Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Aunt kwani mada yako umeandikiwa?

FpojyuNWIAAJNp3.jpeg
 
Kwamba:

"Kwa ugonjwa ule ule utokanao na kula vitu vile vile, wenye dalili zile zile, namna ya kujikinga ile ile na madhara yale yale?"
Ugonjwa sio uleule kwani unasababishwa na virusi vya aina tofauti.

Madhara sio yale yale,yanafanana tu kwa asilimia kubwa,lakini Ebola 'unafyeka' kuliko Marburg.

Kwa sasa,kuna chanjo ya Ebola lakini hakuna chanjo ya Marburg.
 
Unataka b iitwe d kwasababu zinataka kufanana
Ninataka satellite iitwe satelaiti, internet iitwe intaneti, router iitwe ruta, typhoid iitwe taifodi, Ampiclox iitwe ampikloksi nk kama ilivyokuwa juzi.

Nina taabu na majina mapya haya kwa mbwa Mzee ghafla.

Kama tulivyouita ugonjwa wenye dalili, visababishi, madhara, nk hizi Congo, Uganda, Gabon, Sierra Leone Liberia, Guinea nk tuendelee hivyo hivyo.

Tukifanya hivyo wananchi wanajua cha kufanya ikiwamo kuacha kula popo au nyani.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ugonjwa sio uleule kwani unasababishwa na virusi vya aina tofauti.

Madhara sio yale yale,yanafanana tu kwa asilimia kubwa,lakini Ebola 'unafyeka' kuliko Marburg.

Kwa sasa,kuna chanjo ya Ebola lakini hakuna chanjo ya Marburg.

Lakini si tulisha kubaliana details ni kwa professionals kama kwenye yale mambo ya Malaria?

Kwa kusema ebola kila mtanzania mara moja atajua tuna nini mlangoni na kuchukua tahadhali husika mapema.

Kwanini kujaribu kufunza mbwa Mzee majina mapya? Hasa hasa kama kila kitu kuuhusu huu ni kile kile kasoro jina la kirusi ambacho nacho ni cha jamii ile Ile?

Ni kweli hatuoni, au tunataka kujificha kwa kufumba macho kama watoto wadogo?
 
Afu juzi BBC Swahili wanatangaza li Antony diallo la star tv likakatiza matangazo ili wa Tanzania wassisikie.

mitanzania inaweza kuwa mijinga ila siyo wote, wengine tunajitambua nini tunafanya

EBOLA IPOOO!!!!
Ingekuwa awamu ya tano angesemwa yule bwana mpaka basi. Ila sasa wapinzani tuko tunarambaaa boke
 
Tumekumbwa gonjwa hatari lenye kuuwa hadi 90% ya wahanga.

Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola.

View attachment 2562190

"Kwamba tumependa kutoliita koleo kwa jina lake."

Maajabu ya Mussa.

Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?

Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili.

Maisha yanaendelea kama vile kila kitu ni sawa.

Ya nini kutoambiana ukweli wote tukajipanga kukabiliana nalo ana kwa ana kama nchi?

Tahadhali iliyotolewa na wizara na kutogusana imo. Inawezekana namna gani kwenye maisha yetu ya kawaida watu kutokugusana masokoni, magulioni, mashuleni, makanisani, misikitini, kwenye mabasi au kwenye madala dala?

Ebola si ya maji tiririka, barakoa, michaichai, matango pori wala upigaji nyungu.

Walioyasikia ya kwetu wameshtuka kuliko sisi wakati sisi tukichukulia poa. Dhidi ya gonjwa hili dunia tayari inatunyanyapaa.

Angalia Rwanda, The New Times - Rwanda on Marburg alert after Tanzania outbreak

Angalia mabeberu, BBC News - Ebola-like Marburg virus kills five people in Tanzania

Coverage zao ni makini na kamilifu (extensive and focussed). Kwetu wenge la awamu ile na njama za mabeberu bado lingalipo.

Kwanini watu wasiambiwe ukweli wote kukiwa kungali mapema? Ya nini kujidanganya?

Magonjwa haya si vita (vya kiuchumi). Ebola si corona ambayo kuuwa kwake kulikuwa hadi 2%. Hiyo hata ikihusianisha uzee na uwepo wa magonjwa mengine pia.

Kwa hakika kwenye ugonjwa huu tusipoamka mapema usanii wetu uliozoeleka, utatuumbua.
Tusipende kujenga taharuki kwa mambo ambayo hatuna uhakika nayo.

Waliopeleka sample maabara chini ya usimamizi wa WHO wameeleza vyema kilichoonekana.

Sisi tulio nje ya maabara tumetengeneza theory mpya ya tunachokitaka na kutamani. Ukiulizwa wewe sample ulichukua wapi na kupimia wapi?

Haya ni magonjwa yaliyo kwenye grupu moja HAEMORRHAGIC FEVER.
Yanabeba sifa zinazofanana ila visababishi ni tofauti.

Tutumie uhuru wetu wa kujieleza vizuri na kutafakari kwa kuhusisha ubongo wetu na maarifa tuliyonayo na si kufurahisha genge. Leta ushahidi wako.
 
Kwa kusema ebola kila mtanzania mara moja atajua tuna nini mlangoni na kuchukua tahadhali husika mapema.
Jaribu kuwaza,uwatangazie watu ni Ebola kumbe sio ni Maburg,wakajua kuwa ina chanjo,wakapata chanjo ya ebola wakidhani wamejikinga.Halafu mlipuko ukaendelea kusambaa,watu haohao wakadhurika na kupata Marburg...kwa ujinsi unavyoweza kuua kwa haraka..unadhani utakuwa umesaidia au umetengeneza tatizo zaidi?

Pia,mambo ya kisayansi,yanaendeshwa kisayansi.Huwezi tangaza Ebola wakati kuna Marburg.
 
Ingekuwa awamu ya tano angesemwa yule bwana mpaka basi. Ila sasa wapinzani tuko tunarambaaa boke
Hii ngwengwe hata angekuwa nani wenye akili zao hawawezi kumvumilia.

Maisha ya watu hayawezi kuwa ya kufanyia mzaha!
 
Marbug ni Marbug na Ebola ni Ebola
Ila Congo, Uganda, Gabon, Guinea, Sierra Leone, Liberia na kote kwingine mliita ebola isipokuwa Tanzania?

Hudhani muanze kurekebisha kwanza kule mlikokuwa mlikosea kama leo ndiyo sahihi sasa?
 
Tumekumbwa gonjwa hatari lenye kuuwa hadi 90% ya wahanga.

Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola.

View attachment 2562190

"Kwamba tumependa kutoliita koleo kwa jina lake."

Maajabu ya Mussa.

Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?

Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili.

Maisha yanaendelea kama vile kila kitu ni sawa.

Ya nini kutoambiana ukweli wote tukajipanga kukabiliana nalo ana kwa ana kama nchi?

Tahadhali iliyotolewa na wizara na kutogusana imo. Inawezekana namna gani kwenye maisha yetu ya kawaida watu kutokugusana masokoni, magulioni, mashuleni, makanisani, misikitini, kwenye mabasi au kwenye madala dala?

Ebola si ya maji tiririka, barakoa, michaichai, matango pori wala upigaji nyungu.

Walioyasikia ya kwetu wameshtuka kuliko sisi wakati sisi tukichukulia poa. Dhidi ya gonjwa hili dunia tayari inatunyanyapaa.

Angalia Rwanda, The New Times - Rwanda on Marburg alert after Tanzania outbreak

Angalia mabeberu, BBC News - Ebola-like Marburg virus kills five people in Tanzania

Coverage zao ni makini na kamilifu (extensive and focussed). Kwetu wenge la awamu ile na njama za mabeberu bado lingalipo.

Kwanini watu wasiambiwe ukweli wote kukiwa kungali mapema? Ya nini kujidanganya?

Magonjwa haya si vita (vya kiuchumi). Ebola si corona ambayo kuuwa kwake kulikuwa hadi 2%. Hiyo hata ikihusianisha uzee na uwepo wa magonjwa mengine pia.

Kwa hakika kwenye ugonjwa huu tusipoamka mapema usanii wetu uliozoeleka, utatuumbua.

Wewe unao uhakika gani kama hiyo ni Ebola??.

Mimi sio daktari lakini nina uhakika kabisa huo ugonjwa uliotokea mkoani Kagera sio Ebola kwani Ebola ni ugonjwa unaoambukiza kwa haraka sana (a highly contagious disease) na ni ngumu kuuficha kipindi unapoambukiza, kwa maneno mengine kama ugonjwa huo ungekuwa ni Ebola basi hadi leo tungesha hesabu vifo makumi au mamia kadha na wagonjwa kadhaa, chukua mfano wa Congo na huko West Africa kipindi Ebola ilipoibuka.

Wizara inaposema huo ugonjwa ni Marburg watakuwa sahihi kwa asilimia kubwa kwani dalili za Ebola na Marburg zinafanana isitoshe watakuwa wamechukua sampuli kuzifanyia Uchunguzi wa kitaalamu.

Mungu ainusuru nchi yetu na magonjwa hususan Ebola, Amin.
 
Kagera ipo karibu na Uganda ambako Ebola ili trend sana hivi karibuni kuuita ugonjwa huo Murburg ni ujinga na ni muendelezo wa serikali ya CCM najua mnakumbuka hata kile kipindi Corona inaingia wakaja na misemo sijui flue kali nk kumbe ni Corona.

Wahudumu wa afya wataopelekwa huko wajiongeze wenyewe maana serikali Yao haiwajali Bali inawafikiria zaid mabeberu watawaonaje wakitangaza ni Ebola.
 
Hii ngwengwe hata angekuwa nani wenye akili zao hawawezi kumvumilia.

Maisha ya watu hayawezi kuwa ya kufanyia mzaha!
Tatizo hujui hatua za ufuatiliaji wa magonjwa ya aina hii na ni kwa kiadi gani WHO inajihusisha kwenye usimamizi wake.

Bado tumesaini mikataba ya kutoa taarifa sahihi kulingana na aina hizi za magonjwa. Migongano mikubwa na kukosa usaidizi ni moja ya vitu unavyoweza kukutana navyo unapojifanya kukiuka ukweli.

Tusikae nyuma ya keyboard na kuanzisha yanayofikirika tu. Nenda kadome jinsi mambo kama haya yanavyofanyiwa kazi kwa level ya nchi, ukanda na dunia.

Kama wewe maabara yako imetoa majibu tofauti yalete.
 
Ila Congo, Uganda, Gabon, Guinea, Sierra Leone, Liberia na kote kwingine mliita ebola isipokuwa Tanzania?

Hudhani muanze kurekebisha kwanza kule mlikokuwa mlikosea kama leo ndiyo sahihi sasa?
Unafikiri ni ubatizo tu watu wanatoa majina?

Mkajifunze kwanza haya mambo yanafanyiwaje kazi ndo uje kujitizama unavyojiaibisha. Pata nafasi ya kujifunza kwanza juu ya jambo kabla ya kulisemea. Mambo mengine yanahitsji maarifa yake si kushupaza shingo tu. Bring the evidence kama si ndoto za mchana.
 
Tusipende kujenga taharuki kwa mambo ambayo hatuna uhakika nayo.

Waliopeleka sample maabara chini ya usimamizi wa WHO wameeleza vyema kilichoonekana.

Sisi tulio nje ya maabara tumetengeneza theory mpya ya tunachokitaka na kutamani. Ukiulizwa wewe sample ulichukua wapi na kupimia wapi?

Haya ni magonjwa yaliyo kwenye grupu moja HAEMORRHAGIC FEVER.
Yanabeba sifa zinazofanana ila visababishi ni tofauti.

Tutumie uhuru wetu wa kujieleza vizuri na kutafakari kwa kuhusisha ubongo wetu na maarifa tuliyonayo na si kufurahisha genge. Leta ushahidi wako.

Tunasikitishwa na neno lenu ovu hili - "taharuki." Neno hili liliasisiwa awamu Ile ya giza. Ni aibu kujaribu kulileta tena katikati ya gonjwa hili leo ambalo nchi nyingine isipokuwa sisi wanalichukulia seriously.

Hata hivyo nikupongeze kuwa ni hatua njema angalau kukiri wazi wazi hivi:

"Haya ni magonjwa yaliyo kwenye grupu moja HAEMORRHAGIC FEVER.
Yanabeba sifa zinazofanana ila visababishi ni tofauti."

Ndani ya lindi la ugonjwa huu umuhimu wa taarifa sahihi hauwezi kudogoshwa. Watu ni lazima wafahamishwe nini kipo mlangoni.

Kiswahili kimekua lini kiasi cha kuweza kudadavua Kwa uwazi kuwa zipo aina ngapi za malaria, ukimwi, au grupu la haemorrhagic fever na vikorombwezo vyake?

Kwa nini mngependa kutuhodhi kiasi hiki kama mbuzi mbuzi tu? Kwamba maisha yetu nani huyo aliye na uchungu zaidi nayo kuliko sisi wenyewe?

Hivi tangia taarifa ya mwanzo wagonjwa 8 vifo 5 hatupaswi kujua maendeleo yoyote? Kwamba ugonjwa umekwisha, unapungua au unaongezeka?

Kwamba hatukupeleka sisi sample? Inahusiana vipi hapa ndugu? Mbona hata tulipo ambiwa sample za mapapai, mbuzi, oil nk zimewahi kuwapo walikuwa tayari kuulizwa kulikoni kutuchukulia poa?

Kama internet ni intaneti, router ni ruta, messenger ni mesenja, hospital ni hospitali, meza ni meza nk, Kwa Nini Marburg siyo Ebola?

Ujanja ujanja huu ni Kwa maslahi ya nani ndugu zangu?
 
Marburg : ni viumbe wanaojitegemea kwa sifa za uhai wao/species.

Ebola: ni viumbe wanaojitegemea kwa uhai wao/species .

Wote hao wanasababisha HAEMORRHAGIC FEVER.

Huwezi kulazimisha Marburg kuwa Ebola.

Nenda kajisomee na ujisomee haya magonjwa na taratibu zake zinavyofanyiwa kazi.
Pata maarifa kabla ya kushupaza shingo. Tukubali kuelimika kwanza ndo tuendelee na tafakari.

Otherwise ni time wastage, review ur understanding.

Una uelewa na jambo unalolizungumzia au ni hisia zako zinakusukuma tu?
 
Back
Top Bottom