudu asababishaye malaria,na ni kweli malaria ndio ifahamikayo mtaani sio plasmodium.

Kwa kuwa umesema mwenyewe hayo ni magonjwa mawili tofauti,unadhani ni sahihi kwamba baada ya wataalam wa afya kuthibitisha kuwa,huo ni ugonjwa wa Marburg na sio Ebola,watangaze kuwa ni ebola hata kama yanafanana kwa asilimia kubwa?

Na sababu kuu ya kuudanganya uma iwe ni kuwa "uswahilini hawautambui marburg bali ebola"

Mkuu,hata kama Marburg virus disease na Ebola virus disease yanafanana kwa asilimia kubwa,lakini huwezi kuita Ebola- marburg na marburg-ebola.Ni magonjwa tofauti,yasababishwayo na wadudu tofauti.
 

Maelezo yako yamezingatia kuwa ni kwa mara ya kwanza Tanzania kuuita Marburg baada ya kuuita ugonjwa huo huo ebola? Kwani ulipokuwa Congo, Uganda, Gabon, Guinea, Sierra Leone, Liberia nk tuliuita je? Tukiaminishwa watu wa huko ni wala popo na nyani?

Umezingatia pia kuwa maneno haya "similar" na "slightly" kama yalivyotumika kwenye mfanano na tofauti hapa chini?

Marburg and Ebola viruses are filamentous filoviruses that are distinct from each other but that cause clinically similar diseases characterized by hemorrhagic fevers and capillary leakage. Ebola virus infection is slightly more virulent than Marburg virus infection."

Bila shaka utakubaliana nami, kwetu ugonjwa ni ebola ila scientifically ni Marburg.

Kama ndivyo faida gani mswahili anapata kwa kumwambia tunakabiliwa na Marburg badala ya kumwambia anakabiliwa na Ebola anayoijua?

Akijua ni ebola si ataacha hata kula nyani na popo? Sasa Marburg atoke vipi? Ugonjwa mpya siyo?

Kwanini tunataka kucheza na lugha ya beberu kuwahadaa watu? Ndiyo maana kwenda robo fainali ni habari kubwa kuliko roho za watu siyo?
 
Duuuh ii nchi inawajuaji wengi!! yani uko kwingine Marburg ndo inaitwa ebola

umesoma afya...ungesoma afya ungeelewa tofauti yao
 
Mkuu,unachojaribu kufanya ni kuhalalisha mada uliyokuja nayo hata kama unajiona haupo sahihi.

Kuna mahali umekubali kuwa ni magonjwa mawili tofauti,lakini bado ulazimisha kuwa yaitwe jina moja.

Hiyo Marburg disease,sisi sio wa kwanza kupata,Uganda walipata,Congo,Ghana,Equitorial Guninea n.k..hizo nchi baadhi walipata Ebola pia.Lakini hawakuwahi kuuita ugonjwa wa marburg kuwa ni Ebola.
 
sasa ata kama uswahilini akuna google ndo Marburg iitwe ebola utakua unajitambua kweli yani ugonjwa mwingine upewe jina la ugonjwa mwingine!!!
Post #27 umeiona? Ninakazia:

"Bila shaka utakubaliana nami, kwetu ugonjwa ni ebola ila scientifically ni Marburg.

Kama ndivyo faida gani mswahili anapata kwa kumwambia tunakabiliwa na Marburg badala ya kumwambia anakabiliwa na Ebola anayoijua?

Akijua ni ebola si ataacha hata kula nyani na popo? Sasa Marburg atoke vipi? Ugonjwa mpya siyo?"
 
punguza ujuaji alafu kubali kujifunza kwani unafikili ebola ni common name yani kama jina la kujitungia.... Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na ebola virus na Marburg ni ugonjwa unaosababishwa na Marburg virus ote awa wanapatikana katika kundi la filovirus ambalo ni kundi la long filamentous virus na wana characteristics ya kusababisha hemorrhage fever yan ni homa inayosababisha kupungua kwa strength ya blood vessels na kupelekea kua rahisi kuburst na mtu kutokwa na damu

sasa kwa lugha rahisi ata kama simba na tiger wanafanana kwa kua ote wapo kwnye kundi moja mtu akishambuliwa na tiger atuwezi kusema kashambuliwa na simba kisa tu watu awajawai kumsikia tiger
 
Ebola ni scientifically na Marburg ni scientifically yani tatizo unaliona jina Ebola limekaa kama local na Marburg limekaa kishua
 

Labda kama ghafla unataka kuiandika historia upya.

Kiswahili ni kifinyu. Ebola ni neno la kigeni lililotoholewa kwenye kiswahili. Likaeleweka na kukubalika na kuwa rasmi kuhusiana na ugonjwa huu.

Marburg ni neno jipya na utohozi wake au kwa kiswahili tungali jina hatuna.

Baada ya siku zote kuelezana ebola ulipokuwa kwingine kote, sasa tunataka kutoka kivingine:

"Kwa ugonjwa ule ule utokanao na kula popo au nyani, wenye dalili zile zile, kujikinga kule kule na madhara yale yale."

Mtawadanganya wajinga werevu watawang'amua.

Cc: sudan iii
 

Post #36 inayo majibu yako. Punguza ujuaji.

Ninakazia:

Baada ya siku zote kuelezana ebola ulipokuwa kwingine kote, sasa tunataka kutoka kivingine:

"Kwa ugonjwa ule ule utokanao na kula popo au nyani, wenye dalili zile zile, kujikinga kule kule na madhara yale yale."

Mtawadanganya wajinga werevu watawang'amua.
 
Ebola ni scientifically na Marburg ni scientifically yani tatizo unaliona jina Ebola limekaa kama local na Marburg limekaa kishua

Kiswahili ni kifinyu ndugu kukidhi mahitaji yote ya kisayansi yaliyopo. Ndiyo maana Kwa kiswahili hata satellite ni satelaiti, Internet ni intaneti, Router ni ruta, Malaria ni Malaria, virus ni virusi nk.

Ndivyo hivyo kwa Marburg, Ebola na jamii zake zote kwa kiswahili ni Ebola. Ndiyo maana imekuwa ikisemwa hivyo hapa nchini siku zote isipokuwa juzi.

Zingatia madhumuni ya lugha ni kuufikisha ujumbe kwa walengwa. Kwa sasa ni kwa watanzania.

Upakeni rangi ugonjwa huu. Uiteni mtakavyo. Anasema mswahili mtamlaumu dobi bure, kaniki rangi yake na la kuvunda halina ubani.

Tatizo si jina tatizo ni ugonjwa.

Tunakabiliwa na ugonjwa mpya. Ugonjwa mbaya wenye kuambukiza kwa urahisi. Kama unaijua ebola basi umeujua ugonjwa huu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…